Urais CCM: Hofu ya uasi yatanda

Urais CCM: Hofu ya uasi yatanda

chaikavu

JF-Expert Member
Joined
Apr 18, 2015
Posts
760
Reaction score
473
MAKUNDI ya wagombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), yanadaiwa kuanza mchakato wa kuhakikisha mgombea wanayemuunga mkono, ndiye anayeteuliwa na chama hicho kupeperusha bendera ya chama katika Uchaguzi Mkuu.

Chanzo chetu cha habari kinasema kuwa, kundi la mgombea anayetajwa kutaka kuwania nafasi hiyo, limeanza kutumia kiasi kikubwa cha fedha na kuzigawa kwa baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), ambapo kitendo hicho kimefananishwa na uasi ndani ya chama.

Pia chanzo hicho kilisema baadhi ya wajumbe wa NEC wameanza kupewa maelekezo ya kufanya uasi dhidi ya vikao vya maamuzi ambavyo vitavyoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete.

Inadaiwa kuwa, hivi karibuni rafiki wa karibu na mgombea huyo, alipokea fedha kutoka nje ya nchi ili kufanikisha kampeni ya mgombea wao kwa kuwaita baadhi ya wajumbe wa NEC nyumbani kwake na kuwapa kiasi kikubwa cha fedha.

Chanzo hicho kilidai kuwa, lengo la vikao vinavyoshirikisha wajumbe hao ni kuhakikisha mgombea wao anaingia Ikulu kwa gharama yoyote na kupewa maelekezo ya kufanya.

Maelekezo hayo ni pamoja na kuhoji sababu za mgombea huyo kupewa adhabu kwa kosa la kuanza kampeni mapema, kuing'oa Kamati Kuu inayoongozwa na Rais Kikwete na Sekretarieti ya CCM inayoongozwa na Katibu Mkuu, Bw. Abdulrahman Kinana kwa tuhuma za kutomshauri Mwenyekiti wa chama kuhusu umuhimu wa kuitisha vikao.

Rafiki wa mgombea huyo, anadaiwa kuwataka wajumbe hao kumuombea kura mgombea wao katika vikao vya chama kwa maelezo kuwa, yeye ndiye mwenye kuimudu nafasi hiyo kuliko wagombea wengine katika mchakato huo.

Baadhi ya wajumbe hao, wanadaiwa kupewa kazi ya kuwachafua na kuwadhalilisha viongozi wa CCM ngazi ya juu akiwemo Rais Kikwete, Bw. Philip Mangula (Makamu mwenyekiti wa CCM-Bara), Bw. Kinana na Bw. Nape Nnauye (Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Taifa).

Inadaiwa kuwa, zaidi ya sh. bilioni 10.7 zimepangwa kutumika ili kuwahonga wajumbe 370 wa NEC, wajumbe 2,011 wa Mkutano Mkuu pamoja na wajumbe 270 wa Zanzibar ili kuhakikisha chama kinamteua mgombea huyo kuwania urais Oktoba mwaka huu.

Taarifa zaidi zinadai kuwa, lengo la kutaka kuwafukuza wajumbe wote wa Kamati Kuu na Sekretarieti ya chama ni kutoa fursa ya kuchagua wajumbe wapya ambao watasimamia mchakato wa kupitisha jina la mgombea wao kwa tiketi ya CCM.


Chanzo: Majira
 
Ccm inahitaji kukaa kando ili ijitathmini na kujiweka upande wa taifa badala ya kukimbilia ikulu wakati imebeba silaha za kulimaliza taifa.

Mtu yeyote anayekula njama, na kupanga hila za kuhujumu haki na kweli kwenye chama chake, na kutumia njiia haramu za kushinikiza yeye ndiye awe the best candidate huku akijua siyo, anatakiwa kwanza chama kimfikishe kwenye idara za nidhamu ya chama ili ajitetee na kuonywa ikiwa itabainika amekosea bahati mbaya.

