Urais CHADEMA it's like a death sentence!

death is death no matter occasioning circumstances! after all we are already living like the dead while still alive in body only, so the courageous of us, unlike the timid and rubbery ones like author of this thread; have decided to face death in another planet; under CDM of course, you will die anyway. RIP
 
death sentence or dead sentense?

tumia tu kiswahili,elimu yenyewe hiyo ya kuunga unga ndugu yangu ngeri bado issue kama mimi hapa motot wa mkulima.
english kozi kibao!
 
MwanaJF Kim Kardash,

Nielewavyo ni kwamba CHADEMA wamekasirishwa na Mbunge wao Shibuda kwa kutangaza kugombea u-Rais akiwa CCM. Papo hapo alimwomba Kikwete eti awe kampeni meneja wake!!!

Shibuda pia amekuwa akishambulia CDM na viongozi wenzake kiasi cha kuridhisha kwamba yeye ni mamluki wa CCM. Kwa hiyo hata akivuliwa uanachama, umma utaendelea kuwa na imani ile ile na CHADEMA. Sasa ni lazima CDM wawe makini sana ktk kuchunguza na kuingiza wana-CCM, hasa viongozi wanaohamia chama hicho toka chama tawala..

Kuhusu Mh. Zitto Kabwe kugombea urais 2015, wanaCDM wengi wamemshauri angoje hadi atimize umri kwani hatakuwa na miaka 40 wakati huo. Akijaribu kubadilisha katiba, waTz watamwona ana maslahi binafsi, ingawa kuna mantik kushusha umri wa kuweza kuwa Rais hadi miaka 35 kama huko America.

Kuhusu Zitto kutaka kuwa Mwenyekiti wa CDM, ni vema ashirikiane na viongozi wenzake kujenga chama, hasa katika msimu huu wa kuvua gamba na kuvaa gwanda. Kuimarisha CDM badala ya kuunda makundi iwe ndio mkakati mahsusi kwa sasa kwa kila kiongozi, akiwemo Zitto. Hivyo ndivyo atavyoweza kuridhisha wanachama wamchague 2013 kuwa Mwenyekiti.

Matamshi kwa Chadema kina ukabila au ukanda, wakati magamba yanavuliwa na magwanda yanavaliwa kila sehemu ya nchi yetu, ni upuuzi mtupu usiostahili kutiwa maanani.
 
Shibuda awe Rais? Wa Tanzania? Duh! Mimi ni home Boy wangu but kwa title ya Urais hata msifanye nayo matani. Mnaona yanayotokea sasa na yote hayo ni mzaha wenu huu huu. ZK namfagilia kwa uwezo wake wa kujenga hoja na kufumua uozo but pia kwa title hiyo bado hafai. Inataka Wisdom ya hali ya juu sana. Kwangu mimi nawaomba wampe nafasi WS kama atakubali kugombea tena.
Dah umenikumbusha mbali sana. Nyang'homboli alikuwa mzee mmoja mlemavu wa macho mpiga zeze maarufu. no comment.
 
Nilifungua post yako kwa spidi saaana, alafu nakutana na mambo ya nafsi ya m2 ilio megeka!! wewe ni 1 wawalio sema CDM itashindwa vibaya arumeru leo tena unakuja na mengine, hisia haziwekwi hewani kizembe hivi ndugu, peleka kwenye udaku kuuule!!

Nilipendekeza slaa ndio agombee arumeru nikiamini mchango wake bungeni tunauhitaji,na nikaeleza nafasi ya chadema kushinda uchaguzi ule kama kitamsimamisha slaa,ndicho nilichokipresent
 
Ni nani asiye jua kuwa Shibuda ni kada nambari wani wa ccm? Shibuda kaja cdm kwa malengo yake makuu nayo ni kuivuruga cdm lakini anapaswa elewe kuwa cdm ina watu makini na waelewa zaidi yake hivyo hawezi kitu ameshtukiwa. Njama zenu twazijua kitambo

Kwa hiyo na nyie mlimpokea kada wa ccm kwa malengo maalum au?na vipi hawa makada wa ccm mnaoendelea kuwapokea sasa,mmejipanga vipi kuishi nao ndani ya zizi moja?acheni unafiki jipangeni chama chenu kiwe na mtandao mpana zaidi badala ya kutegemea zaidi makombo ya ccm bila ya hivyo yataendelea kuwakuta kutokana na hiyo operasheni sangara yenu ambao siku hizi mmeipachika kajina kangine matokeo yake inawapelekea kuzoa zoa hata madege yasoliwa....
 
