Dual citizenship ! for whose benefit? The reasons given to support dual citizenship are weak and they are intended to give some powerful political leaders and some elites an opportunity to avoid charges or blunders they might do in one country by escaping to another country. Some people support the idea of dual citizenship by saying that it will facilitate more investment in the country and enable Tanzanians to live freely and being able to be employed permanently in other countries - this is good and we support it. The questions are: In which country Tanzanians with dual citizenship stand up for in times of crisis between the two nations? Can't we see that this idea will give the imperialists chances to plant their puppets in weaker countries like Tanzania? And lastly, what guarantee us that these Tanzanians with dual citizenship will be helpful and supportive to Tanzania?
India na China mfano kampuni nyingi za Technologia zimeanzishwa na wananchi wao walioenda kusoma nje kufanya kazi na kurudi nyumbani.
Vipi pale aliposema diaspora ni muhimu sana kiasi kwamba Nigeria huwa wanapanga kupindua nchi ili watoe wakimbizi watakaopata makaratasi nje!!! Wanaambiana nipindue, nisipindue sasa hivi? Fulani we pindua! Wakati huo wanakuwa wameshaandaa wakimbizi!!Ndugai anawaongelea "hawa Wazanzibari" kama ni aliens, anawakandya wabunge kwamba hawajui kitu bila qualification.
Membe anakwambia New York (City) kuna Wa Nigeria milioni nne, wakati population nzima ya NYC ni milioni 8.3, sasa hao Wa Nigeria wanafika takriban nusu ya watu wote NYC?
Kaenda kumvua nguo mzee wa watu Amil Jamal na jinsi alivyofariki kwa kukosa matibabu Canada kwa sababu hakuwa na uraia, Jamal kajifia na dignity yake mawazoni mwa Watanzania, leo Membe kamvua dignity yote.
Kaanika magonjwa ya mapacha waliokuwa wanaumwa "sickle cells" na kuhudumiwa na Wizara ya Mambo ya Nje kama mtu asiyejua kwamba habari za ugonjwa wa mtu ni jambo la faragha.
Huyu ni mtu aliyesoma John Hopkins!
Halafu ni top diplomat nchini, hata kuongea suave with savoir faire tu hajui.
Faux paus left right and center.
Halafu unaambiwa huyu ni top contender kwenye presidential race, ana some semblance of being a frontrunner with realistic chances if he can ward off the Lowassa locomotive.
Wabongo tusishangae tukapata rais halafu tukasema "bora hata ya Kikwete"
Vipi pale aliposema diaspora ni muhimu sana kiasi kwamba Nigeria huwa wanapanga kupindua nchi ili watoe wakimbizi watakaopata makaratasi nje!!! Wanaambiana nipindue, nisipindue sasa hivi? Fulani we pindua! Wakati huo wanakuwa wameshaandaa wakimbizi!!
Sasa jamani kama una uwezo wa kupindua nchi ukashika madaraka kwa nini usuke mpango wa kupata makaratasi ya kwenda kupiga box ilhali nyumbani unaweza kusuka mpango wa kupindua nchi na umeshapindua? Kwa nini uondoke? Hahahahahaaaaa....
Halafu Membe kasema hao watoto mapacha wa balozi Canada mwisho wa siku waliwaajiri. I am sure itakuwa ni hapo kwake foreign kama maafisa ubalozi kwa sababu kasema waliendelea kuishi Canada. Question is, walikuwa na qualification au ni kwa vile walikuwa wanaumwa sickle cell au ni kwa vile ni watoto wa wakubwa? Yani anazidi kuthibitisha bila hata aibu wala kuogopa kilio cha Watanzania wengi kwamba watoto wa viongozi huwa wanabebwa, tena wizara moja inayoongoza kwa hilo hiyo ni foreign affairs.
Kuna jamaa mmoja mtoto wa wakubwa (tena wakubwa waliostaafu bado wanafagiliwa sijui kwa nini), kuna wakati mkewe alifukuzwa kwa kukosa makaratasi ugenini, babaake akaenda kazini, tena wakati huo ndio mmoja wa ma head honcho wa nchi, within one week Tanzania ikamuajiri huyo dada foreign affairs na kum post alipofukuziwa, akapewa visa ya utumishi wa kibalozi, immigration waliomfukuza walikoma na wabongo.... Na ndio hawa viongozi type za kina Membe hawa, hawana sense of equal opportunity. Tena kina Membe wametoka vijijini huko, wameona shida kibao, lakini wanawasahau walikotokea, utadhani Membe alikuwa hajawahi kuona watoto wenye sickle cell kwao Mtwara huko ambao hawana mtu wa kuwapigia mapande wakatibiwe au kuajiriwa foreign affairs.