Lakini pale inapokuwa bayana kwamba ni mafia, anatumia kila njia halal na haramu ikiwemo rushwa, vurugu na kushawishi uasi ulio kinyume cha sheria, lengo lake likiwa ni kutafuta uongozi, huyu anatakiwa avuliwe uanachama ili chama kiweze kuendeshwa bila mihemuko ya ugaidi na uhaini wa ndani.


Huyo mtu anayetumia hila, uwongo, rushwa, fitina, udanganyifu na vitisho kwenye chama chake, chama chake kikimwogopa, ni dhahiri chama hicho ni dhaifu na moja kwa moja kinajiondolea sifa ya kukabiliana na changamoto kubwa zilizopo na zinazoweza kujitokeza. Kwa mtaji huo, Watanzania hawanasababu ya kuchagua chama chenye woga wa kipum.bavu wakati ambao wimbo wetu ni kupata uongozi imara.

Kama lowasa atawatisha kwa fedha zake na za kutoka nje, huku akijua na dunia ikijua hana sifa ya kuwa raisi, lakini kwa woga wa ccm wakamwogopa na kumptisha, hiyo ccm itaongozaje nchi wakati taifa linatishiwa na changamoto ambazo hazijawahi kuwepo kutoka ndani na nje ya nchi? Kwa hiyo kila atakaye black mail, ama kujitunishia misuli, ccm hiyo kwa woga itaridhia matakwa yake hata kama yako kinyume na kweli. Huyo Lowasa, atakapokuwa raisi kwa nguvu ya rushwa, ama kwa woga wa ccm, nani atahakikisha anasimamia maslahi ya taifa, wakati atakuwa tayari keshatangaza ubabe na chama chake hakina uwezo wa kumsimamia wala kumdhibiti?


Ninasema tena, Tanzania inahitaji uongozi imara na safi. Ccm ina makandokando mengi na kamwe kwa sababu yoyote, msije mkafanya kosa la kusimamisha fisadi linalokataliwa na kila mtu, kwa kuwa limetumia rushwa na ushawishi haramu, nanyi mkaliogopa mkasuribi hadi liwamalize, na kuwaondoa kwenye utaratibu, mbaki mnapiga miayo.

Jifunzeni kwa CHADEMA. waliovowafanya na wakala wenu ZITO KABWE, hawakuogopa kwamba ata influence negatively. Walichukua hatua sahihi na bila kumpa nafasi ya kufanya uharibifu zaidi. Chama si mtu. Leo Zito hayupo, CHADEMA kimekuwa na kuimarika wa kiwango na kasi haijawahi kuwepo.

Ccm mwondoeni huyo fisadi na mfitini miongoni mwenu. Hana nguvu wala sera yoyote zaidi ya tamaa na ubinafsi. Inawezekana pia anapigana kwenda ikulu kwa sababu huko anakochukulia fedha, ana mikataba. Kama ninyi mtamwogopa, mwacheni kwenye chama lakini kwenye uraisi asahau. Na ccm chatu haipewi uraisi Tanzania!.
 
Hawa jamaa walikoanza kufifia ni kukosa mwenye sauti ndani ya kambi yao. Tangia waweze kumzibiti mzee wa ''Privatization'' mwaka 2005, Kila mtu sasa ndani ya kambi ana nguvu hehehehehe hadi Vuvuzena ana nguvu sana. Na kwa kuwa aliyepaswa kuwa na nguvu hana hio nguvu kwa kupenda kwake, Anatumia ''Inzi'' wetu kuwadhibiti wanaomnyima usingizi na anadeal nao gizani gizani ila wakikutana nuruni kwa wale waliobakia hai anacheka nao kama kawaida na kuwaahidi makubwa.

Tatizo la msingi lilianzia hapo.. Mzee wa ''opportunity'' na Mzee wa ''privatization'' walipitishwa kwa sauti ya Baba.. sasa kambi haina Baba wa kusikiliza hadharani..... Yupo anayesikilizwa mafichoni na ni rafiki wa kila kambi hadharani.

Asomaye na asifahamu neno hili.
Cyber Crime Act ishindwe na ilegee.
 