Lkini shibuda kasema atamuomba slaa awe meneja wake wa kampeni za urais,kuna dhambi gani?kwanini msimuache atumie haki yake then mkutane nae kwenye vikao vya kuchuja wagombea?Heche na genge lake walikua na haraka gani nae kama sio uoga tu?
Huwa ninashangaa sana mtu anayejidai kuwakosoa wengine huku akitumia uongo kuhalalisha hoja zake, huwa anategemea nini?! Kwamba kila mtu ni mjinga na atadanganyika kwa mbinu hizo au?! Hivi ni kweli shibuda kasema atamuomba Dr. Slaa awe meneja wake wa kampeni za urais? Ikiwa hujui kwa usahihi alichosema shibuda na bila shaka hujui alikisemea wapi, utajuaje sababu za wanaompinga?! Mara nyingi huwa mnawasema wafuasi wa Chadema kuwa wanaiunga mkono hata ikikosea, ajabu ni kuwa nyie wenyewe hamuiungi mkono ikifanya sawa! Hivi inaingia akilini mtu anayetaka kugombea urais kupitia ccm atangaze nia hiyo katika kikao cha kamati kuu ya Cuf au nccr mageuzi?!
 
Hawa wasema kweli wa karne hii bwana, yaani watu wasichopenda kusikia ndio the truth?
kajifunza kiswahili tena,ningekua najua kichagga ningeandika ili unielewe sawasawa kwa nilichocomment,nimeandika nipo hapa to speak the truth na yale ambayo watu hawapendi kuyasikia,kwa kitendo cha kuweka kiunganishi na ni wazi hapo kuna vitu viwili,the truth na yale ambayo hampendi kuyasikia,kwanini unavichanganya makusudi na kukifanya kimoja???! hujui kiswahili.
 
death sentence or dead sentense?

tumia tu kiswahili,elimu yenyewe hiyo ya kuunga unga ndugu yangu ngeri bado issue kama mimi hapa motot wa mkulima.
english kozi kibao!

sen·tence

   /ˈsɛntns/ Show Spelled[sen-tns] Show IPA
noun 1. Grammar . a grammatical unit of one or more words that expresses an independent statement, question, request, command, exclamation, etc., and that typically has a subject as well as a predicate, as in John is here. or Is John here? In print or writing, a sentence typically begins with a capital letter and ends with appropriate punctuation; in speech it displays recognizable, communicative intonation patterns and is often marked by preceding and following pauses.

Lete hoja acha vioja....!na aliekwambia kuwa na elimu ni kujua kidhungu nani huyo kakuroga vibaya??
 
MwanaJF Kim Kardash,

Nielewavyo ni kwamba CHADEMA wamekasirishwa na Mbunge wao Shibuda kwa kutangaza kugombea u-Rais akiwa CCM. Papo hapo alimwomba Kikwete eti awe kampeni meneja wake!!!

Shibuda pia amekuwa akishambulia CDM na viongozi wenzake kiasi cha kuridhisha kwamba yeye ni mamluki wa CCM. Kwa hiyo hata akivuliwa uanachama, umma utaendelea kuwa na imani ile ile na CHADEMA. Sasa ni lazima CDM wawe makini sana ktk kuchunguza na kuingiza wana-CCM, hasa viongozi wanaohamia chama hicho toka chama tawala..

