Urais 2015: Mtei amshukia Zitto


umeeleza vizuri sana na kwa hekima kubwa sana ila umesahau ishu ndogo sana...kutangaza nia kwa zzk kwa kipindi hiki ambacho chama kinaangaika kujijenga ni kudhoofisha chama kujijenga, mentally people will shift towards election...itasaidia nini zzk akiwa raisi huku ana wabunge 10??? Atatekeleza ilani ipi kama sio ya ccm??? Ishu ni right thing at a right time. Narudia : wakati wa msiba tuomboleze kama familia wakati wa sherehe tusherehekee kama familia. Ishu sio tuu kushika dola...ila pia ni kutawala
 
Kwa mara ya kwanza nampa like pasco ila tu zitto ana muda wa kujirekebisha ili kufanya kazi kitimu zaidi ndan ya chadema
 

Laiti ungemsikiliza Mkurugenzi wa habari na uenezi wa CDM John Mnyika jana alivyokuwa anajibu maswali ya Fina Mango usingethubutu kuandika ulichoandika.
CDM ni movement na njama yoyote ya kuidhoofisha hamtafanikiwa.Hayo ndiyo machache ninayoweza kukueleza kwa sasa.
 

Idiot!...Oohhh Boy!
 
CHADEMA ni chama makini, naamini kimekua na kuimarika vya kutosha pia naamini kinauwezo wa kustahimili swala la kumpata mgombea makini wa urais 2015 na kukiletea chama, madiwani wengi, wabunge na ushindi wa kishindo ktk kushika dola.
 
Idiot!...Oohhh Boy!
Ukiwa unaoga mtoni, akaja kichaa na kukuibia nguo zako zote na kuanza kukimbia nazo, ukitoka mtoni na kumkimbiza, watu watakao shuhudia mbio hizo, watawaona nyie wote wawili ni vichaa!.
Humu jf tuna vichaa kibao tuu ambao sio lazima mpaka waokote makopo!.
Kama aliyekuita wewe ni kichaa na wewe umejibu kwa kumtukana, sisi wasomoja tunawaona wote ni vichaa tuu japo mnatofautiana level!.
 
CDM ni movement na njama yoyote ya kuidhoofisha hamtafanikiwa.Hayo ndiyo machache ninayoweza kukueleza kwa sasa.
Umenikumbusha ule msemo wa
"Kuna njama za kuhujumu na kudhulumu...
sasa kumbe kuna njama za kuidhoofisha hiyo movement!,
Na ndio umetuhesabu akina sisi tuma na kutuambiwa "hatutafanikiwa!"
Asante na tuendelee, ila nakuomba uweke kwenye kumbukumbu zako
Matokeo ya 2015 ni "He who laugh last, laugh most"!.
P.
 

Mkuu wewe endelea kufanya kazi uliyotumwa kufanya.Maneno mengi ya nini? Sisi wengine tayari tunajua mwisho wake.
 

Thankyou for showing us your true colour.So you mean your Party CCM will laugh Last? Fantastic...!
 
Thankyou for showing us your true colour.So you mean your Party CCM will laugh Last? Fantastic...!
Mkuu Molemo, hili ni moja ya matatizo ya hawa ninao waita "manazi" wa Chadema waliotamalaki humu jf!, Kila ukitofautiana nao, basi unapachikwa kila aina ya majina!. Inaonekana CCM inawakosesha usingizi, manazi wa type yako, ndio maana kwenu kile anayewakosoa basi ni lazima awe katumwa na ni CCM!. Hivi siwezi kuwa CUF, TLP, UDP, NCCR-Mageuzi etc, lazima tuu niwe CCM?. Au kwa sababu mgombea wangu ni EL basi mimi ndio CCM!.

Dhamira yangu, tena with very clear conscious inanituma kufanya ukosoaji wa wazi wa vyama vyote. Niliwaambia "CCM Imechokwa", "Chadema haijajipanga" na "SUK kwa CUF ni imejichimbia kaburi". What matters most ni "the motive behind" ukosoaji huo!. At the end of the day, unaweza kuja kukuta sisi wakosoaji wa Chadema, ndio tunaisaidia zaidi Chadema kuliko nyie waimbiaji wa nyimbo za sifa, shangwe na mapambio!.

By the way, nimesikia ukitajwa kufanyia kazi Chadema makao makuu, ukipata fursa kuingia ofisini kwa Dr. Slaa, fungua lile buku la wageni, perusi perusi majina, utaliona jina la Pasco wa jf, huwa ninafika hapo from time to time na nitaendelea kufika as days go by!. Ila pia Lumumba huwa ninafika na kule Buguruni pia hutembelea!.
Kwa vile unaamini nimetumwa, nakushauri umshauri Dr. na Freeman, siku nyingine Pasco wa jf akitia mguu hapo Togo, arudishiwe mlangoni, asiruhusiwe hata kuingiza mguu ndani, maana umeshamshukia nitakuwa nimetumwa na CCM kuwapeleleza!.
P.
 

