Katika hali inayoashiria kuwapo kwa mgawanyiko mkubwa kuelekea katika kuteua mgombea urais ndani ya CCM na pia kumjibu Katibu Mwenezi wa CCM Bw. Nape Nauye, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga amesema hakuna aliye na hati miliki ya chama hicho kikongwe nchini!
Aidha Mgeja amewaonya viongozi wa chama hicho kuacha mara moja kuwatisha makada wake wanaotangaza nia ya kuwania nafasi ya kugombea urais kupitia CCM! Hii ni baada ya Nape kuweka vikwazo na hatua sita ambazo chama hicho kitazitumia kupata mgombea wake!
Chanzo: Magazeti asubuhi Star TV.
My take: Kuna uwezekano mkubwa tukashuhudia mtifuano ambao haujawahi kutokea tangu mwaka 1977 CCM ilipozaliwa! Tusubiri tuone sinema ya buree!!