Kuhusu Mh. Zitto Kabwe kugombea urais 2015, wanaCDM wengi wamemshauri angoje hadi atimize umri kwani hatakuwa na miaka 40 wakati huo. Akijaribu kubadilisha katiba, waTz watamwona ana maslahi binafsi, ingawa kuna mantik kushusha umri wa kuweza kuwa Rais hadi miaka 35 kama huko America.

Kuhusu Zitto kutaka kuwa Mwenyekiti wa CDM, ni vema ashirikiane na viongozi wenzake kujenga chama, hasa katika msimu huu wa kuvua gamba na kuvaa gwanda. Kuimarisha CDM badala ya kuunda makundi iwe ndio mkakati mahsusi kwa sasa kwa kila kiongozi, akiwemo Zitto. Hivyo ndivyo atavyoweza kuridhisha wanachama wamchague 2013 kuwa Mwenyekiti.

Matamshi kwa Chadema kina ukabila au ukanda, wakati magamba yanavuliwa na magwanda yanavaliwa kila sehemu ya nchi yetu, ni upuuzi mtupu usiostahili kutiwa maanani.

Kwanini umegoma kuamini kwamba zitto akiwa mwenyekiti pengine ndio chama kitaamarika zaidi?zitto ni kijana na mtaji wa cdm kama ambavyo watu wanadai ni vijana sasa kwanini hamuoni umuhimu wa kumuweka mbele kijana mwenzao ambae wanaongea lugha moja,kuna nini kimejificha hapo?
 
Huwa ninashangaa sana mtu anayejidai kuwakosoa wengine huku akitumia uongo kuhalalisha hoja zake, huwa anategemea nini?! Kwamba kila mtu ni mjinga na atadanganyika kwa mbinu hizo au?! Hivi ni kweli shibuda kasema atamuomba Dr. Slaa awe meneja wake wa kampeni za urais? Ikiwa hujui kwa usahihi alichosema shibuda na bila shaka hujui alikisemea wapi, utajuaje sababu za wanaompinga?! Mara nyingi huwa mnawasema wafuasi wa Chadema kuwa wanaiunga mkono hata ikikosea, ajabu ni kuwa nyie wenyewe hamuiungi mkono ikifanya sawa! Hivi inaingia akilini mtu anayetaka kugombea urais kupitia ccm atangaze nia hiyo katika kikao cha kamati kuu ya Cuf au nccr mageuzi?!

Jenga tabia ya kupenda kujisomea,hata magazeti,acha uvivu wa kitanzania kutopenda kusoma.Haya nimekutafunia kazi kwako kumeza tu...
Shibuda amuwakia Heche Send to a friend
Mwananchi,Friday, 18 May 2012 22:40

Habel Chidawali, Dodoma

MBUNGE wa Maswa Magharibi, John Shibuda (Chadema), amemshukia Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (Bavicha) wa chama hicho, John Heche akimta amwombe radhi ndani ya siku tatu, vinginevyo atamshtaki kwa umma.

Shibuda alitoa kauli hiyo jana akitaka Heche atekeleze hilo ndani ya siku tatu, alipozungumza na vyombo vya habari kuhusu kauli zilizotolewa na Bavicha kuwa mbunge huyo ataondolewa ubunge.

Mbali na kumnyooshea kidole Heche, Shibuda alikwenda mbali zaidi na kumtaka Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa kuwa meneja wake wa kampeni katika harakati zake za kuingia Ikulu mwaka 2015 akisema, Dk Slaa atasaidiana na Rais Jakaya Kikwete katika kazi hiyo.