Kwa Mzee Amir Habib Jamal, alikuwa mtu mzima na mgonjwa. Uraia wa Kanada unampa huduma ya bure ya afya na kiinua mgongo cha kila mwezi kwa wazee wastaafu kama yeye. Kwa nini amsubiri Nyerere kumsaidia wakati watoto wake ni raia wa Kanada na wanajua faida yake kwa mzee wao hasa ukizingatia kuwa hawakuwa matajiri.KUUMWA KWA MZEE JAMAL,AGIZO LA MWL NYERERE NA UTEKELEZAJI WA MEMBE KUHUSU SERA YA URAIA PACHA.
Jana niliahidi kuendelea na simulizi kuhusu mambo kadhaa yamhuhusuyo Ndg.Bernard Kamilius Membe na siasa za nchi yetu.Simulizi hizi zipo katika mtindo wa "series".Kila "episode" ya "series" hizi itahusisha matukio muhimu yasiyo maarufu kwa watu wengi lakini yana mvuto wa kipekee katika wasifu wa Ndg.Bernard Kamilius Membe.
Nitaendelea nilipoishia jana......
Baada ya Mwl.Julius Kambarage Nyerere kumpatia majibu Ndg.Bernard Kamilius Membe kuhusu swali la Ndg.Jakaya Mrisho Kikwete juu ya ushiriki wa vijana kwenye kinyang'anyiro cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 uliojumuisha vyama vingi,likaibuka suala la ugonjwa na matibabu ya aliyewahi kuwa waziri wake wa fedha enzi za uongozi wake aliyeitwa Mzee Jamal.
Kwa vijana wa sasa wasiomjua Mzee Jamal huyu alikuwa waziri wa fedha katika serikali ya awamu ya kwanza chini ya uongozi wa Mwl.Julius Kambarage Nyerere.Alikuwa na asili ya kihindi.Lakini ni mzawa wa nchini Tanzania.
Alikuwa mfanyabiashara,raia mwema aliyeshiriki katika mapambano ya kupigania uhuru tangu enzi za TANU hadi pale ilipozaliwa CCM.
Baadaye aliachana na siasa.Akarejea katika shughuli zake binafsi.Na hata umri ulipomtupa mkono alisafiri kuishi na mwanaye nchini Canada hadi umauti ulipomfika.Alikuwa rafiki mkubwa wa Mwl.Julius Kambarage Nyerere.
Wakati wa mazungumzo yao mengine Ndg.Bernard Kamilius Membe alimjulisha Mwl.Julius Kambarage Nyerere juu ya hali ya afya ya rafiki yake wa muda mrefu Mzee Jamal.
Kwa wakati huo Mzee Jamal alikuwa akiumwa sana.Na gharama za matibabu zilikuwa juu sana nchini Canada hivyo kufanya familia yake kushindwa kuzimudu ipasavyo.
Pamoja na kuwa mfanyabiashara miaka ya nyuma na kuwahi kuwa waziri wa fedha enzi za Mwl.Julius Kambarage Nyerere lakini hakuweza kujilimbikizia mali wala kukwepa kodi.
Baada ya Mwl.Julius Kambarage Nyerere kuelezwa na Ndg.Bernard Kamilius Membe kuhusu kuumwa kwa Mzee Jamal ilibidi Mwl.Julius Kambarage Nyerere aombe ofisi za ubalozi kupelekwa siku inayofuata kumwona na kumjulia hali rafiki yake Mzee Jamal.
Siku iliyofuatia alipelekwa akiambatana na Ndg.Bernard Kamilius Membe.Hali aliyomkuta nayo Mzee Jamal haikuwa nzuri sana.Mtoto wake alilia sana akiomba msaada wa kugharamiwa matibabu na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ubalozi uliopo Canada.
Mwl.Julius Kambarage Nyerere aliumizwa sana na hali ile.Akamwagiza Ndg.Bernard Kamilius Membe kuzungumza na Balozi wetu wakati huo nchini Canada ili apate mihadi ya kuonana na waziri mkuu wa Canada wa wakati huo ambaye alikuwa na mahusiano naye mazuri.Nia ni kuzungumzia suala la matibabu ya Mzee Jamal.
Baada ya waziri mkuu wa Canada kuridhia kuonana na Mwl.Julius Kambarage Nyerere siku ilipowadia Mwl.Julius Kambarage Nyerere aliambatana na Ndg.Bernard Kamilius Membe katika kikao kila na waziri mkuu wa Canada.
Mazungumzo yalikuwa na ajenda moja tu ya matibabu ya Mzee Jamal.Mwl.Julius Kambarage Nyerere aliomba msaada wa matibabu bure kwa Mzee Jamal kwasababu familia yake haimudu gharama zake na hali ya Mzee Jamal inazidi kuwa mbaya kila siku iendayo kwa Mungu.