CCM wamezoe kupanga mipango ya kuvisambaratisha vyama vya upinzani sasa imefika zamu yao ya kulana wenyewe kwa wenyewe.

Kwa mtindo huu wa kutumia pesa utawafanya wachague garasha ambalo litawapeleka kaburini moja kwa moja.
 
Kupasuka ni lazima, acha kiwafie wananyanyasa watz kuliko chama chochote duniani
 
Watanzania tulio wengi tunajiuliza ni lipi lengo la huyu Lowassa kutaka kwa nguvu zote kuingia Ikulu, ni kuwatumikia wananchi? Kukitumikia chama chake? Au ni kwa ajili ya maslahi yake binafsi??? Lowassa ana lipi jipya na unique la kuifanyia nchi hii???

Iko wazi, Lowassa ni mwizi na fisadi aliekubuhu...Watanzania tunapaswa kumuogopa mtu huyu???
 
Magazeti yanayoandika habari za namna hii na kukariri "chanzo chetu cha habari" yanatakiwa kudhibitiwa...hivi kikao cha wahariri kilichofanyika Morogoro kilileta mabadiliko gani. Hizi ni habari za uzushi!
 
CCM bye bye....Wanamwaga mboga na ugali wenyewe, shauri ya kuidhulumu nchi waliyokabidhiwa..wanavuruga hadi moto ili mmojawapo asipike chochote...!
UKAWA jiko lao lipo chumba cha pili, wao watapakua tu 'msasi wa wananchi', watawapakulia wananchi, wananchi wanakula bila waasiwasi...wala hakuna kunyanyaswa...let October come soon!...go UKAWA all the way!
 
Naomba niwaulize ndugu zangu Watanzania, ni nani anaetumia nguvu nyingi ktk hili la Mh Edo ni yeye binafsi au ni kundi fulani la wapambe wake? Kwanini Hela nyingi zinatumika kiasi hiki kuhakikisha anateuliwa? Namuomba MWANA DIWANI atupe ufafanuzi wa hili jambo. Taifa letu limefika mahali pabaya mno. No money no Leadership.
 
tumechoka kusikia habari hizo hizo wachaguane tu yaishe tuendelee na mengine, wenye kupata presha na wapate wenye kufa nao tuwapige chepe tu.
 
Kama kuna mtu anayejua kulipa fadhila ni JK. Kawapa ulaji kiila mtu wa karibu. Sasa ameona aongezee siku za kumfunua mwali ili wana ccm wote wapewe kaulaji kidogo.
Fedha zoote hizo aliona zikikusanywa kutoka kwetu, sasa anataka wakuu wenzake wagawiwe kidogo. Mwali akifunuliwa usiseme sikulamba mkono wake. Hosea kawekwa mbaliiii hana cha kusema hapa. Wazee wanachu..mbishana maa.vii baada ya kushiba sana yanatoka tu.
Poleni ccm kwa kuvimbiwa. Cheua tu mhishimiwa Edooo
 
Hizi fitina ndio zinazoiua CCM na Taifa kwa ujumla.
Eti anatumia pesa kutoka nche ya nchi!!!
Afadhali kabisa mana nilifikiri anatumia mtutu wa bunduki!!
Mana hii nchi inapaswa ichukuliwe na komando mmoja kupita mtutu wa bunduki na makofi mengi awatoe wajinga wajinga wote waliopo madarakani wanaokesha kutumia wapuuzi waje kutudanganya kwenye mitandao.

