Uranium kuchimbwa namtumbo tutafaidika au ni kama north mara?

drgeorge

Member
Jun 22, 2009
99
23
Wakiongea kwa mbwembwe wakuu wa wilaya waliotembelea huko wilaya ya Namtumbo Ruvuma na kuwaambia watanzania kuwa hakuna madhara yoyote, Binafsi siwaelewi wao ni wataalamu wa Nishati na Madini hasa Uranium? Binafsi siamini kama tutakuwa salama sana. Kama North Mara tu watu wameathirika na maji machafu ya sumu kutoka mgodi wa Dhahabuhivi kweli tutafaidika au ndio kama Heroshima na Nagasaki?

Kama Tembo wanasafirishwa hadi Vietnam na Twiga wetu wanapanda ndege, hivi kweli tunaweza kudhibiti na kuhakikisha usalama wa raia wetu.

Halafu TBCCM badala la kutaja asilimia ya mrahaba wao wanataja kiasi cha fedha, mmmh. Wenye taarifa na utaalamu hasa juu ya athari na namna ambavyo imethibitishwa kuwa usalama utakuwepo tusiathirike na mionzi atujuze. Binafsi nina wasiwasi sana na usalama wetu.
 
Ni mambo ya kitahaira tu, hao jamaa wanachimba hayo ma-uranium kwa miaka 15, lakini sisi Tz tutapata jumla ya kama USD 600 mil., kwa kipindi chote icho. Kwa hakika inatupasa tuitoe madarakani haraka iwezekanavyo...
 
Back
Top Bottom