Uchaguzi 2020 Tanzania kama Ulaya inawezekana: Ni huyu Rais Magufuli tena 2020-2025!

The Giantist

JF-Expert Member
Dec 12, 2018
214
86
Wajinga ni watu wazuri mara mia zaidi, kuliko mtu mpumbavu. Kwanini mjinga... Mjinga ni mzito katika kuelewa na kujifunza jambo. Lakini ukifanya juhudi kidogo za kumuelimisha atakuelewa na kwa hakika hata jambo lenyewe hilo atalielewa kwa uzuri. Hii ni kinyume kabisa na mtu mpumbavu na upumbavu. Upumbavu hautoki kwa kufundishwa ama kuelekezwa. Mpumbavu hataki kufundishwa na hata hapendi kuelekezwa, yeye ni anajifanya tu mara zote. Upo usemi usemao, "Kuna mtu ambaye hajui na hajui kama hajui, huyo ni mpumbavu, achana naye atakupotezea muda." Kwahiyo, faida kubwa utakayoweza kuipata kwa mpumbavu ni kukupotezea muda tu na ukajikuta huwezi tena kwenda mbele. Hili ni tatizo kubwa!

Sijasoma sheria, lakini nimejifunza kupitia waliosoma sheriia. Wao wanasema kabla hujachanhia mada iwayo yote, huna budi ku-declare interest. Hivyo basi nami sina budi kufanya hivyo, mimi ni muumini wa siasa ya CCM, na mara nyingi utanipata Lumumba au White House Dodoma. Karibuni sana.

Ndugu zangu, nimeanza na maneno hayo ili kwamba tupate kuwekana sawa mapema kabla sijaingia kwenye msingi hasa wa ujumbe huu kwenu. Sasa, kutokana na juhudi za serikali zetu tangu Uhuru hata sasa, chini ya uongozi wa Chama Cha Mapinduzi na vyama vya TANU na ASP huko nyuma miaka ya 1977 kurudi nyuma kidogo mpaka miaka ya 1961. Serikali zote hizo zimeweza kupunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya wajinga, mpaka ninayaandika ni dhahiri shahiri kuwa idadi ya wajinga imepungua sana.

Na kwa bahati mbaya sana, wakati serikali ilipokuwa kwenye vita dhidi ya adui ujinga, ndipo upumba*** nao ukaanza kuchomoza katika mgongo wa wapinzani kwenye vijichochoro vya vyama vya upinzani. Ni wapinzani wengi ndio ambao wameathirika na upumba***. Sasa nataka niusemee huo upumba*** wenyewe hasa. Ili nisiwapotezee muda wenu wa kufanya kazi kwa ajili ya ujenzi wa nchi, sina budi kueleza kwa uchache na kwa ufupi sana.

Jana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, alipata kusema hivi, akiwa anaongea na wanaCCM wa wilaya ya Dodoma Mjini mkoani Dodoma, na mimi nikiwa mmoja wao mahali hapo. Yeye alisema "Nataka Tanzania iwe kama ulaya, nataka nchi hii iwe kama ulaya, sisi ndiyo tuwe tunatoa misaada na uwezo tunao na kikubwa ni mipango na mipango imeshatengenezwa na Chama changu Cha Mapinduzi." Mwisho wa kunukuu.

Maajabu ya upumbavu wa wapumbavu, ulianza mara tu baada ya Rais kuyasema maneno hayo. Ijapokuwa Rais aliongea mambo mengi sana, lakini wapumba*** waliyasikia machache, na kwa vile walisikia machache, basi wakaibuka na hoja zao nyepesi katika hayo machache waliyoyasikia. Sikuwashangaa katika hoja zao nyepesi ambazo walizianzisha tangu Rais akiwa Rufiji, Mkuranga na hata alipokuwa njiani kuelekea Dodoma. Lakini katika hili la jana, nimeamua nitoke niseme. Hatuwezi tukaacha upumbavu uendelee kuathiri jamaa hawa, na kwamba upumbavu hauwezi kuondolewa darasani. Hivyo basi, ni matumaini yangu kuwa jukwaa hili ni mahsusi kwa ajili ya kuondoa upumbavu huo.

