Ben Saanane
JF-Expert Member
- Jan 18, 2007
- 14,580
- 18,227
Turudi kwenye mjadala wa ESCROW kwanza maana Chenge ni mtuhumiwa pia
mwenye akili timamu atajua dhumuni la hii ngonjela yako.hakuna cha zaidi ya siasa chafu na kujaribu kufanya penitration kwa jamii to potray interest binafs against membe.ijulikane tu watu hawamchagui membe kwasababu ya gotham bali kwa kumwamni membe mwenyewe nakuona anafaa.ikitokea uthibitishe juu ya madai yako kwamba membe anabebwa na nyota ya mama salma will u be in a pisition.news with no source have no power to convice and converted to just a poem.INAWEZEKANA KATIKA UCHAGUZI UJAO AKAPATIKANA RAIS KUTOKA NJE YA CHAMA CHA MAPINDUZI LAKIN RAIS BORA ATAPATIKANA KUTOKA NDANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI MWENYE WEREDI MKUBWA MWAMINIFU MUADILIFU NA AMBAYE MWENYE NIA YA DHATI KABISA KATOKA KULITUMIKIA TAIFA PASIPO KUWA NA VIGUGUMIZI KATIKA MAAMUZI.MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE
Sasa Membe atabaki na nani wakuu??
atabaki na pesa za gadafi!Sasa Membe atabaki na nani wakuu??
Huyu chenge! kila pahala yupo, hadi kwenye "kuscrew"Turudi kwenye mjadala wa ESCROW kwanza maana Chenge ni mtuhumiwa pia
Hii vita yenu ya Urais kapiganeni baada ya kumaliza suala la Escrow.
Jitakaseni kwanza kutoka escrow ndio muanze kupambana.
Mushi unachosema ni sahii pinda namkubali sana yupo makini a ajua anafanya nini na anamalengo gani anahofu namungu huyo ndio rais tunaemuitaji.Sasa wandugu kwa hali ilivyo kwa sasa pinda taayari ameshanusa ikulu kila mtu sasa anakimbilia tunda zuri mtini Gotham simlaum ameona ni wapi kwenye muelekeo wa mafanikio na kwenye mikono ya hekima na busara.
Ana kashfa ya kula pesa za Ghaddafi, kashfa ya vitambulisho vya taifa, kuficha hela uarabuni, kuvujisha siri za serikali
atabaki na wapiga kura mkuu.ndiye kiongozi ambaye anaonekana anauwezo asiye na skendo za wiz.
NIMEKUFUATILIA VIZURI SANA.Mpambe nambari moja wa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa katika mbio za Urais nchini bwana Jack Steven Gotham anacheza miguu miwili kwenye siasa ya Urais, imebainika. Mpambe huyu ambaye ni maarufu kiasi kutokana na ukaribu wake na Membe, ndiye anayetajwa kufanya kazi ya ndani za Bernard Membe ikiwemo kufanya vikao vya kuwashawishi wajumbe wa NEC ya CCM wamuunge mkono Membe, kushika mkoba wa fedha za kuwalipa wajumbe na mikakati mingine. Jack sasa amepata jina jipya la Christian Ronaldo wa Urais.
Jack Gotham ni kijana wa karibu sana wa Membe ambaye amesaidiwa kupata mafanikio aliyonayo kiuchumi ikiwemo kushinda tenda ya Vitambulisho vya taifa, lakini hivi karibuni baada ya ujio wa waziri mkuu Mizengo Pinda katika mbio za Urais, Gotham ameyumba. Inasemekana kambi ya waziri mkuu ilikutana na Gotham kumuomba awe upande wao, kikao kilichofanyika nyumbani kwa kigogo mmoja eneo la Oysterbay jijini Dar es salaam. Bwana Gotham alitafakari na kuwaletea jibu baada ya siku chache kuwa anamuunga mkono Pinda kwakuwa Membe amekuwa hauziki na ni ngumu kumnadi kutokana na hulka na tabia yake ya kutokuwa karibu na watu.
Kwa kipindi chote cha katajwa kwa Pinda kwenye mbio za urais, msimamo wa Jack Gotham kwa Membe umeonekana kuyumba kwa kiasi kikubwa huku wakati mwingine aakionekana kuuma na kupuliza pande zote.
Jack Gotham anaendelea kukutana na vigogo wa juu wa team Pinda ikiwemo mke wa Pinda huku akimuhakikishia kuwa yeye Jack yako pamoja na Pinda katika mbio za Urais, na kwamba Membe ni rafiki yake, ila kwenye hili la Urais hauziki na hawezi.
Jack Gotham anaweza kumshambulia Edward Lowassa bila woga, lakini hana ubavu wa kumsema vibaya Pinda. Jack amewaelekeza baadhi ya vijana wa Membe kuwa wasimshambulie Pinda, jambo ambalo limeleta mgawanyiko makubwa.
Jack Gotham sasa ametunga udugu na Pinda, ambao anauita"ukaka". Amekaririwa akisema Pinda ni kaka yake na amemlea. Hii ni danganya toto ya kuficha usanii wake asionekane kuwa anamuunga mkono waziri mkuu Pinda. Hakuna udugu wowote baina ya wawili hawa, wala Pinda hakumlea Jack Gotham.
Jack Gotham anatoa siri za Membe kwa waziri mkuu Pinda lakini Pinda kwakuwa bado anamashaka nae amekuwa hampatii baadhi ya mipango yake ya ndani.
Jack Gotham anakutana na mzee Pinda na anavuta mzigo kama kawaida, huku pia akiendelea kukutana na waziri Membe na kuchukua dola za kimarekani.
Uamuzi huu wa Gotham katika mbio za urais unatajwa kumuweka katika wakati mgumu bwana Membe, kwakuwa kila siku ameendelea kupoteza wafuasi wake muhimu. Hata ukanda wa Pwani ambao ulikua ukiaminika kumuunga mkono, wajumbe wengi wa NEC wamemuhama Membe na kuhamia kwa mtoto wa mkulima. Mama Salma Kikwete anatajwa kuwa sasa ameanza kamchoka Membe na ameanza kujiondoa taratibu katika kumuunga mkono. Nyota ya mama Salma Kikwete ndiyo iliyokuwa inambeba Membe kisiasa na kufanya aungwe mkono ukanda wa Pwani.
Minong'ono imeanza kujitokeza kwa watu wa karibu na Membe juu ya msimamo wa meneja wao Jack Gotham. Aidha team Pinda pia imeanza kuhoji kwanini mtu huyu hachagui moja, kama anamuunga mkono Pinda au Membe. Hii inamuweka Gotham katika wakati mgumu na kumfananisha kama mtu aliyepanda farasi wawili, atapasuka msamba.
Jack Gotham ameamua kuwa Christian Ronaldo.
Kwa uchambuzi na maoni yako mkuu kwa sifa ulizozihainisha bila shaka atakuwa ni Mizengo Pinda ndiyo kiongozi pekee mwenye sifa hizo mwaminifu,muadilifu na huwa anafanya maamuzi sahihi na makini wakati wote huwa hakurupuki kama ambavyo wengine huwa wamekuwa wakikurupuka kwa kufanya maamuzi magumu yasiyo sahihi na kuitia serikali hasara kubwa tumeshuhudia kwa Edward Lowassa na kwa Membe pia