Ha..!Ha...!Haaaaa! Mkuu nimesoma gazeti la Mwananchi la leo na limesema Kambi ya EL inang'ara mikoani kote. BTW nadhani sasa unaelekea Courtyard kwenye mkutano wa Sumaye ambapo anatarajiwa kumlipua mtu wako.Ha....Haaaa...!
 
Uongozi ni hekima si tu kuangalia katiba.. mbona hujiulizi katiba ya ccm inaruhusu mtu yoyote kuwania uenyekiti wa chama lakini kwa taratibu zao mwenyekiti aliyeko hapingwi mpaka amalize muda wake.

Jiulize pia ndani ya ccm kuna wengi wanaoutaka urais ila kwa sasa wakiulizwa hutumia hekima kujibu na si kukurupuka maana haki ina mipaka na taratibu za kufuata, kimsingi kwa sasa chama kipo katika harakati za kujijenga na sio mbio za urais ndani ya chama sasa ingekuwa vema tukaona mikakati yake ya kukisaidia cdm kushika dola bila kujali nani atapeperusha bendera ya cdm 2015
 

Mkuu wangu wewe ni Genious.
 

Siwezi kupingana nawe kwani najua dhahiri Zitto tunaye katika mada hii tukijadili akiwa na ID nyingine, hivyo anajua nini kinaendelea, na wengine tunaoshindana nao humu tukifikiri ni wa Nape kumbe ni wa Zitto Kabwe au Zitto mwenyewe.
 


Kati yako na Zitto nani mnafiki? Zitto, Mnyika, Slaa, Mbowe na wengine wanatoa maoni yao hadharani wakitumia majina na utambulisho wao halisi. Wewe unamshambulia Zitto ukitumia jina Molemo. What is Molemo by the way. Najua una jina halisi, then kwa nini unajificha na ID za kiJF kumshambulia Zitto? Wewe ndiye mnafiki namba moja, maana nina uhakika wewe ni mmoja wapo wa waliopewa vijinafasi hapo CDM, na ukiwa na kiongozi wako Zitto unajifanya kumpigia makofi, lakini baadae ukirudi nyuma ya kompyuta unamponda. KAMA WEWE SIO MNAFIKI JITOKEZE HADHARANI KWA JINA LAKO, USEME UNAMPINGA ZITTO. Eti unaongelea mashujaa!!! Nitajie hata shujaa mmoja aliyewahi kuwa shujaa kwa kujificha na viji ID feki kwenye mitandao...
 

Mnafiki ni wewe namba moja.Mbona wewe umejificha na ID feki ya TUKO.Wewe ndiye mchochezi namba moja unayetaka tukiona mtu anavuruga chama tuogope kusema pole sana.Kama wewe sio mnafiki ungeanza kusema wewe ni nani? Kutumia majina halisi si hoja BTW unaweza kutumia majina halisi huku ukiwa na ID feki hata kumi.Huenda wewe ni mmoja wao na ninabishana na mtu mwenye ID hata kumi.
Usidhani kila mtu anayetetea ustaarabu ndani ya chama amepewa vijivyeo hapo CDM na wala usidhani kila mtu ana njaa kama ulivyo.
Unataka kunifundisha namna ya kutoa maoni hapa JF.Pole sana na umekosea sana.
Watu tuna uchungu na demokrasia na tunachelea kuona watu wachache wakigeuza demokrasia kuleta fujo.
Kwanini usimshauri huyo kipenzi wako asiwe mstaarabu kwa maslahi ya chama? Kwanini asiwe kama Mnyika au January Makamba? Kwani akifuata ushauri wa wazee wake ndani ya chama huo mwaka 2015 haitafika? Lazima sisi wengine tumwambie NO punguza spidi,jenga chama kama wenzako,tulia kama wenzako halafu kipenga kikipulizwa chukua fomu.Hapa kuna kosa gani? Hapa kashambuliwa au kaambiwa ukweli?
Ninakushangaa wewe TUKO unayeona swahiba wako kaonewa kwa kufundishwa ustahimilivu wa kisiasa.
Narudia tena kukuonya usitake kuchagulia watu cha kujadili hapa JF.Hakuna sheria yoyote iliyovunjwa,LAU kama kuna sheria nimevunja nishtaki kwa MODS wanifungie kwa sababu umeonyesha wewe ni dikteta mkubwa usiyependa kuona Swahiba wako akiguswa.Mtu mnafiki na mzandiki anajulikana tu kwa maneno yake kama wewe unayeshambulia mleta mada badala ya kujadili mada yenyewe.Huo ni uwendawazimu!
Samwel Sitta alisema mwanasiasa ni lazima uwe na ngozi ngumu sasa kama mnalalamika hivi kwa kuhoji tu matendo yenu kwa nia njema je,tukiwapa Urais mtaweza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…