Kwanza ni lazima sisi watanzania tumpongeze Rais wetu Dkt. Magufuli na kwamba ni lazima tujivunie kuwa na Rais wa aina hii. Ni ukweli mchungu kwa jamaa zetu hawa CHADEMA kusikia kwamba Rais Magufuli ni miongoni mwa Marais wa mfano wa kuigwa ndani ya Afrika na Dunia. Na hiyo ni kutokana na ujasiri wake, uchapa kazi wake, uadilifu wake, na kwa usimamizi wake mzuri katika kusimamia rasilimali za nchi kwa maslahi ya wananchi na Taifa kwa jumla. Na huyu ndiye Rais wetu Dkt. John Magufuli, ni wajibu wetu kumuunga mkono katika juhudi zake za ujenzi wa Taifa ili kuleta maendeleo ya wananchi. Na kubwa kabisa ni kuhakikisha kuwa nchi yetu Tanzania inafikia hatua ya kujitegemea yenyewe kiuchumi.

Hivyo basi kauli aliyoitoa Rais Magufuli, ni kauli ambayo sisi kama sehemu ya msingi ya nchi hii, hatukupaswa kuibeza hata kidogo. Ni kauli ya ushindi, ni kauli yenye kujenga fikra sahihi za kizalendo huku tukipigania lengo moja, ambalo litaipa heshima Tanzania yetu pamoja na sisi wenyewe. Hatupaswi kuibeza kama ambavyo wapumbavu wanafanya na wanaendelea kufanya hata sasa. Mtu kusimama hadharani na kuanza kuibeza kauli ile, ni ishara ya wazi kuwa hujui shabaha ya nchi yako, na kwamba hujui unapokwenda na kwa hakika hata tulipotoka kama Taifa ni wazi kuwa hujui. Na huo ndio upambavu wenyewe.

Binafsi nimefurahi wa sana na kauli hiyo ya Rais na kwa kusema ukweli ninakubaliana naye kwa kiasi kikubwa. Ni kauli iliyotoka kwa Kiongozi mwenye maono makubwa na mwenye dhamiri nzuri ambayo anataka itekelezwe ili tuiishi ndani ya Tanzania ambayo Viongozi wetu waasisi waliitamani iwe Tanzania siku moja!

Mhe. Rais Magufuli amesema mambo matatu muhimu na mazito na ambayo kupitia hayo ndio inatoa ujumbe mkuu wa maneno yake hayo. Kwanza, neno kama; pili, neno msaada na tatu, ni neno mipango!

Kwa hiyo, yeye anasema "nataka Tanzania iwe kama ulaya, nataka nchi hii iwe kama ulaya..." Ni dhahiri shahiri kuwa hatujafika pale ambapo kama nchi tunataka kufika. Wote tunafahamu hali ya utajiri kwa mataifa ya ulaya. Ni mataifa makubwa yaliyopiga hatua kubwa katika maeneo yote yanayogusa maisha ya watu kisiasa, na kiuchumi. Hapa Rais wetu, ndio kusema alikuwa anaonesha njia hiyo, na mahala ambapo ndio kusudio letu kufika. Na kwa hakika ni katika kuukuza uchumi wa nchi yetu. Na hilo lipo wazi, tunaona miradi mikubwa ambayo kukamilika kwake ndio itaonesha uelekeo kwa urahisi sana kwa mfano mradi wa maji wa Mwl. Nyerere, Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR), kukuza sekta ya utalii, usafirishaji wa nchi kavu na anga n.k. Na kwa kusema ukweli, huyu Rais Magufuli ndiye aina ya kiongozi ambaye watanzania na Tanzania inamtaka sasa katika zama hizi za uchapaji wa kazi. Kiongozi mwenye maono makubwa ya kuleta mabadiliko makubwa katika Maendeleo ya nchi.

