Urais wa Samia; Tumkunje angali mbichi

Urais wa Samia; Tumkunje angali mbichi

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
16,863
Reaction score
62,389
Vipo viashiria kwa mbali vinaonyesha kuwa rais Samia ameanza kukizoea kiti (Hili ni jambo zuri), na pia ameanza kukipenda kiti (hili siyo jambo baya) ila ameanza kutamani kukilinda kiti kwa gharama yoyote (hili ni tatizo)

Tatizo ninaloliona ni kuwa hii dhana ya ya tatu ya kutamani kukilinda kiti kwa gharama yoyote ndiyo mwanzo wa yeye kuanza kupiga danadana hitajio la msingi la wananchi juu ya namna wanavyotaka nchi yao iongozwe, yaani hitajio la katiba mpya. Hii ni ishara mbaya kabisa ya kiuongozi, kwa sababu inaonyesha dhahiri kuwa na yeye hana tofauti na watangulizi wake ambao Ukweli wanaujua kuwa katiba hii siyo miafaka katika mazingira ya sasa ya kisiasa na kiuchumi, lakini waliendelea kuikumbatia tu kwa sababu uwepo wa katiba mpya unaweza kutoa HAKI nchini ambazo zinaweza kupelekea wao kushindwa chaguzi na wakakosa means za kulazimisha ushindi wao binafsi na chama chao cha CCM.

1. Kauli ya rais hakosei
Samia alitoa kauli hii, wengi tunaweza kuichukulia juujuu, lakini hii kauli inamaana kubwa mbaya sana, ina maana kuwa yeye anaweza kufanya lolote katika nchi na litakuwa sahihi tu, asihojiwe! Ipo haja ya kumkatalia kwa nguvu rais pindi tukiona anakwenda chaka, tumueleze wazi kuwa kwenye suala kadha wa kadha hauko sahihi, mfano ni katika suala hili la kuzuia mikutano ya vyama vya siasa ya wazi nchi mzima kinyume cha sheria.

2. Kupiga danadana katiba mpya
Kauli ya Samia kuwa suala la katiba mpya tumpe muda ajenge uchumi kwanza, ni kauli iliyopakwa mafuta kumaanisha kuwa licha ya hilo suala la katiba mpya kuwa ni la msingi kwetu sisi wananchi lakini kwake yeye kama rais siyo la kipaumbele, na huenda anamaanisha kuwa halitaki ila tu anatumia "tafsida" ili kumpaka chura lipsitiki. Hapa binafsi nina maswali yafuatayo kwa Samua mwenyewe.

a) Kama anajua kuwa uchumi ni kipaumbele kuliko Katiba mpya, kwa nini yeye binafsi alishiriki kikamilifu kwenye mambo ya katiba mpya mwaka 2013 kwa kuomba nafasi ya kuwa Makamu mwenyekiti wa bunge la katiba?, Kwa nini asingejiweka pembeni na masuala ya katiba mpya wakati huo na badala yake kushauri serikali ijikite katika yjenga uchumi?

b) Yeye sasa hivi ni mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi, na Chama kiliweka suala la katiba mpya kwenye ilani yake ya mwaka 2015, Kama Samia anadhani Uchumi hauwezi kujengwa sambamba na katiba mpya, kwa nini alizunguuka nchi nzima nwaka 2015 kuinadi Ilani hiyo yenye kuelezea kuwa uchumi utajengwa na katiba mpya itapatikana?

