Engineer Pamela Maassay; mwakilishi sahihi Ubunge wa Afrika Mashariki

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
ENGINEER PAMELA MAASSAY: MWAKILISHI SAHIHI UBUNGE WA AFRIKA MASHARIKI.

Na Mashiku Chokala,

Baada ya majina ya awali ya Lawrence Masha na Ezekiah Wenje kukataliwa bungeni katika kinyang'anyiro cha ubunge wa Afrika Mashariki (EALA) kupitia Chadema, hatimaye Chama hicho kimekubali kuweka uwiano wa jinsia na kupeleka upya majina bungeni yakiwa na uwakilishi wa mgombea wa kike.

Barua iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa bunge Ndugu Thomas Kashilila ya April 28 mwaka huu, ilikitaka Chadema kufanya mchakato wa ndani na kupeleka upya majina ya wagombea kabla ya tarehe 03 mwezi May mwaka huu. Tayari Kamati kuu ya Chadema imeitwa kukutana huko Zanzibar tarehe 2 mwezi May ili kupitisha majina ya wagonbea na kupelekwa upya bungeni tarehe 3.

Kwa upande wa wanaume majina yatakayopelekwa ni yaleyale ya awali yani Lawrence Masha na Ezekiah Wenje. Kwahiyo wanaume hawatachukua fomu katika zoezi hili linaloendelea. Kwa sasa wanatafutwa wagombea wa kike ambao majina yao yataunganishwa na ya kina Wenje kwenda bungeni kupigiwa kura.

Wapo wagombea kadhaa waliojitokeza kujaza fomu wakiomba nafasi hii. Ukweli ni kwamba karibu wote wana sifa za kutosha kuwafanya kuwa wabunge wa EALA kupitia Chadema na wakawakilisha vizuri taifa letu.

Kwakuwa kamati kuu itakaa Zanzibar na haitawahoji wagombea, badala yake watapiga kura kwa kusoma CV za wagombea nimeona si vibaya kuzungumzia Mhandisi Pamela Maasay mmoja wa wagombea waliochukua fomu kutaka nafasi hiyo ya uwakilishi wa nchi.

PAMELA NI NANI?
Kwa kifupi naweza kumwelezea kama binti wa kitanzania, Mhandisi kitaaluma, mwanaharakati wa mazingira na haki za binadamu, mwanasiasa, kijana msomi na mwenye bidii.

ELIMU:
-Pamela ni msomi wa Shahada ya Uzamili katika elimu ya Afya ya Jamii (Masters of Public Health) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 2015 - 2017.
-Ana shahada ya kwanza ya Uhandisi wa kemikali (Bachelor degree in Food and Biochemical Engineering) kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam 2007 - 2011.
-Ana stashahada ya Sayansi ya Maabara (Diploma in Laboratory Science) kutoka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), 2003 - 2006.
-Ana Stashahada ya Sayansi ya Mazingira (Enviromental Science) kutoka Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Atlantic, 2011 - 2013.

UZOEFU WA KAZI:
-Kwa sasa Engineer Pamela anafanya kazi kama Mhandisi wa Kemikali (Biochemichal Engineer) katika Kiwanda cha vinywaji baridi cha Cocacola Kwanza, kilichopo jijini Dar Es Salaam.
-Kabla ya hapo amewahi kufanya kazi kampuni ya uzalishaji bidhaa za plastic ya Jumbo na kiwanda cha dawa cha Shelys Pharmaceutical.

UZOEFU WA KISIASA:
Pamela kwa sasa ni Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA) jimbo la Kawe na Mjumbe wa baraza kuu la Chadema Taifa. Pia ni mjumbe wa Kamati Tendaji ya BAVICHA Taifa. Vilevile amewahi kushika nafasi nyingine za kisiasa nje na ndani ya Chadema, ikiwemo ubunge wa bunge maalumu la Katiba.

Pamoja na mambo mengine Pamela ameshiriki kufanikisha kampeni za ubunge za Mhe.Halima Mdee tangu uchaguzi wa mwaka 2010 na hata wa 2015. Alishiriki katika timu iliyoandaa kitabu cha Mhe.Halima Mdee kilichozungumzia mafanikio ya miaka mitano ya Halima Mdee katika jimbo la Kawe. Kitabu hicho kilizinduliwa mwaka 2015 na Mhe.Freeman Mbowe, kilisaidia sana wananchi kujua kazi za maendeleo zilizofanywa na mbunge wao.

Nje ya Kawe, Pamela ameshiriki siasa za kitaifa katika matukio mbalimbali. Mwaka 2015 wakati wa uchaguzi mkuu, baada ya kufanya kampeni Kawe, alishirikiana na vijana wengine akina Nusrat Hanje, Malisa, Dr.Cyrilo n.k kuzunguka nchi nzima kuwanadi wagombea ubunge katika majimbo 20 nchini. Program hiyo iliandaliwa na vijana hao wenyewe, wakitumia rasilimali zao wenyewe na kufanikiwa kuzunguka mikoa yote nchini katika majimbo 20 waliyoyachagua.

