carbohydates
Member
- Oct 13, 2026
- 53
- 87
Tanzania inatarajia kuimarisha biashara ya umeme katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika, huku Mkoa wa Rukwa ukitarajiwa kuwa miongoni mwa maeneo yatakayochochea mabadiliko hayo baada ya kukamilika kwa Kituo cha Kupoza na Kusambaza Umeme cha Malangali.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, amesema mradi huo utafungua fursa mpya za kiuchumi kwa kuongeza upatikanaji wa umeme wa uhakika, kuvutia wawekezaji na kuiwezesha Tanzania kuuza umeme kwa nchi jirani, ikiwamo Zambia.
Akizungumza wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho mkoani Rukwa, Ndejembi alisema mkoa huo una mahitaji ya takribani megawati 30, lakini kwa sasa hupokea megawati 16 pekee, hali inayozuia ukuaji wa shughuli za uzalishaji na uchakataji wa mazao ya kilimo na madini.
“Leo hii TANESCO inanunua umeme Zambia, lakini kwa laini hii sisi tutaanza kuiuzia Zambia umeme mkubwa na wa uhakika,” alisema.
Kauli hiyo inaashiria mabadiliko yanayotarajiwa katika biashara ya nishati, kutoka utegemezi wa ununuzi wa umeme kutoka nje kwenda kuongeza uwezo wa kuuza umeme katika masoko ya nchi jirani.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Lazaro Twange, ujenzi wa Kituo cha Malangali umefikia asilimia 85.17, huku kazi za kuwasha na kuingiza umeme zikitarajiwa kukamilika Novemba 2026.
Alisema kituo hicho kinajengwa na kampuni ya TBEA kutoka China kwa gharama ya Sh bilioni 161.9, kikiwa na uwezo wa kupokea umeme wa kilovolti 400 na kuushusha katika viwango vya kilovolti 220, 66 na 33.
Kituo hicho kitakuwa na transfoma nne na njia nane za kusambaza umeme katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Rukwa, hatua inayolenga kuboresha upatikanaji wa nishati na kuongeza uwezo wa kusambaza umeme kwa watumiaji.
Chanzo: Radio Saut FM