Urais 2015: Nilichokisema jana kuhusiana na kauli ya Lowassa

Naomba niongee ukweli. Sijawahi kuvutuwa na hoja za Kigwangala....:confused:

Eti anauliza why imemchukua miaka saba kujibu hoja? Mbona jibu rahisi sana... Kwamba yote yaliyosemwa jana na EL ni usanii tu... Ukweli ni ule wa miaka saba iliyopita... Labda tusema tu kuwa kuna baadhi ya wahusika hawakuwajibishwa kama ambavyo ktk escrow wameachwa.

Kama mimi nisivyovutia na lowasa kutokana na kushindwa kujenga hoja analeta bla bla bla tu
 
Safi sana Hk umemweleza ukweli huyu fisadi lowasa.anatapatapa alikuwa wapi miaka 7 iliyopita?
 
wewe ni katika wehu waliojazana WAMA? rejea bandiko langu na ulielewe then tujadiliane kwa hoja siyo mistari ya taarabu ... nani wa kusafishwa? Lowassa ama beneficiaries wa ESCROW? UJANGILI? SEMBE? ... jipange uje upya ...

WEWE UMEJAZANA RICHMOND, HIVI UMEELEWA NILICHOKUULIZA? HICHO HUYO BOSI WAKO ANACHOKISEMA KWAMBA NI KITU GANI RAIS HAKIJUI ni kwa nini hakisemi hicho ambacho RAIS HAKIJUI?

KWA HIYO UNATAKA KUSEMA KWAMBA KUWEPO WEZI WA ESCROW KUNA MSAFISHA LOWASA NA RICHOND?

WOTE MMEOZA KWA WIZI NA HAKUNA MWENYE NAFUU KWENYE HILI LICHAMA LETU HILI.
 
Huyu ni kigwangala huyu huyu,kama anayajua kama hayajui hana uhakika sisi tutakuaje na uhakika wa maelezo yake na maswali yake? Nakudhauri kigwangala hayo kayaseme kwenye mkutano wa hadhara wa ccm utajibiwa.
 
Kigwangallah na wale wanaomwambia achunge maneno:

Hakuna kitu kimetufanya tuwe masikini wakubwa hadi bajeti yetu iwe inasaidiwa na Wadhamini kama huu UNAFIKI wetu.

Nimekuwa natamani sana ifike siku watu wawe wanaongea bila kuogopa kama ilivyokuwa enzi ya Nyerere.

Hata kama sikubaliani na Lowassa au Kigwangallah, ila kwa ujasiri wa kusema waziwazi bila kumumunya maneno, nakupa hongera sana maana hilo ndiyo linatakiwa. Unaandika au unasema wazi kulichokusonga moyoni bila kumtukana mtu.
Gwajima alipompandishia Pengo, hakukuwa na makosa ila baadhi ya maneno yaliyotumika hayakuwa mazuri.

Kigwangallah kaandika yake ya moyoni, hakutowa hata TUSI moja. Sasa hii ya tunza maneno yako, watch out, chunga sana, be careful na vitisho vingine vingi ndivyo vilivyotufikisha hapa. Unaweza kukuta hata Lowassa mwenyewe ni mpenzi wa lugha za kukosoana na kuwapa watu uhuru wa kuongea bila kusita ili muradi hujavunja sheria, sasa wapambi mnachukia nini? Mwenyewe ameshasema "Hatalipa kisasi" hivyo msimtishe MJASILI.

HK, ni haki yako kikatiba kugombea. Utashinda au hutashinda, hilo ni swala jingine. Pia na wewe jiandae kushambuliwa "kistaarabu" humu ndani ya JF na nje ya JF maana ndiyo Demokrasia tunayoitaka na wewe pia unaitumia.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Lowasa ana maswali mengi ya kutujibu watanzania.nilishangaa Sana Jana alipohojiwa na waandishi wa habari ambao.binafsi napata mashaka watakuwa wamehongwa.hakutoa ufafanuzi wa tabia yake yake ya kutoa rushwa kwa wananchi ili wamkubali. Na cha ajabu hakuna mwandishi hata mmoja aliyeuliza swali hili.kama Si kuwa wamehongwa tusemeje? Jamani ndugu zangu watanzania tutajuta kumchaguwa huyu mtu anayetumia fedha kuingia ikulu.Hatufai huyu uongozi haununuliwi hata siku moja.nimegusia hii tabia yake ya kutoa rushwa.hayo ya miaka ya nyuma ya wizi Na ufisadi wa Mali ya umma sijaelezea.
 