Rais Magufuli anaendelea kusema, "sisi ndiyo tuwe tunatoa misaada na uwezo tunao...". Kwanza ni vizuri ikafahamika kuwa neno msaada lina maana sawa na maneno kama kitu anachotoa mtu mmoja ili kutimiza haja ya mtu mwingine. Hivyo kumbe mtu unaweza ukatoa kitu cho chote labda hata fedha kwa lengo la kumtimizia mtu mwingine haja yake/zake. Kwa jinsi hiyo kama nchi, Rais anaposema maneno hayo ni dhahiri kuwa anayasema kwa kuwa ameona uwezo huo tunao, na anaonesha wazi kuwa zipo rasimali za nchi ambazo ikiwa tutazitumia vema pamoja na uwepo wa njia za uchukuzi nzuri na kuwepo kwa nishati ya umeme wa kutosha, tunaweza siku moja kuwapa msaada watu hawa wa ulaya ikiwa watahitaji kutoka kwetu. Na sio lazima msaada huo utolewe mwaka kesho. Maendeleo ni mchakato, na shabaha yetu ni kuzisaidi nchi za ulaya siku moja. Lakini pia, huwezi kutoa msaada kwa jirani kama hujajitosheleza. Kwa hiyo, Rais anaposema maneno hayo ni dhahiri kuwa anatafuta kuitosheleza Tanzania na watanzania, ili ile ziada itakayobaki tuweze kuwasaidia na wenzetu wengine. Haya ndio maono ya kiongozi wa wanadamu ndani ya nchi ni lazima awe nayo. Ni Dkt Magufuli tu kwa sasa ndiye atakayeweza kuyafanya hayo, katika kuweka misingi imara ya kufikia huko, na kwa hakika hakuna mwingine nje yake na nje ya CCM!

Mwisho Mhe. Rais Dkt John Magufuli, anasisitiza namna au njia ambayo tukikubali kufanya kuanzia sasa, basi tutafikia azima hiyo. Hapa anasema "..... kikubwa ni mipango na mipango imeshatengenezwa na Chama changu Cha Mapinduzi." Unaposema mipango ni wazi kuwa inamaanisha upangaji, na neno upangaji lina maana sawa na maneno mchakato wa pamoja wa kuunda na kudumisha mpango, na mchakato wa kiakili wa kufikiri mpango na mchakato wa shughuli zinazotakikana kuunda lengo linalotamaniwa katika kiwango fulani. Kwa hiyo, ni sehemu ya msingi ya tabia ya uerevu. Mchakato huu wa kufikiria ni muhimu kwa uumbaji na unoaji wa mpango, au uunganishaji wake na mipango mingine, yaani, inaunganisha utabiri wa maendeleo pamoja na maandalizi ya mazingira ya jinsi ya kukabiliana nayo.

Ili uanze kutekeleza jambo lo lote lile, huna namna ya kuanza bila kuweka mipango yako chini. Ndio kusema tunaanza na mipango na kisha utekelezaji katika kuelekea kutimiza jambo na kuleta matokeo ya kukuza uchumi wa nchi na hatimaye nchi kuwa kama ulaya. Haitoshi kuwa kama ulaya pekee yake lakini pia na kuzisaidia nchi za ulaya ikiwa watataka tuwafanyie hivyo. Na mpango ambao mhe. Rais Dkt Magufuli anausemea, ni ilani ya CCM. Ilani Safi na inayoonesha njia kwa mapana yake. Tunataka Rais na Chama ambacho dira yake na malengo yake na mipango yake ni kwa maslahi ya nchi na Dunia pia. Rais huyo ni Dkt Magufuli na Chama hicho ni CCM.

Baada ya kusema hayo, ni matumaini yangu kuwa ufipa watajitahidi kuachana na upumbav** wao, ijapokuwa najua ni wagumu kuelewa ndani ya muda mfupi, lakini hata wasipotaka kufahamu sasa watafahamu kwenye sanduku la kura.

Tanzania kama ulaya inawezekana!

#Ni huyu huyu Magufuli tena 2020-2025
Sauti ya Mdodomia
07/08/2020.
 
Sawa umewataja wajinga na wapumbavu lakini umewasahau washamba, limbukeni na madikteta uchwara...nakukumbusha tu wala sina nia mbaya The Giantist
 
Ulaya kuna utawala wa sheria, huwezi kumhonga polisi wala hakimu ili ushinde kesi.

Watendaji wasiowajibika wanaweza kuwajibishwa na wananchi hata ikiwa ni Rais.

Kila mhimili una mipaka yake, hakimu hatoi hukumu kwa amri kutoka juu.

Ni Yeye 2020 atatuletea utawala unaoheshimu sheria.
 
Ulaya kuna utawala wa sheria, huwezi kumhonga polisi wala hakimu ili ushinde kesi.

Watendaji wasiowajibika wanaweza kuwajibishwa na wananchi hata ikiwa ni Rais.

Kila mhimili una mipaka yake, hakimu hatoi hukumu kwa amri kutoka juu.

Ni Yeye 2020 atatuletea utawala unaoheshimu sheria.
Dah. . ni kazi na bata banaaa
 
Yaani umeandika mengi lakini ni ujinga mtupu,kama wewe mleta mada ndo mwandishi basi ni mjinga na mpumbavu wa mwisho,unasema watu wamechukua kipengele kidogo kwenye hotuba yake,huyo ni mkuu wa nchi tutachukua si kipengele tu,nukta kwa nukta ,aya na herufi hadi herufi.

Wewe na wananchi wengine mnaokubali kudanganywa kwamba Tanzania itakuwa kama ulaya ndani ya miaka tano ndo wapumbavu na wajinga mnapelekwa kama kondoo machinjioni kwa kampeni za comedy na ahadi za kijinga.

Miaka 5 sliyomaliza hajabadili Tanzania kama ulaya halafu anakuja tena eti miaka 5 ikayo ndo atabadili,ni wajinga na wapumbavu kama wewe mnaokata viuno humu ndo mnaamini hizo ngonjera za huyo comedian
 
Sasa
IMG_20200808_083637_084.JPG
 
Kwa wale tuliofatilia mwenendo wa siasa za upinzani vs chama tawala tangi 2000 mtakumbuka kuwa hoja za upinzani zilitegemea mapungufu ya utawala uliopo.

Katika utawala wa Mkapa upinzani ulipiga kelele suala la ubinafsishaji holela pamoja na viashiria vya rushwa, mfano katika mikataba ya uwekezaji, n.k.

Wakati wa Kikwete vivyo hivyo. Na naweza kusema utawala wa Kikwete was the most corrupt regime of all.

Cha kushangaza tone ya criticism ya upinzani kwa utawala wa Magufuli ni tofauti na ile tuliyoizoea tawala zilizopita. Kwa vile the man is doing a great job kwenye inshu pengine za muhimu katika kutengeneza misingi ya maendeleo ya kweli, the man hapingwi kwa hoja zile zile za 2000-2015. Upinzani umekuja na hoja (ironically) ambazo kama Magu akiwasikiliza, utawala wake utakuwa/utarudi kuwa sawa na ule wa Mkapa na Kikwete.

Wasiwasi wangu ni kwamba Magufuli atakuwa exhausted na hizi criticism by the time anamaliza mda wake kiasi kwamba aone namna bora ya kuondoka ni kuwa succeeded na mtu soft soft. Namna ile ya Kikwete alivyochoshwa na criticisms akaona njia bora ni kumweka mtu tofauti nae yaani Magufuli.

Hii nchi needs leaders wa aina ya Magufuli (ana Mapungufu yake, lakini yanavumilika kulinganisha na strength zake) kwa miongo kadhaa mbele. Simaanishi kuongezewa muda -- ila hatuhitaji viongozi wapuuzi tena style ninazozisikia nikimsiliza Membe (mtu anayewaza nchi haiwezi kwenda bila wazungu) au Lissu (mtu asiyejua anataka nini -- nae ana vidalili vya kuhisi wazungu ni kila kitu katika maisha yetu).
 
Hii nyie ccm mnataka miaks mingapi ili mtimize kile mlichopanga?.
Hata tuwape miaka 1000 bado mtakuja na ahadi zilezile tu.
Ifike mwisho muache uongo na mkubali mmeshindwa kutupeleka mbele kama Taifa.
 
Back
Top Bottom