Bukyanagandi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2009
- 11,626
- 18,228
Bukyanagandi,
Kama unasema kabila la JPM linajulikana ni KABILA GANI?Mbona hulitaji?Umesema JPM anatoka Chato iliyokuwa mkoa wa Kagera na sasa Chato iko Geita baada ya mgawanyo wa mikoa na Wilaya!
Wasukuma wako Mwanza, Shinyanga na Mara kidogo lakini kwa Chato wengi ni Wahaya,Wanyambo,Wazinza na makabila yote haya yana ukaribu na kiasi cha kuoleana.
Hivi unaweza kujuua uhusiano ulipo kati ya Museveveni na Kabila?
Yes mkuu Makoye 2009, sasa kuhusu uhusiano kati ya M7 na Kabila hapo ujafafanua vizuri mkuu, unauliza uhusiano wa kindugu/damu au wa kisiasa? Kitu kingine unataka tumzungumzie Kabila yupi? Kabila Jr au Sr fafanua kidogo mkuu.
Kabla ujajibu - mimi ntazungumzia Kabila Sr, yeye alikuwa mfuasi wa itikadi za Lumumba na alikuwa anampinga Mobutu hivyo akanzisha vita vya msituni vyenye lengo la kumuondoa madarakani Mobutu, operation zake kivita azikufanikiwa sana kutokana na kutokuwa commited 100% na vita vya ukombozi, alikuwa interested na mambo ya starehe na wanawake - weakness hii ilimsikitisha sana Mpiganaji Che Guevara ambaye wakati huo alikuwa ni Waziri chini ya Fidel Castro huko Cuba, lakini aliamua kuacha kazi na kuja Africa kwa siri na wanajeshi wachache kwa nia ya kuja kumsaidia Kabila kuwapa mafunzo wapiganaji wa Kabila katika msitu wa Congo alishiriki vile vile katika mapambano ya kuvizia dhidi ya jeshi la Mobutu chini ya ushauri wa CIA.
Che Guevara alikaa miezi tisa kama nakumbuka vizuri, lakini attitude za Kabila 2wards armed struggle zilimkatisha tamaa, straw ya mwisho ilitokea wakati walipo safiri kuja Dar kutoka porini DRC, walikuja kuchukua mizigo fulani na fedha zilizo kuwa donated na socialist countries kusaidia katika masuala ya ukombozi.
Kabila na Che walipo wasili Dar wakitokea Kigoma kwa Train kwa usalama wao wakawa wanalala hoteli tofauti, walikaa kwa muda wakifatilia kilicho waleta baada ya kufanikiwa - baadae walipanga siku ya kukutana kwa kupanga mikakati yao, siku waliyo panga kukutana Che aliondoka Hotel aliyofikia kwenda kukutana na Kabali Hotelini kwake, Che anaingia barabarani na kuanza kuembea kwa miguu ghafla anakutana na Kabila ameshikiria usukani wa Mercedes Benz i.e anaendesha!!! Che alishikwa na butwaa mwenzake kumbe peza anaziunguza kwenye matanuzi, siku nyingine wakakubaliana wakutane Hoteli aliyo fikia Che Guavara, kesho yake Che kasubiri wee Kabila aonekani!! Che kakata shauri kumfuata Kabila Hotelini, Che kufika Chumba cha Kabila alikuta mlango ajafungwa kwa ufunguo Che kufungua mlango akamkuta Kabila akiwa na wanawake watatu (sikumbuki vizuri) sijui wanne kitandani - Che kafunga mlango kwa nguvu na kuondoka zake huku amekasirika kweli kweli, baada ya siku chache kupita Che akahamua kurudi kwenye Msitu wa Congo kuwafuata wanajeshi aliyo kuja nao kutoka Cuba wakarudi wote Dar na kuondoka kurudi Cuba kupitia iliyokuwa Ujerumani Mashariki.
Kwenye simulizi zake Che anasema kwamba Kabila awezi ku-organise a credible fighting force kama atajidai kwamba anaweza basi hiyo itakuwa sawa sawa na ndoto za mchana, akasema tatizo lake ni kuendekeza sana starehe kuliko kutaka kuwakomboa Wafrica wenzake. Kwa kifupi kabisa hayo ndio maoni ya Che kuhusu Kabila Sr.
Sasa tuje uhusiano wa M7 na Kabila - again sijui unazungumzia Kabila yupi Sr au Jr - kama ni Kabila Sr - huyo aliwahi kuishi Uganda na familia yake under assumed name akiwa anaendeleza harakati zake za ukombozi huku akifanya biashara, sasa sijui walikuwa na ukaribu gani na M7 zaidi ya kupanga mbinu za kumuondoa madarakani Mobutu kwa kupigana vita kamili wakishirikiana na jeshi la PK, lakini wakati wanapanga hayo Kabila na familia yake alikwisha hamia Dar kwa miaka mingi akijiita Mfipa kwa jina ya O'Mutwale of course O'Mutwale ni Kiganda/Kinyankole/Kihaya kama sikosei.
M7 na Kabila Sr hawana undugu wowote walikuwa ni ma comrade in arm basi i.e wenye lengo moja kuingia madarakani kwa kutumia mtutu wa bunduki na walifanikiwa.
Tukienda mbali kidogo ni hivi: M7 ni Munyankole mwenye damu ya Kihima kama alivyo Mh.Kagame - wakati Kabila alikuwa Mkongomani wa mashariki ya Congo wenye asili ya kabila la Kimanyema kama walivyo baadhi ya wenyeji wa Kigoma, hivyo sidhani kama Kabila Sr ana damu ya Kihima hata kidogo.
Linapo kuja suala la
Kabila Jr (Rais wa sasa DRC) huyo is a different story iliyo ghubikwa na utata mtupu!!!. Nadhani nime eleweka mkuu.