Niliwahi kuwa na rafiki anaitwa Daudi.
Huyu nilikutana nae shule ya msingi na chanzo cha ubest ni ukorofi wake.
Basi daudi alikuwa na kundi lake la uonevu ikatokea akawa best na kuwa ananilinda shule,,, miaka ikaenda tukamaliza.......
Secondary siku hiyo kukawa na disco shuleni kumbe ile shule jirani alikuwa anasoma daudi tukakutana tena story story pale akanitambulisha kama dada yake. pia akawa ananilinda mpaka nikamaliza.
Miaka ikaenda tukamaliza tukaja kukutana tena chuo. chuo tuliishi kama ndugu ndugu kabisa.
Basi kuna siku nikaja kuitwa niende block no 10 kufika namkuta daudi anaumwa sana. nilimuuguza kama wiki mbili hivi akapona!! alivyopona akaniambia leo umenipa hisia za mama sitakusahau.
Basi tulifanikiwa kumaliza,,, sasa ule u best siku ya kuagana tulikumbatiana lia sana pale..... Daudi alilia sana akaanza kuniambia story yake.
kamaliza chuo hana pa kwenda!! Mama yake alifariki siku aliyozaliwa na baada ya hapo baba yake alioa mke mwingine sasa kule nyumbani kuna mateso sana hawezi kurudi ni bora aende mbele yeye ni mwanaume atajua la kufanya.
Alikuwa na mshikaji wake mwanza akaenda huko.
Baada ya miaka mingi nikakutana na daudi kwenye harakati za maisha. akaniambia ameoa na ana mtoto.
Basi ikapita miaka mingi sana tena siku hiyo nikapokea simu nikapewa taarifa za msiba.
Daudi alikutwa mpakani kabanga amekufa na akiwa ametobolewa macho. katika vitu alivyokutwa navyo ni address yangu, na barua yenye mambo ambayo hakuweza kunieleza.
Nilikuta wamesha mzika,, kwenye barua nilipata maelekezo ya mtoto alipo na nilienda kumchukua maana yule mke walitengana mtoto alikuwa kwa rafiki yake.
Mule ndani ya barua aliandika kuna sehemu aliandika hivi " nisamehe kwa kuoa lakini natafuta pesa niweze kukuoa kwani maisha yamenifanya nioe bila kupenda nakupenda na nitakupenda daima". kama unavyojua maisha ya yatima lazima nikuhakikishie usalama utakao kulinda maisha yako yote.
barua ile ilikuwa ina vitu vya majonzi sana maana alijielezea kama akijua anakufq
nilimfuata kijana na niko naye mpka leo maana ndani ya barua aliomba sana nisimpeleke na asilelewe na watu wa kwao
Kijana ni genz yuko form three anafanana na baba yake sana!!!!
Mimi zaidi ya best best yangu aliniachia zawadi ya mtoto.