Kimbunga
Platinum Member
- Oct 4, 2007
- 14,941
- 9,947
Hivi kuna shida gani mtu kutangaza kwamba anataka kugombea Urais. Kuna watu ambition yao ni Urais hivyo wakati wote wanaota kuwa Marais. Zile habari za kwamba muda wa kutangaza bado zimepitwa na wakati. CDM na hata CCM ziwaache watu wenye nia watangaze nia zao ili tupate muda mrefu wa kuwapima na kuwajadili kwa mapana na marefu. Masuala ya kuutaka Urais kwa staili ya nataka sitaki ni uzandiki. At least kwa sasa najua kuna watu wawili CDM wametamka kwamba watagombea kwa kufuata utaratibu wa chama wengine wanaotaka nao watamke na siyo kujiundia makundi kimyakimya. Hayo makundi siku yakilipuka utakuwa ndio mwisho wa chama.