Kashfa ya Richmond ilikuwa ya serikali yote including EDO. EDO hafai kuwa rais wa awamu ya 5. Kama serikali yote ilikuwa inahusika na EDO alikuwa sehemu ya serikali sikivu naye pia alihusika kama waziri mkuu.
 
Mtu asiyetakiwa anajadiliwa?peleka kule weka mbali na watoto!

wewe vipi.hapa wazalendo tunapambana kuzuia jambazi lisiingie kwenye Ofisi ya umma.ndio maana unaona watu tunakazana.kushindana na nguvu ya pesa. za fisadi lowasa siyo kazi ndogo.eboo
 
Nilichokisema jana kutokana na kauli ya Mhe. LOWASSA...

Mh. HKigwangalla. japo umeandika mengi lakini naweza kufupisha yote uliyoyaandika kwa sentensi moja tu nayo ni hii hapa chini, nanukuu;

- ikitokea akawa mgombea wetu, tutaanzia wapi kumnadi na kusema ni mtu safi, muadilifu, anayechukia rushwa na ubadhirifu na kwamba anafaa kuwa Rais, wakati juzi tulisema hafai kuwa Waziri Mkuu na tukamtoa?
HKigwangalla, mimi Mag3, najulikana kwenye jukwaa hili kama mtu asiyemung'unya maneno...sina unafiki na sina uvumilivu kwa wanafiki. Ni kweli LOWASSA hafai, na narudia tena, hafai na hana sifa za kuwa Raisi wa nchi hii lakini swali ni kwamba, ndani ya CCM nani anafaa?

Nitakurudisha nyuma kidogo tukumbushane yaliyotokea kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 mwishoni mwa mwezi wa Oktoba. Nataka pia tukumbushane kuwa wakati huo tayari kashfa kibao zilikuwa zimeiandama serikali ya CCM ikiwa ni pamoja na ya Richmond iliyomlazimisha Lowassa ajiuzulu nafasi yake ya Uwaziri Mkuu kuisetiri serikali kama alivyofanya mnafiki mwingine Mwakyembe. Je nini kilitokea? Naacha picha ziongee;

wtcoj.jpg


Kiwete akimnadi Lowassa Monduli baada ya jana yake kumsafisha Mramba Rombo.

"Tobiko Kikwete, Tobiko…Wataweza? Watamuweza Kikwete," yalikuwa maneno yaliyotamkwa na Lowassa na umati huo kujibu, "Tobiko Kikwete, Tobiko' pamoja na ‘Hawataweza, Hawatamuweza.' Hayo yalitokea jimboni Monduli katika kampeni ya Uchaguzi.

Akimnadi Kikwete, Lowassa alitumia kaulimbiu ya ‘Tulifurahi Pamoja, Tulihuzunika Pamoja na Tutasonga Mbele Pamoja na Tutashinda,' katika kuomba kura, alisema wanajiandaa kujenga kiwanda cha kisasa cha nyama mjini Makuyuni.

Naye Kikwete akimnadi Lowassa alisema, "huyu ni mtu anayewapenda sana, anawahangaikia sana, haya yote (mafanikio) yanayosemwa sasa yametokana na juhudi zake…hakuna mwakilishi mzuri kushinda Edward Ngoyai Lowassa.

"Lowassa ni msafi na tuhuma zinazomkabili ni za uongo na za kupakaziwa," alisema Kikwete.

Mh. HKigwangalla, huu ni mfano moja tu unaoonesha jinsi CCM bila soni ama aibu ina ujasiri wa kumnadi hadi shetani mbele ya wananchi...sasa unapohoji mtaanzia wapi kumnadi Lowassa, swali langu ni hili, ulikuwa wapi mwaka 2010? Kama nilivyosema awali siwafumbii macho wanafiki, walaghai na wapuuzi na wewe hapa umeonesha sifa hizo kwa kiwango cha kutisha.

Ukibisha nitaendelea kuonesha unafiki na ulaghai ulivyokithiri ndani ya chama chako cha CCM...bahati nzuri ni kwamba, kama manyang'au, umefika wakati muafaka muanze kutafunana wenyewe mwa wenyewe kwani mzoga upo hatarini kuyeyuka. Mtatukanana, mtaumbuana na mtakashifiana lakini kwa kuanika uchi wenu mnawawezesha wanachi kuwatambua kwa sura na tabia zenu halisi.
 
Mkuu nadhani hii nafasi aliyonayo huyu jamaa aliye chumbani lakini hajui chumbani lakini hajui chumbani kuna nini ilitakiwa iwe yako...ni hayo tu
 
MD...MPH...MBA bado sana mzee...unajiuliza maswali??? MD...MPH...MBA bado sana mzee...looh
 
Mkuu nadhani hii nafasi aliyonayo huyu jamaa aliye chumbani lakini hajui chumbani lakini hajui chumbani kuna nini ilitakiwa iwe yako...ni hayo tu
 
Nilichokisema jana kutokana na kauli ya Mhe. LOWASSA.

