KIM KARDASH
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 5,139
- 1,149
Chadema-chama kinachojitambulisha kama ni cha kidemokrasia kwa mara nyingine tena kinaoneka kufeli mtihani mwepesi sana wa kuonyesha ukomavu wa demokrasia kwa vitendo hapana maneno.Safari hii chadema kimekua tested na kada wake mashuhuri JOHN MAGALE SHIBUDA ambae ni mbunge wa chama iko akiwakilisha wananchi wa moja kati ya majimbo yanyopatikana katika mkoa wa shinyanga.Shibuda ambae alihamia chama iko akitokea ccm baada ya kudai kufanyiwa mizengwe baada ya kura zake kutotosha kwenye kinyang'anyiro cha ubunge ndani ya ccm hivi majuzi alijaribu kukipima chama chake kuona kama kweli kimekomaa kidemokrasia ama la kwa kutangaza nia tu ya kwamba atagombea urais kupitia chama chake kwenye uchaguzi mkuu ujao.Baada ya kutangaza nia yake hiyo shibuda amekua akishambuliwa na wana chadema toka kila kona ya nchi hii akiwemo mwenyekiti wa umoja wa vijana wa cdm huku wengine wakienda mbali zaidi kwa kupaza sauti kwamba shibuda afukuzwe,kisa nini?kwanini katangaza kugombea urais!!!!!!!!!!!! hilo tu basi hawana lingine.Itakumbukwa pia hali inayomkumba shibuda iliwahi kumpata pia marehemu CHACHA WANGWE alipotangaza nia ya kugombea umakamu mwenyekiti wa cdm na baadae uenyekiti ambao hata hivyo hakugombea tena,alifariki kwa ajali ya gari kabla ya kutimiza nia yake hiyo.Baadae hali hiyo akaja kukumbana nayo zitto kabwe nae alipotangaza nia ya kugombea uenyekiti ba hivi majuzi tena alipotangza nia ya kugombea urais kwa tikiti ya chadema.Yaliyowapata wanasiasa hao yanaacha maswali mengi juu ya hali ya demokrasia ndani ya chadema kiasi kwamba inatishia watu wengine wenye sifa za kugombea uongozi ndani ya chadema kujiuliza mara mbili mbili.