Waziri mkuu wa Canada aliridhia kusaidia gharama za matibabu ya Mzee Jamal lakini akishauri kuwa kwakuwa nchini kwake matibabu ni bure(kwa wakati ule-sijajua kwasasa)lakini kwa mtu mwenye uraia hivyobasi akaagiza Mzee Jamal apatiwe hati ya kusafiria ya Canada na uraia kamili wa Canada.Alifanya hivi kwasababu wao wanaridhia uraia pacha(dual citizenship)lakini kwakuwa Tanzania hatuna sera hii basi ni lazima Mzee Jamal aukane uraia wake wa Tanzania na kupatiwa wa Canada.
Kwa mazingira ya wakati ule Mwl.Julius Kambarage Nyerere na familia ya Mzee Jamal hawakuwa na namna nyingine zaidi ya kukubaliana na ushauri wa waziri mkuu wa Canada ili kuokoa maisha ya Mzee Jamal.
Baada ya kikao kile jukumu la kushughulikia suala la uraia wa Mzee Jamal likakabidhiwa kwa mamlaka husika ya serikali ya Canada na ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pale Canada ukawa na jukumu la kuwasilisha nyaraka muhimu za Mzee Jamal zitakazosaidia kuthibitisha uraia wake wa Tanzania kabla ya kuhamia katika uraia wa Canada.Na ubalozi ukampatia jukumu la kuratibu hili suala Ndg.Bernard Kamilius Membe.
Kwakuwa Mwl.Julius Kambarage Nyerere alikuwa na majukumu mengine katika hizo ziara zake ilimlazimu aendelee na majukumu hayo.Lakini aliambatana na Ndg.Bernard Kamilius Membe kwenda kumuaga Mzee Jamal na familia yake.Wakati akiwa uwanja wa ndege wa nchini Canada baada ya kutoka kumuaga Mzee Jamal na familia yake akielekea nchini Marekani Mwl.Julius Kambarage Nyerere alimwambia Ndg.Bernard Kamilius Membe kuwa ipo haja ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuridhia suala la uraia pacha(dual citizenship)ambao wakati wa uongozi wake waliukataa lakini changamoto ya suala la matibabu ya Mzee Jamal limempa tafakuri kubwa sana.
Siku chache mbeleni tangu Mwl.Julius Kambarage Nyerere aondoke kuelekea nchini Marekani huku nyuma Ndg.Bernard Kamilius Membe kwa kushirikiana na serikali ya nchini Canada na ofisi za ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Canada walifanikisha kupatikana kwa uraia kamili wa Canada wa Mzee Jamal na kuijulisha familia ya Mzee Jamal kuwa wamwandae baba yao kwa ajili ya kufuatwa akaanze matibabu chini ya uangalizi wa serikali ya Canada kwa maelekezo ya waziri mkuu wa Canada.
Siku ya kwenda kumchukua Mzee Jamal ili akaanze matibabu Ndg.Bernard Kamilius Membe akiambatana na ujumbe wa serikali ya Canada nyumbani kwa Mzee Jamal kwa bahati mbaya walipofika tu wakakuta msiba.Mzee Jamal alikuwa kafariki muda mchache kabla ya wao kufika pale.Lilikuwa ni pigo kubwa kwa familia,serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali ya Canada.Kubwa zaidi Mwl.Julius Kambarage Nyerere aliumia sana alipopata zile taarifa.Rafiki yake mkubwa alikuwa kaaga dunia.
Na hii ndio ikawa sababu kuu ya Ndg.Bernard Kamilius Membe kuwasilisha hoja kuwa katika mchakato wa katiba mpya wakati akiwa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa kiwepo kipengele kinachozungumzia suala la uraia pacha(dual citizenship).
Na alitoa sababu muhimu zenye mashiko ili uraia pacha(dual citizenship)iwe ni haki ya kila mtanzania huku suala la Mzee Jamal ikiwa ni moja kati ya "precedents" zinayoishi hadi leo.
Nihitimishe kwa kusema tu kwamba uraia pacha(dual citizenship)haikuwa hoja binafsi ya Ndg.Bernard Kamilius Membe bali ilikuwa na chimbuko lake.Na uzuri wa hoja hii Mwl.Julius Kambarage Nyerere aliweza kumshirikisha hata Mzee Kingunge Ngombale Mwiru miaka ile wakati akimwelezea hali aliyomkuta nayo Mzee Jamal nchini Canada kabla ya umauti kumfika.
Je unajua kwamba "wanamtandao" walikuwa watano tu?
Tukutane tena kesho muda kama huu.......