Nyangeta Marwa
Senior Member
- Nov 10, 2014
- 136
- 60
Mpambe nambari moja wa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa katika mbio za Urais nchini bwana Jack Steven Gotham anacheza miguu miwili kwenye siasa ya Urais, imebainika. Mpambe huyu ambaye ni maarufu kiasi kutokana na ukaribu wake na Membe, ndiye anayetajwa kufanya kazi ya ndani za Bernard Membe ikiwemo kufanya vikao vya kuwashawishi wajumbe wa NEC ya CCM wamuunge mkono Membe, kushika mkoba wa fedha za kuwalipa wajumbe na mikakati mingine. Jack sasa amepata jina jipya la Christian Ronaldo wa Urais.
Jack Gotham ni kijana wa karibu sana wa Membe ambaye amesaidiwa kupata mafanikio aliyonayo kiuchumi ikiwemo kushinda tenda ya Vitambulisho vya taifa, lakini hivi karibuni baada ya ujio wa waziri mkuu Mizengo Pinda katika mbio za Urais, Gotham ameyumba. Inasemekana kambi ya waziri mkuu ilikutana na Gotham kumuomba awe upande wao, kikao kilichofanyika nyumbani kwa kigogo mmoja eneo la Oysterbay jijini Dar es salaam. Bwana Gotham alitafakari na kuwaletea jibu baada ya siku chache kuwa anamuunga mkono Pinda kwakuwa Membe amekuwa hauziki na ni ngumu kumnadi kutokana na hulka na tabia yake ya kutokuwa karibu na watu.
Kwa kipindi chote cha katajwa kwa Pinda kwenye mbio za urais, msimamo wa Jack Gotham kwa Membe umeonekana kuyumba kwa kiasi kikubwa huku wakati mwingine aakionekana kuuma na kupuliza pande zote.
Jack Gotham anaendelea kukutana na vigogo wa juu wa team Pinda ikiwemo mke wa Pinda huku akimuhakikishia kuwa yeye Jack yako pamoja na Pinda katika mbio za Urais, na kwamba Membe ni rafiki yake, ila kwenye hili la Urais hauziki na hawezi.
Jack Gotham anaweza kumshambulia Edward Lowassa bila woga, lakini hana ubavu wa kumsema vibaya Pinda. Jack amewaelekeza baadhi ya vijana wa Membe kuwa wasimshambulie Pinda, jambo ambalo limeleta mgawanyiko makubwa.
Jack Gotham sasa ametunga udugu na Pinda, ambao anauita"ukaka". Amekaririwa akisema Pinda ni kaka yake na amemlea. Hii ni danganya toto ya kuficha usanii wake asionekane kuwa anamuunga mkono waziri mkuu Pinda. Hakuna udugu wowote baina ya wawili hawa, wala Pinda hakumlea Jack Gotham.
Jack Gotham anatoa siri za Membe kwa waziri mkuu Pinda lakini Pinda kwakuwa bado anamashaka nae amekuwa hampatii baadhi ya mipango yake ya ndani.
Jack Gotham anakutana na mzee Pinda na anavuta mzigo kama kawaida, huku pia akiendelea kukutana na waziri Membe na kuchukua dola za kimarekani.
Uamuzi huu wa Gotham katika mbio za urais unatajwa kumuweka katika wakati mgumu bwana Membe, kwakuwa kila siku ameendelea kupoteza wafuasi wake muhimu. Hata ukanda wa Pwani ambao ulikua ukiaminika kumuunga mkono, wajumbe wengi wa NEC wamemuhama Membe na kuhamia kwa mtoto wa mkulima. Mama Salma Kikwete anatajwa kuwa sasa ameanza kamchoka Membe na ameanza kujiondoa taratibu katika kumuunga mkono. Nyota ya mama Salma Kikwete ndiyo iliyokuwa inambeba Membe kisiasa na kufanya aungwe mkono ukanda wa Pwani.
Minong'ono imeanza kujitokeza kwa watu wa karibu na Membe juu ya msimamo wa meneja wao Jack Gotham. Aidha team Pinda pia imeanza kuhoji kwanini mtu huyu hachagui moja, kama anamuunga mkono Pinda au Membe. Hii inamuweka Gotham katika wakati mgumu na kumfananisha kama mtu aliyepanda farasi wawili, atapasuka msamba.
Jack Gotham ameamua kuwa Christian Ronaldo.