3. Rai yangu kwa rais Samia, Kumbuka kuwa mchakato wa katiba mpya ndiyo ulioinua nyota yako na ndiyo utakaoizima
Kabla ya mchakato wa katiba mpya 2013-2014 hakuna aliyekuwa akimjua Samia kama mwanasiasa wa kiwango cha Kitaifa, Ila uongozi aliouonyesha mwaka huo katika bunge ka katiba ndiyo uliompa nafasi ya kutambulika kitaifa na hata kwenye system kuwa huyu anafaa. Sasa ni ajabu sana kwa mtu ambaye alishiriki kwenye jambo muhimu kama hilo kuanza kuleta excuse ya kuliahirisha. Yaani kwenye hili la suala la Katiba mpya kitu ambacho rais Samia anakifanya ni sawa na mwanamke anayesaka mtoto halafu baada ya kupata mimba anataka kuitoa!. Hoja ya katiba mpya ndiyo mimba, na katiba ndiyo mtoto mwenyewe!. Tunataka Samia akamilishe kazi aliyowahi kushiriki kuifanya, kazi iliyoibua nyota yake ya kiuongozi nchini, yaani kuwapatia wananchi katiba nzuri na bora

4. Rai kwenu Wazalendo wa nchi hii
Ndugu zangu, tusikubali nchi hii kuwa ya kidikteta, tunapoona chembechembe za udikteta ikiwa ni hata kauli ya kuteleza ya kiongozi tusikae kimya, maana tukikaa kimya wataanza kuamini katika invincibility kitu ambacho ni illusion na mdogomdogo wataanza kujenga tabia za udikteta. Kwa hiyo tumkunje rais Samia angali mbichi kabla hajanogewa sana na mamlaka makubwa anayopewa na katiba hii. Tukimuacha akakomaa katika ulevi wa madaraka utokanao na katiba hii atatuzingua sana huko mbeleni maana wahenga walisema, Power corrupts absolute power corrupts absolutely.

5. Mwisho kabisa hoja ya katiba mpya haiwezi kufa mpaka katiba mpya ipatikane
Na hili suala wadau tumeshalijadili sana kuwa.

1. Katiba mpya ni takwa la kisheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2012, tunataka rais atekeleze sheria.

2. Katiba ya sasa ya Muungano na ya Serikali ya Mapindizi ya Zanzibar vinapingana, kwa mfano kwenye muundo wa serikali ya SMZ, Masuala ya mahakama ya rufani etc. Hizi katiba mbili haziko in sync. Sasa hatuwezi katika nchi kuwa na katiba inayopingana na katiba nyingine, huo ni uendawazimu

3. Katiba mpya imewahi kuwemo kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM, Sasa haiwezekani chama kilekile kilichowahi kunadi ilani, kitumie ahadi hiyo kupata kura halafu baada ya hapo kikatae ahadi yake ya kwenye ilani yake kwa hoja kuwa ahadi yake ya mwanzo ilikuwa inachelewesha kujenga uchumi, kwa hiyo eti sasa tujenge uchumi kwanza huo ni ulaghai wa wazi mbele ya wananchi, tunataka CCM iwe na soni!.

4. Katiba mpya iliyo bora zaidi ndiyo itakayolinda Haki zetu, uhuru wetu binafsi, itasimika fairness katika nchi, na itatulinda dhidi ya uwezekano wa kupata kiongozi dikteta akatuvuruga!.
 
Muacheni mama achape kazi ainue uchumi mambo mengine baadae
 
Kama unadhani ni rahisi kuleta katiba mpya hebu waambie CHADEMA warudishe kipengele cha ukomo wa madaraka na kile cha kumwajibisha mwenyekiti.

Na kama unadhani ni rahisi kuvumilia ukosoaji, mkosoe Mbowe.

Mwanasiasa anayependa kukosolewa nchi hii ni wachache sana, kina JK huko upinzani afadhali Zitto.

Usisingizie wananchi ndio wanahitaji sana katiba mpya wakati agenda zingine mnazotaka kuziweka ni za maslahi ya kisiasa.

Mwishowe, kama mnahitaji mafanikio shirikisheni watu.

Tatizo ninaloliona, kuna watu ambao ni kama wamepoteza mwelekeo ndio wanajifanya wanaharakati. Ndio maana agenda zao kila siku zinabadilika.

Wakati kina Nyerere wanapambania uhuru walihakikisha makundi yote yanawaunga mkono
  • Wasanii
  • Wanaharakati
  • Jumuiya za kimataifa
  • Wasomi
  • Viongozi wa dini
  • Watawala wa kimila
  • Vyama vya wafanyakazi

Na haya makundi mpaka leo, CCM bado imeyakumbatia.