Mimi nilianza kushiriki siasa toka nikiwa mdogo sana. Kuanzia Chipukizi, Greenguard wa UVCCM na baadaye UVCCM. Miaka ya mwanzo ya 90 nilivutiwa sana na mijadala ya mfumo wa vyama vingi ama kimoja. Nakumbuka, binafsi nilivutiwa zaidi na mfumo wa kutanua demokrasia, nakumbuka nilichangia hoja zangu kwenye mkutano wa tume pale Nzega mjini, viwanja vya parking pembeni ya jukwaa. Wengi kwa hakika hawakuunga mkono mfumo wa vyama vingi. Waliamini katika chama kimoja. Nilijiunga rasmi CCM mwaka 1994. Mwaka 2005, niligombea Ubunge wa Jimbo la Nzega, kura hazikutosha kwenye mchakato wa maoni ndani ya CCM na vikao vilisema kuwa wakati wangu bado.


Niliendelea kufuatilia kwa ukaribu sana kilichokuwa kinaendelea kwenye duru za siasa. Mijadala ya Bungeni ilikuwa ya moto sana, mara nyingine ikitutia simanzi sisi vijana wa CCM haswa namna tulivyokuwa tukishuhudia wabunge wachache sana wa upinzani wakiishambulia serikali yetu ya CCM kuhusiana na wimbo mpya kwenye duru za siasa za miaka hiyo, 'ufisadi'. Ufisadi ikiwa ni order of the day. Ufisadi ikiwa ni mtaji na ajenda kuu ya wapinzani Bungeni, of-course pia ajenda ya kikundi kidogo cha wabunge wa CCM waliojitambulisha kama vinara wa kupinga ufisadi. Miaka hiyo kila mtu akiuchukia ufisadi na mafisadi.


Mwaka 2008, mimi nikiwa kijana mwana mabadiliko na ninayechukia ufisadi na mafisadi, kama walivyokuwa vijana wenzangu wengi, kwenye duru za siasa na nje ya duru za siasa, nilivutiwa na mijadala iliyokuwa Bungeni kutokana na hoja iliyowasilishwa bungeni na Dr. Harrison George Mwakyembe kuhusiana na mchakato wa kununua umeme wa dharura, na zabuni hiyo kupewa kampuni ya Richmond Development Company LLC ikidaiwa kuwa mchakato huo ulikuwa na ubatilifu na mazingira ya rushwa ndani yake. Nikiwa kama mwananchi mwenye strong affinity na siasa, uongozi na namna nchi yetu inavyoendeshwa, nilivutiwa sana na namna wabunge wengi wa CCM walivyoamka na kuonesha kwa dhati ya mioyo yao namna walivyokerwa na ufisadi wa Richmond. Nakumbuka Mbunge wangu Lucas Selelii alikuwa kinara mmojawapo.


Mwanzoni sikutarajia kama Waziri Mkuu niliyempenda sana na kumuamini, niliyemtazama kama kiongozi wa mfano kwangu, aliyenivutia sana kwa namna alivyokuwa akichapa kazi na akitoa kauli za straight forward kwenye mambo mengi ya msingi, akikemea uzembe, akiadhibu wabadhirifu bila soni wala huruma, akifika kila kona ya nchi ambapo akitokea tu, basi wazembe na wabadhirifu wanaangusha angusha karatasi hovyo, Mhe. Edward Ngoyai Lowassa eti naye angehusishwa kwa namna yoyote ile! Sikuamini. Lakini sikuamini zaidi niliposikia anajiuzulu...tena eti kwa sababu ya Richmond.


Nakumbuka sana kwenye duru za siasa yeye na Mjomba wangu Mhe.Jakaya Kikwete walipochukua fomu za kuwania Urais mwaka 1995, wakiwa na ujana ujana mwingi na sisi tukiwashangilia na kuwapenda kama inspirational figures wetu. Na ilipotokea mwaka 2005 alipoingia Mjomba, nilijua wazi kabisa kuwa Waziri Mkuu angekuwa Mhe. Lowassa, na tulitabiri kipindi kile kuwa Mhe. Lowassa angekuwa Rais baada ya kumaliza kipindi cha Uwaziri Mkuu, yaani 2015. Nilisimamisha kagari kangu maeneo ya Biafra na kukimbia kwenye Pub moja pale jirani kutazama televisheni iliyokuwa inarusha kutoka Bungeni, nakumbuka watu walijaa kwa wingi sana na wengi wakishangilia kuonesha kufurahishwa kwao namna serikali ilivyokuwa ikiwajibika Bungeni. Sikuamini. Serikali imeanguka! Lowassa out. Sikuamini kabisa.