Hii ilikua ni commitment ya hali ya juu sana kwa vijana kuamua kutumia gharama zao, na muda wao kuzunguka nchi nzima kuwafanyia kampeni wagombea ubunge. Ziara hii iliyotumia jumla ya siku 32 ilihitimishwa jimbo la Vwava wilayani Mbozi, ambapo kati ya wagombea 20 waliofanyiwa kampeni na vijana hawa, 13 walishinda ubunge.

Pamela pia ameshiriki kukijenga Chadema katika operesheni ya "Chadema ni msingi" katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwemo jimbo la Kawe na Rombo mkoani Kilimanjaro.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, Pamela alikuwa miongoni mwa wajumbe wa kamati ya Chadema iliyotengeneza program maalumu ya kuchukua mawakala wa uchaguzi kutoka vyuo vikuu. Kupitia program hiyo Pamela alifanikiwa kusimika wanafunzi wa vyuo vikuu kuwa mawakala majimbo ya Ubungo na Kawe.

Pamela pia alishiriki kuwania Ubunge wa viti maalumu kupitia jimbo la Kawe na kushinda katika kura za maoni. Japo hakuteuliwa lakini aliendelea kuwa mvumilivu kwa chama akishiriki shughuli mbalimbali za ujenzi wa chama.

UZOEFU KIMATAIFA:
Kwa kuwa moja ya vigezo vya ubunge wa Afrika Mashariki ni kuwa na uzoefu na masuala ya kimataifa, Pamela ni moja ya wagombea wachache wanawake wenye uzoefu mkubwa wa masuala ya kimataifa. Pamela ni balozi wa program ya kuandaa vijana viongozi barani Afrika iitwayo Young African Leaders Initiative (YALI) iliyoasisiwa na Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama.

Pamela pia amewahi kuteuliwa katika kamati ya maandalizi ya kongamano la vijana duniani (World Youth Day 2016), lililofanyika nchini Poland tarehe 26 hadi 31 mwezi July mwaka jana na kuzinduliwa na Papa Francis. Kongamano hili kubwa zaidi duniani, lililokutanisha vijana zaidi ya laki 5 wa kikristo kutoka nchi mbalimbali duniani, lilifanyika mji wa Kraków, nchini Poland, ambapo Pamela alikuwa sehemu ya kamati ya maandalizi (organizing committee) ya kongamano hilo.

Si hivyo tu bali pia Pamela ni mjumbe wa bodi wa taasisi ya kiutu ya Colour of Hope ya nchini Ujerumani inayotoa misaada mbalimbali ya kiutu kwa watu waliokumbwa na majanga. Taasisi hii imeshiriki sana kusaidia watu wa Haiti walipokumbwa na tetemeko. Pamela ameshiriki mara kadhaa vikao vya taasisi hiyo nchini Ujerumani akiwakilisha Tanzania.

HARAKATI ZA MAZINGIRA:
Pamoja na uzoefu wake mzuri kisiasa na masuala ya kimataifa, Pamela ni mwanaharakati mzuri wa mazingira. Aliamua kusoma stashahada ya Sayansi ya Mazingira ili awe balozi wa kuisaidia dunia kuepukana na changamoto za mazingira zinazotukabili.

Kupitia ubalozi wa YALI, Pamela amefanikiwa kuanzisha kampeni ya kitaifa iitwayo [HASHTAG]#TanzaniaGoesGreen[/HASHTAG] ambapo kupitia kampeni hiyo miti mbalimbali imefanikiwa kupandwa maeneo mbalimbali nchini, katika jitihada za kupungiza hewa ukaa duniani kufikia mwaka 2025 kama yalivyo malengo ya Umoja wa mataifa.

Jijini Dar Es Salaam kampeni hiyo ilifanikiwa kupanda takribani miti 1,000 maeneo mbalimbali, huku mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Tanga na Singida kupitia taasisi mbalimbali za kiraia (CSOs) zikiunga mkono kampeni hiyo ya Pamela ya [HASHTAG]#TanzaniaGoesGreen[/HASHTAG] na kuhamasisha upandaji miti maeneo mbalimbali. Mkoani Tabora kampeni ya [HASHTAG]#TanzaniaGoesGreen[/HASHTAG] imewezesha miti kupandwa kando ya barabara kuu za mkoa huo, hasa barabara yotr ya Tabora - Urambo (yenye kilomita 110) na Tabora - Nzega (kilomita 120).

UZOEFU AFRIKA MASHARIKI:
Pamela ni mjumbe mwalikwa wa Mtandao wa mazingira Afrika mashariki (East African Network for Environmental Compliance & Enforcement) ambapo ametumia nafasi yake hiyo kuzunguka nchi mbalimbali Africa Mashariki kuhamasisha utunzaji wa mazingira.