Kwa upande wa pili, leo wanaojifanya ni wapinzani na wanaharakati wamekuwa wabinafsi kupindukia, kazi yao imekuwa ni kutukana huyu msaliti, yule msaliti. Wao ndio wanajiona wema sana na watakatifu sana.

Na kwamba wao ndio mabingwa wa kupigania haki, wengine wote hawafai🤣

Anyway, sisi wengine yetu macho. Maana hakuna mwanasiasa masikini.

Wengi ni matajiri na wamechuma utajiri wao chini ya utawala huu huu mbovu wa CCM. Sasa hivi wanafurahia maisha huku wakitudanganya sisi ili maisha yetu yawe mazuri tunahitaji katiba mpya au kuwapa wao madaraka.

Akili kichwani.
 
Hauna mtu aliyemzuia kuchapa kazi, tunataka tu katiba mpya iliyobora
Tumpe mda kwanza unaona hali ya hewa ilivo ,uchumi umeshuka,macorona kama yote.
Mama yetu ni msikivu sana.hana kiburi,hana majivuno.
Ni imani yetu muda ukifika atafanya
 
Kama unadhani ni rahisi kuleta katiba mpya hebu waambie CHADEMA warudishe kipengele cha ukomo wa madaraka na kile cha kumwajibisha mwenyekiti.

Na kama unadhani ni rahisi kuvumilia ukosoaji, mkosoe Mbowe.
Mambo ya Chadema waachie wao, sisi tuzungumze mambo ya nchi kwanza. Nchi haina chama bali wananchi wana vyama.
 
Kama unadhani ni rahisi kuleta katiba mpya hebu waambie CHADEMA warudishe kipengele cha ukomo wa madaraka na kile cha kumwajibisha mwenyekiti.

Na kama unadhani ni rahisi kuvumilia ukosoaji, mkosoe Mbowe.
Umekimbia hoja iliyoko mezani kisa Chadema, this is not right, humtendei haki mleta mada.
 
Daah!!! Mzee yule alikuwa Anatuambia Anainyoosha Nchi na Mama anasema Anataka Kuisimamisha Nchi Kiuchumi kwa Katiba ile ile Inayompa Inayotoa Mamlaka ya Kufanya Lolote na Chochote; So bado tuko Njia panda na Tulidhani Nchi Ilinyooka Kumbe Ilikuwa ni Bado..
 
Unaposema samaki akunjwe angali mbichi ni sahihi lakini pia tukumbuke huyu samaki alikalia hicho kiti bila kutegemea, hivyo kuanza kwa kusua sua ni kawaida kwa mtu wa aina hii.

Lakini pale anapoanza kuonesha kuizoea ofisi, na mazoea yenyewe yakawa na viashiria vya kwenda kinyume na sheria, hapo kweli lazima tuwe wakali kumrudisha njiani.

Ila tukumbuke, huyu alikuwa msaidizi wa yule aliekuwa hafuati sheria, inawezekana kabisa kuna mambo kadhaa aliyojifunza toka kwa mtangulizi wake.

Bahati mbaya mambo yenyewe ndio hayo negative ya kuipa kisogo sheria na yote yanayotakiwa na wananchi kwa ujumla ili kukilinda chama chake, hivyo kumbe huyu samaki anaweza asiwe mbichi kama tunavyofikiri bali ameshakauka.
 
Mpaka mtatajana ni kwanini mlishirikiana kumwondosha.

Katiba mpya ni mawazo ya upande mmoja ambao haujawahi kushika dola.

Katiba ya Warioba na ile pendekezwa haikuzingatia maoni ya wale ambao hawakuwa wanachama wa vyama pinzanihivyo ilikosa uhalali kutumika popote Tanzania.

Katiba huwa haitende haki ila watu wanaohudumu kwenye taasisi hiyo ndio kichocheo cha kutenda haki, ila pia ndio chanzo cha kuteteleja katika matengamano kwa kuwa kila mmoja anakuwa na uhuru uliopitiliza kiasi ambacho kinaharibu udhibiti wa mienendo ya tabia za kiharifu kwa kisingizio uhuru wa kujieleza na haki za binadamu.

