Hiyo ni sawa na mtu kufuga mnyama pori kama Simba au Tiger.
Wanazoeana kiasi cha kucheza na kufurahi pamoja.
Siku ya siku huyo mnyama pori anamchenjia na kumrarua huyo mtu na ama kumuua kabisa au kumwachia kilema cha maisha.
Roy Horn wa Siegfried & Roy mpaka leo hayuko sawa. Kapooza kwa kiasi fulani.
Diana Hanson naye aliraruliwa hadi kufa na Simba ambaye walikuwa wamezoeana.
Mwingine, Dawn Brancheau, ambaye alikuwa mkufunzi wa wanyama naye aliuliwa na nyangumi aitwaye Tillikum. Huyu mdada alikuwa kazoeana sana na huyu nyangumi kiasi cha kumchumu na kumchezea chezea utadhani alikuwa babu yake.
Sasa hayo ya urafiki na jinsia tofauti hayana tofauti sana na hayo matukio ya wanyama pori kuwachenjia watu waliowazoea. Fursa ikijitokeza na ijitokeze katika wakati muafaka basi sina shaka ya kwamba huo urafiki unaweza ukaenda mbele zaidi na wahusika kujikuta wakifanya mambo ambayo hayafanywi na marafiki wa kawaida na kufanya yale yanayofanywa na watu wenye uhusiano wa kingono au kimapenzi.