"Inaonekana Heche ana mtindio wa ubongo na wala si mzima wa akili yule, maana habari ya kutangaza kuwania urais ni haki ya kila mmoja. Hata nilipokuwa CCM mara kadhaa nilitangaza, lakini UVCCM haikutoa tamko, wala hakuna mtu wa usalama aliyekuja kunigongea. Iweje leo huku?" alisema akihoji na kuongeza:

"Kule CCM nilikimbia dhuluma na huku siwezi kukubali dhuluma, ndiyo maana nimekuwa mkimya kwa muda mrefu nikisoma mazingira. Lakini wakati wa kuzungumza umefika kwa kuwa ni haki yangu, huku nikitambua kuwa nchi inajengwa na wenye moyo na inaliwa na wenye meno.''
Alisema kuwa kutangaza nia ya kugombea urais ni haki ya kila mmoja na kwamba, Katiba ya Tanzania inamruhusu kila mmoja kufanya hivyo, lakini kinachotokea kwa Bavicha ni uhuni na wendawazimu unaokwenda sanjari na ulimbukeni.

Akizungumza kwa jazba na kutumia misamiati mingi, Shibuda alisema kuwa kinachofanywa na Heche ni msumari wa jeneza la kuua demokrasia na kutaka kumzika yeye kisiasa, akisema kuwa hatanyamaza hadi kifo chake.

"Heche anatengeneza jeneza la kunizika kisiasa, siwezi kunyamaza na viongozi wa juu wanajua kwamba Shibuda siyo wa kunyamaza na hawezi kunipora uanachama wangu hata siku moja kwani nimesimama imara ndani ya Chadema,'' aliongeza.

Mbunge huyo alimtaka Mwenyekiti wa Chadema Taifa kuitisha kikao mara moja na kujadili uwezo wa Heche na ikibidi wamfukuze mara moja ndani ya chama kwa kuwa anawagawa wananchi kwa ukabila na kwamba yupo kwa ajili ya masilahi ya wachache.

Kuhusu madai ya kutiliwa shaka ndani ya chama, alisema kuwa ni utaratibu wa kawaida kwa mwanasiasa mwenye mvuto kupambana na matatizo hayo, huku akisifu uwezo wa Mbowe akisema kuwa, amekuwa akiwatuliza wanachama wa Chadema kwa kuwa ameelewa msimamo wake (Shibuda) ni upi.

Akizungumzia nafasi yake ndani ya Chadema alisema hana shaka na uanachama wake na kwamba kinachomponza ni yeye (Shibuda) ni uwazi na ukweli, lakini hayupo katika kukisaliti chama.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

kwanini mnawaziba midomo wanachama wenu wanapojaribu kusema mipango yao ya kisiasa ya huko mbele?ndio hoja ya msingi hapa
Akili yako imeganda kama CCM. Vinginevyo ungeoanisha hoja yangu na kichwa cha mada tunayojadili usingeropoka hapa.
 
Umenyimwa binti (mchumba) ukaamua kuoa binti mwingine na katika harusi hiyo mpambe awe baba yake na binti uliyenyimwa usimwoe, mmmmmmm hii imetulia kweli? Shibuda zinamtosha kweli? na hii ni aina gani ya demokrasia kama siyo kumkaribisha Chatu mchana kweupe?
 
Nilipendekeza slaa ndio agombee arumeru nikiamini mchango wake bungeni tunauhitaji,na nikaeleza nafasi ya chadema kushinda uchaguzi ule kama kitamsimamisha slaa,ndicho nilichokipresent

Hivi wewe ni nani ndani ya Chadema kutoa ushauri juu ya nani agombee wapi? Huoni kazi aliyoifanya Dr. Slaa mpaka sasa kuhamasisha na kukuza chama? Bungeni tunao makamanda wa kutosha, na ulipata jibu lako papo kwa papo ambapo Chadema ilishinda Arumeru bila kumsimamisha Slaa. Kajipange tena.
 
hivi kutoa ushauri kwa chadema lazima uwe somebidy ndani ya chadema???

bado ushauri wake ulikuwa mzuri, hata kama Nassari aliwekwa na akashinda haipelekei kuwa alitoa ushauri mbaya! ndio maana hata nassari hakuwa peke yake ndani ya chadema...na yule aliyeshindana naye alipata kura! that said different people have different opinions!

mkuu uzee wako unasaidia nini humu JF??
 
Back
Top Bottom