Hivi hii nchi haina sheria ya kusafirisha hela haramu?
Kama kuna hela haramu zinazoletwa nchini kwa ajili ya uchaguzi tena kumsaidia mtu mmoja kupitishwa tu na chama chake kwa nini asikamatwe kwa kosa la jinai?
Kwa nini tunaletewa porojo za makosa ya jinai yaliyoko wazi halafu wanaoleta porojo wanahitimisha la kusema aliyefanya jinai kama hiyo afukuzwe kwenye chama au jina lake likatwe? Hapa kuna nini kama sio fitina ?!Hivi kweli mtu atoe rushwa ya mamilioni ya pesa kwa watu nchi nzima tena kwa watu tunaoaminishwa kwamba hawamtaki halafu hakamatwi na polisi au PCCB badala yake tunasikia tu jina lake ndio likatwe? Haiingii akili kwa watu tusiyempenda mtu yeyote kwa ahadi ya kimaslahi au kujuana.!
Ndani ya CCM wamesahau kuwa kuna watu wengi nje ya chama hicho wasio na vyama. Wanawapima watu kwa uwezo wao sio ushabiki wa kikundi cha watu..
Hivi kweli kama mtu hapendwi na watu tena ndani ya CCM chama ambacho utaratibu wake unajulikana kwamba unafanywa na vikao halali ,hofu ya rushwa inatoka wapi wakati kura za maamuzi ni za siri?

Hivi ni mjumbe yupi wa CCM anayeweza kumpigia kura mtu asiyempenda kwa sababu tu ya rushwa wakati kura ni siri na kila mjumbe wa CCM anajua anachokifanya?

Tatizo hapa lipo wazi ni kwamba kuna vikundi vidogo vidogo ambavyo hata hela zao watu hawazitaki mana hela yake ukiichukua utapata shida kumnadi mgombea wao. Lakini kusema kuwa mtu mmoja anaingiza mabilioni toka nje ni uzushi .Vinginevyo vitolewe vielelezo na walioziingiza hizo pesa wachukuliwe hatua kuanzia watendaji wote waliozembea na kuacha pesa haramu ziingie nchini.

Hebu tuangalie hii orodha ya wanaotajwa kuwa wameanza au wameshawishiwa kuchukua form:
(1)Mizengo Pinda -waziri mkuu wa Tanzania
(2)Bernad Camilius Membe -Waziri wa mambo ya nje
(3)Prof.Mark Mwandosya- Waziri asiye na wizara maalum
(4)Stiphen Masatu Wasira- Waziri wa kilimo
(5)Lazaro Nyarandu -Waziri wa maliasili
(6)Samweli Sita -Waziri wa Uchukuzi.
(7)Harison Mwakyembe-Waziri E.Afrika
(8)John Pombe Magufuli -Waziri wa Ujenzi.
(9)Mwigulu Lameki Nchemba Naibu w/ fedha
(10)January Makamba -Naibu w/Mawasiliano.

Hao wote niliowataja wapo madarakani wanasimamia dola na wanaweza kutoa amri kwenye vyombo vyote vya dola wakati wowote na ndio washauri wakuu wa mh. Rais .

Sasa kama hawa wanawatuma wapambe wao kuja tena kulalamika na kupiga majungu kwenye mitandao badala ya kuchukua hatua dhidi ya makosa ya jinai yanayofanywa na wasaka urais itakuwa ni jambo la aibu na la fedheha kwa Taifa letu .

Na kama ni kweli timu yote ya mawaziri niliyoitaja hapo juu imeshindwa kuzuia uhalifu unaofanywa na baadhi yao kama tunavyoambiwa basi kati yao hakuna hata mmoja anayefaa kuwa hata diwani wa Kata yangu ninakotokea.
Vinginevyo wanatumia fursa zao kuandaa watu wa kuchafua wenzao bila hofu mana wao ndio walioshika dola.Na au hao ndio wanaotumia nafasi zao kuingiza pesa haramu za kampeni kama kweki zimeingia nchini. Kama sio hivyo basi haya ni majungu na tunamuomba mwwnyekiti wa CCM asikubali kusikiliza majungu ya makundi ya watu wasio na uwezo wala sifa.Kazi yao ni kulalamika badala ya kukijenga chama wanakibomoa kwa kucheza kila mchezo wa wapinzani.

Mwisho niseme kwamba
Chuki
Ukabila na
Udini
Ndivyo vinavyoonekana kushamiri wakati huu wa uchaguzi .Tukiendelea kuviendekeza matokeo yake vitazidi hata baada ya uchaguzi.

Mungu ibariki Afrika .Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom