Urambo mashariki kwa Mh.Sitta mambo yameiva

Urambo mashariki kwa Mh.Sitta mambo yameiva

MZEE WA USSOKE

Senior Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
120
Reaction score
42
Nawasalimu wote watanzania wenzangu, Amani iwe kwenu:

Jimbo la Urambo mashariki limeongozwa kwa miaka mingi sana na Ndugu Samuel Sitta,

Na sasa ametangaza kutogombea na anataka kumwachia jimbo mke wake Mama Magreth Sitta,nadhani dhana za kuachiana madaraka kifamili imepitwa na wakati..

Ashukuliwe Mungu kwa kumwinua kijana wetu Derrick Luhende( mjukuu wa mzee maarufu hapa ussoke marehemu T.S.Mapolu ) Kijana mcha Mungu,mpambanaji,mwenye msimamo usioyumba...ameamua kutangaza Nia ya kulichukua Jimbo hili Iwapo tu Chama chake cha Chadema na Umoja wao wa Ukawa utampa ridhaa....

Na lengo lake kubwa ni jimbo la Urambo litoke mikononi mwa CCM, kama ikiwa yeye au yeyote Yule atakayepewa nafasi atashirikiana naye kuleta ushindi..

Hili ni tumaini jipya la Urambo ,tumuunge mkono

Dr.Martin Luther aliwahi kusema " ni heri mtu mmoja akakutia moyo wakati wa shida,kuliko watu wengi kukushangilia wakati wa mafanikio"

" Mbunge wa watu kwa ajili ya watu"

Karibu kwa ushauri,maoni,mapendekezo,na kukosolewa pia.

Mungu awabariki nyote
 
Wewe ndio Derrick Luhende au kakutuma kupima upepo? Kweli kura za wanna urambo zitapatikana jjf?
 
mkuu hapo ussoke kwa miaka mingi mkekuwa waoga wa wageuzi mtaepuka vip watu kupewa chunvi na kofia za ccm?
 
Na Msafiri mtemelwa Vp, hagombei tena

Nafasi kwa ukawa kufanya tathmini haraka wamsimamishe kijana wa chama kipi na awe anakubalika kwa vijana na kina mama wa Urambo . Awe na ushawishi mkubwa na anae yaweza majukwaa bila kusahau kauwezo ka kulipa gharama ndogo ndogo. Wakishampata huyo ukawa iteue makada wachache watakaoweka kambi jimboni na kuanza kueneza elimu ya uraia. Wasipombana ki sawa sawa huyo mama akitumia wingi wa wamama wenzie anaweza kuwatoa knock out hivi hivi. Utaratibu huo utumike pia kwenye majimbo mnayotaka kuyachukua toka ccm. Hao hao makada ndio watumike kukagua fomu za wagombea wa ukawa kubaini makosa na hiyo itapunguza mapingamizi hasa kwa nafasi za madiwani watakaogombea.
 
eti anamuachia mke wake ebo!!!! Kwani hilo jimbo ni mali yake??? Nitashangaa saaana wananchi wa urambo mkimchagua mama sita kwa maana mtakuwa mmekubaliana na usultani wao, Tanzania sio mali yao au sehemu ya uk oo wao bali tanzania ni mali ya watanzania ... Hapa mnatakiwa muonyeshe ushupavu.
 
eti anamuachia mke wake ebo!!!! Kwani hilo jimbo ni mali yake??? Nitashangaa saaana wananchi wa urambo mkimchagua mama sita kwa maana mtakuwa mmekubaliana na usultani wao, Tanzania sio mali yao au sehemu ya uk oo wao bali tanzania ni mali ya watanzania ... Hapa mnatakiwa muonyeshe ushupavu wa hali ya juu.
 
muwe sawa wanyamwez tupen ccm kulee msikae kama wadigo,wazigua,wasambaa wanguu na waluguru,wakwere,wapogoro,wapare,wazaramo. haya ndo makabila magumu sana kuelewa kuwa ccm ni jinamizi baya sana kwa maisha yao.
 
6 na mama mtoa rushwa waende zao salama, kama hawajafaidika, they will never satisfy any more
 
...naunga mkono juhudi za ukombozi wa taifa na wana urambo...
 
Aliacha udokozi aliokuwa anafanya akiwa shuleni any way watanzania ndiyo wenye maamuzi hasa wakaazi wa jimbo hilo ngoja wakati ufike.
 
Wakati ukifika vijana wengi wenye sifa watajitokeza na kugombea wapiga kura wataamua lakini hawa wakujitokeza mapema kama lowasa mara nyingi ni matapeli wa siasa.
 
Ukoo wa Mapolu?? Hapati kura Wanajisikia sana wale, kwao usoke mlimani pale.
 
Wewe ndio Derrick Luhende au kakutuma kupima upepo? Kweli kura za wanna urambo zitapatikana jjf?

Kwani Mkuu tayari kura zimeanza kupigwa? Sijaona mahali mleta mada kaandika kwamba anaomba kura?!!
 
Back
Top Bottom