Suluhisho ni kuwa na serikali moja, Rais mmoja, makamu wa Rais mmoja, waziri mkuu (Bara) na waziri kiongozi(Visiwani) basi zingine hizo ni mbwembwe zisizo na tija kwa maendeleo ya nchi na watu wake.
 
Na nchi inahitaji usalama, afya, kuheshimiana, ajira, biashara, uchumi, miundombinu, uwajibikaji.

Hivi vitu ni zaidi ya katiba mpya
Huko kuheshimiana hakuwezi kuwepo kama sheria za nchi hazifuatwi, think critically before you type.
 
Na nchi inahitaji usalama, afya, kuheshimiana, ajira, biashara, uchumi, miundombinu, uwajibikaji.

Hivi vitu ni zaidi ya katiba mpya
Katiba bora inaharakisha hivyo vitu kupatikana.

Kuna direct association kati ya uongozi bora na siasa safi, na kuna association kati ya uongozi bora, Siasa safi na maendeleo.
Sasa Katiba nzuri ndiyo inayoweza kuguarantee siasa safi nchini na wala si hisani binafsi ya mtawala. Think big!
 
Katiba bora inaharakisha hivyo vitu kupatikana.

Kuna direct association kati ya uongozi bora na siasa safi, na kuna association kati ya uongozi bora, Siasa safi na maendeleo.
Sasa Katiba nzuri ndiyo inayoweza kuguarantee siasa safi nchini na wala si hisani binafsi ya mtawala. Think big!
Siku zote mtu mwenye hazina na anayeheshimiwa na majeshi anaweza kufanya chochote bila kujali katiba ina ubora gani kama hatuna utamaduni wa kuheshimu miongozo.

Kwanza katiba ni karatasi tu ambalo kila Rais anayeingia madarakani anaweza kuanzisha mchakato wa kulifanya anavyotaka liwe bila kuzuiliwa na mtu yeyote.
 
Siku zote mtu mwenye hazina na anayeheshimiwa na majeshi anaweza kufanya chochote bila kujali katiba ina ubora gani kama hatuna utamaduni wa kuheshimu miongozo.

Kwanza katiba ni karatasi tu ambalo kila Rais anayeingia madarakani anaweza kuanzisha mchakato wa kulifanya anavyotaka liwe bila kuzuiliwa na mtu yeyote.
Kama unadhani katiba ni karatasi tu basi pole sana sidhani kama mhadala huu unakufaa.

Na kana unadhani mwenye majeshi abaweza kufanya lolote basi pia ni tatizo, kwa sababu majeshi hayo nayo yanaweza kumfanya chochote! . Na akitoka madarakani hayo majeshi yanamtii mwingine!. Ndiyo umuhimu wa katiba mpya ili iwe mlinzi wa matumizi ya hovyo ya madaraka yanayoweza kupelekea kuumiza watu hovyo!
 
Kama unadhani katiba ni karatasi tu basi pole sana sidhani kama mhadala huu unakufaa.

Na kana unadhani mwenye majeshi abaweza kufanya lolote basi pia ni tatizo, kwa sababu majeshi hayo nayo yanaweza kumfanya chochote! . Na akitoka madarakani hayo majeshi yanamtii mwingine!. Ndiyo umuhimu wa katiba mpya ili iwe mlinzi wa matumizi ya hovyo ya madaraka yanayoweza kupelekea kuumiza watu hovyo!
Sawa,

Tuendelee kuipambania hivi hivi tukiwa nyuma ya keyboards.
 
Unaposema samaki akunjwe angali mbichi ni sahihi lakini pia tukumbuke huyu samaki alikalia hicho kiti bila kutegemea, hivyo kuanza kwa kusua sua ni kawaida kwa mtu wa aina hii...
Kwa hiyo uki mkunja "atavunjika"
 
Back
Top Bottom