Pamela pia ni mjumbe wa Kamati ya wataalamu (Technical Committee) ya Wizara ya Viwanda na Biashara ya kuregulate viwango vya bidhaa kwa nchi za Afrika Mashariki. Kwa sasa kila nchi ina standards zake katika kuregulate bidhaa. Ndio maana kwa Tanzania Shirika la viwango (TBS) linaweza kupitisha bidhaa lakini ikienda Kenya ikakataliwa kwa kuwa ipo chini ya viwango vya Kenya. Au ya Kenya iliyopitishwa na KBS ikaenda Rwanda ikaonekana ipo chini ya kiwango.

Kwahiyo serikali za nchi zote 5 za Afrika Mashariki zimeamua kuunda Kamati ya wataalamu (Technical Committee) ambayo itakuja na mapendelezo ya standards za bidhaa kwa nchi zote za Afrika Mashariki ziwe za kufanana. Pamela ni mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo kutoka Tanzania, walioteuliwa na Wizara ya viwanda na biashara.

Pia Pamela amewahi kushiriki katika makongamano mbalimbali ya kitaaluma katika nchi za Afrika Mashariki kama vile Mkutano mkuu wa wataalamu wa Afya (African Health and Scientific Conference) lililofanyika mjini Kampala nchini Uganda, March 25 mwaka 2015.

Pia amehudhuria Mkutano mkuu wa kimataifa wa Wahandisi wa kemikali (International Conference on Chemical and Biochemical Engineering - ICCBE) lililofanyika mjini Nairobi, Kenya tarehe 2 hadi 3 November, 2016.

Si hivyo tu, Pamela ameshiriki kuandaa mkutano mkuu wa vijana wasomi wa vyuo vikuu kuhusu Uhuru (African Students For Liberty) uliofanyika Chuo Kikuu cha Catholic University of Eastern Africa mjini Nairobi, Kenya uliofanyika tarehe 15 na 16 mwezi May mwaka 2015.

USHIRIKI WAKE BUNGE LA KATIBA:
Pamela alikuwa mbunge wa bunge maalumu la Katiba. Licha ya kwamba hakuwa mwakilishi kutoka chama chochote cha siasa lakini aliungana na wabunge wa UKAWA alipoona Katiba ya wananchi inasiginwa.

Pasipo kujali kupoteza mamilioni ya fedha, au kitoeleweka na taasisi iliyomtuma, aliamua kususia bunge hilo na kutoka nje na hakurudi tena. Hii ni commitment ya hali ya juu mno hasa ukizingatia kuwa uwakilishi wake haukua unatokana na chama chochote, hivyo angeweza kubaki bungeni akapata fedha na asiwajibike popote. Lakini akaamua kuacha "mamilioni" ya pesa ili kutetea na kulinda maoni ya wananchi yaliyokuwa yakisiginwa na chama cha mapinduzi.

HITIMISHO:
Ikiwa Chadema itaamua kutupa watanzania zawadi ya muwakilishi bora, mwakilishi sahihi, na mwakilishi makini wa bunge la Afrika Mashariki basi itatupatia Engineer Pamela Maasay. Ana Elimu ya kutosha, ana uzoefu wa kutosha katika siasa na masuala ya kimataifa, pia ni mtu aliyejitoa kwa ajili ya chama kwa jasho na damu.

Kwa kifupi ndiye mgombea pekee ambaye amepitiliza vigezo vilivyowekwa, (A candidate with a lot of added advantage). Naamini akipewa nafasi ya uwakilishi wa EALA, atatumia uzoefu wake na elimu yale nzuri kuisaidia Tanzania kupiga hatua kubwa maendeleo baina ya nchi za Afrika Mashariki.

Chadema tupeni Engineer Pamela Maasay. Tanzania inamtaka Engineer Pamela Maasay. Msomi, Mwanaharakati, Mwanasiasa kijana, Mcha Mungu. EALA MPYA, FIKRA MPYA.!

Mashiku Chokala,
Katibu Mwenezi - Chadema Ilala
01/05/2017.
tmp_10101-IMG-20170501-WA00101175693831.jpg

tmp_10101-IMG-20170501-WA0009119777280.jpg
 
Ok ana CV nzuri ila kwenye mambo ya uongozi CV itakuwa haina tija kma hatoweza kutumia elimu yake kuleta mabadiliko kwenye eneo husika maana bunge la Afrika mashariki hatushindanishi CV ila hoja zenye tija kwa maslahi mapana ya taifa letu hivyo hilo ndio la muhim zaidi all in all best wishes kwake
 
View attachment 503476
View attachment 503477
HAFAI: WOTE WATAPIGIWA KURA YA HAPANA
 
Naona unapaa siku hizi kikazi, na kutumwa kuwapigia debe. Hongera kwa kujiongeza najua kuwa paparazi haitoshi. Nasuburi kuiona sura yake kuleeeee

Naona anapenda kuwa na watu tu pembeni yake, ataweza mwenyewe.

Huna picha zingine au tuwafundishe majambo?
 
...kwanini wanawarudisha watu waliokataliwa??...kwanini wasteue majina mapya??....kuna watu kama David Kafulila ambao ni makini sana na wanajua hata mambo ya uchumi na wana experience kubwa ya kuwa bungeni....hao kina Masha wakikataliwa tena itakuwaje?
 
Back
Top Bottom