Urais 2015: Khamis Mgeja atema cheche

Urais 2015: Khamis Mgeja atema cheche

Nape Mnauye aka Mnauye Jr ni member humu ndani, badala ya kuwatumia akina Msalani pale Lumumba aje humu apate elimu ya Bure...
 
Kwa mara nyingine wajumbe mbali mbali wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi wamezidi kukemea uhuni unaofanywa na baadhi ya makada wa chama hicho hasa Nape, kwa kutoa kauli za uchonganishi na bila kufata utaratibu na kanuni za chama.

Naomba nisiongee sana, pitia attachement hapo chini.

Asanteni
Ocampo four

Sasa yeye katumia vikao gani?
 
Nyinyi wenyewe mlikuwa mkisema Nape ni Kamanda oh mara Nape ni jembe, leo mnamuita muhuni mbona wana Lumumba hamueleweki, MAGAMBA YANA RUKA NA KUKANYAGANA. Kazi ipo
 
Membe ajiandae kiisaikolojia kuwa raia wa kawaida kwa kuwa
1.URAIS hatoupata,
2.UBUNGE,Jimbo la Mtama alishaaga ( Hatogombea),
3.Kikwete aliekuwa anambeba anamaliza muda wake.
 
Kwahiyo hapa Mzee Khamis Mgeja anamsema Nape kwa sababu anafukiria anamsema vibaya Lowassa. Cha ajabu anamsifia Kinana ambaye anafanya kazi na Nape! Sasa sijui anatumia kigezo gani kuwatenganisha wawili hawa?
 
mwaka huu kazi kweli kweli! mimi kama mwanachama wa ccm naweza nayaona yafuatayo;
1. Hakuna kiongozi hata mmoja ndani ya chama chetu ambae hayuko kwenye kundi la mgombea fulani kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
2.kuna viongozi ambao dhahili wanachukizwa na hali ya mambo iliyopo ndani ya ccm kuelekea uchaguzi mkuu na kura za maoni na kuna wengine ni wanafiki tu wanatengeneza mapito ya wanaopenda wapitishwe na chama.
3. kuna wanachama wenzetu ambao wao wanajiona ni wanachama wa daraja la juu kuliko wanachama wengine na wanaweza kumkaripia mwanachama mwenzao,kumtishia chochote na hata kumtengenezea scandle.
4.kuna wanachama wenzetu wachumia tumbo wanao taka fulani apitishwe ili walipwe fadhila wapewe vyeo ama vya kisiasa au kiutendaji kama si wao moja kwa moja basi ndugu zao na hali hii ni hatari sana kwa mstakabali wa nchi yetu maana taifa litakuwa na viongozi wajinga na wenye upeo mdogo wa uelewa wa mambo.
6.kuna kundi linalo penda kazi ya nape na kuna kundi linalo lia na nape usiku kucha kuwa hafai toka kapewa nafasi ya uenezi na kuna kundi lonalo mbariki nape na kazi zake zote.hawa wanaamini kuwa napenanaendana na kasi ya siasa za ushindani.
6.kuna mitandao hatari imeundwa na wagombea kutengeneza mikakati isiyo shindwa kuhakikisha wagombea wao wanapitishwa kwenye kura za maoni kwa gharama yoyote ile ikiwemo kuchafuana kwenye media n.k na hawa ndiyo mgenja analia nao bila shaka.
7.viongozi wa ccm akiwemo nauye wanahubiri sana kufuata misingi na taratibu za chama kwenye nafasi ya urais tu wakati hali iliyopo kwenye majimbo ni mbaya sana watu wanatamani kutoana roho na mbaya zaidi watu wa meandaa milima ya hela kwaajili ya ubunge tu.
Kwa mantiki hiyo alichp sema mzee mgenja hata kama mfuasi wa lowasa yilo sahihi inatakiwa ccm ichukuwe tahadhali nyingi dhidi ya makundi ya wagombea tofuti na hivyo ijiandae kwa mpasuko mkubwa ambao unaweza kugharimu sana chama kwenye uchaguzi ujap

Sina nyongeza
 
Back
Top Bottom