Jana nikapata habari kuwa Mhe. Edward Lowassa amezungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini - amekana kuhusika kwake na Richmond. Nikashtushwa sana na hili. Nikajiuliza hivi ni nini kinataka kutokea kwenye siasa za nchi yangu? Mjadala wa Richmond ulifungwa Bungeni miaka 7 iliyopita, je inabidi ufunguliwe upya, na watu wapya tutafakari upya? Maana kuna minong'ono kuwa Mhe. Lowassa anataka kuwania Urais mwaka 2015, na ana mpango wa kutangaza nia muda si mrefu. Nikajiuliza, ni kwa nini imemchukua Mhe. Lowassa zaidi ya miaka saba kujibu hadharani kuwa hakuhusika na Richmond? Kwa nini anatamka maneno haya leo na kwa nini hakujitetea Bungeni siku ile alipojiuzulu? Nakumbuka siku ile alisema tatizo ni uWaziri Mkuu, kwa nini hakufafanua na alikuwa na fursa hiyo kama 'primus inter pares (first among equals)?' Kipindi fulani alisemekana kuwa ni 'gamba' na lingepaswa kuvuliwa...likaishia kiunoni! Ni kwa nini halikuvuka? Maswali haya sijawahi kuyapatia majibu.


Hivi ilikuwaje Rais wa Nchi, ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, Kamati ya Wabunge Wote wa CCM Bungeni, na mamlaka zote za kiserikali kushindwa kumlinda Waziri Mkuu wake dhidi ya tuhuma za kuhusika kwake kwenye Richmond mwaka 2008? Maana kwenye siasa za mabunge yanayofuata mfumo wa Westminster, Waziri Mkuu ni 'primus inter pares', kwamba ana fursa ya kwanza ya kuzungumza kwenye mijadala Bungeni na ana-enjoy nguvu ya kuwa na majority bungeni kuendesha mambo ya serikali na kutawala mijadala na maamuzi. Ilikuwaje Chama kilimuacha Waziri Mkuu wake akaanguka? Ilikuwaje? Maswali: je kulikuwa na ukweli dhidi yake kuhusiana na tuhuma za Kamati? Ama Kamati ilitumika vibaya na mahasimu wake? Yeye amekana, sasa wanakamati inabidi wamjibu watuweke wazi, na wamjibu kwa uwazi bila kuficha, maana kama alionewa ijulikane na sisi tuliohuzunishwa ama kufurahishwa na Bunge wakati ule tuujue ukweli. Yeye anasema hakuhusika na ndiyo maana Kamati ya Mwakyembe haikuona haja ya kumwita kumhoji. Ukweli tunauhitaji sana leo kuliko jana. Ukweli huu ni haki yetu.


Kama Kamati ilimuonea, basi imuombe radhi na ituombe radhi watanzania wote. Kama kweli Mhe. Lowassa atagombea Urais Twentyfifteen, itakuwaje kwenye mijadala ya uchaguzi na CCM itasimamaje (kama itampitisha kuwa mgombea) kumuombea kura wakati ilimuangusha Bungeni kutoka kwenye nafasi nyeti ya Uwaziri Mkuu? CCM itatoa majibu gani kuhusu kwa nini ilimuita 'gamba' na ikatangaza hadharani kuanza mchakato wa kuvua magamba (ambao haukukamilika). Nilisema jana, Mhe. Lowassa amefungua pandora box, na kama atatangaza kweli kuwania Urais, inabidi haya mambo yawekwe wazi, yamalizwe, maana hauwezi jua ya kesho - ikitokea akawa mgombea wetu, tutaanzia wapi kumnadi na kusema ni mtu safi, muadilifu, anayechukia rushwa na ubadhirifu na kwamba anafaa kuwa Rais, wakati juzi tulisema hafai kuwa Waziri Mkuu na tukamtoa? Nilisema jana kuwa , CCM haipaswi ku-risk kuteua wagombea wenye mambo mengi ya kutolea maelezo kwa wananchi, ikifanya hivyo itaangushwa asubuhi ya saa nne. Watanzania wa leo siyo wa juzi.

Hii nchi bhana:confused:eti mtu dhaifu kama wewe hata hukuwahi kupata nafasi ya kuongoza wizara kwenye serikali dhaifu ya mjomba wako unautaka urais...mnafikiri ikulu ni msoga nini?hapa ni Lowassa au ukawa tu!
 
Back
Top Bottom