Urafiki: Sababu za marafiki kutengana

Urafiki: Sababu za marafiki kutengana

The Alchemist

Senior Member
Joined
Jun 15, 2016
Posts
177
Reaction score
148
Wakuu, kuna mwenye rafiki wa utotoni ambaye siyo marafiki tena. Kwa namna moja ama nyingine, kuna marafiki ulikuwa nao leo haupo nao tena. Nini sababu?

Kuna sababu mbalimbali ambazo hufanya marafiki kutengana. Sijui kama hii thread ipo, ila kama ipo nisamehewe.

Sababu hizi ni kama;

1) Kubadilika kwa maisha:- ndoa, kuolewa/kuoa, kupata mtoto, kazi n.k. Kama mmoja akiolewa basi hutenga zaidi muda na kuwa na familia na urafiki uwekwa pembeni na pengine kwisha kabisa. Akipata kazi, basi, huweka zaidi muda kwenye kazi usika na muda wa urafiki upungua na gap kuwa kubwa mara dufu na mwisho urafiki uisha. Kama kazi ni mkoa ama nchi tofauti, basi urafiki uwa atarini zaidi. Pia, kuwa na watoto yaweza kuwa sababu inayoendana na hizi.

2) Kutofautiana kimtizamo:- Huku kuletwa na ukuaji na pengine kupevuka kwa fikra. Mitazamo ipo mingi. Kimsingi, hii haiwezi kuwa sababu lakini, sadly huwa sababu. Yaweza kuwa mitizamo ya kimaisha, kisiasa ama kiimani. Pia, kukua kwaweza kuwaweka marafiki katika fikra tofauti na hivyo kuwafanya kutengana. Tabia za utotoni ama za shule zaweza kubadilika na kuleta utengano.

3) Kukosekana kwa uaminifu:- hii yaweza kusababishwa na usaliti, uongo ama umbea. Hii inajieleza wazi na yenyewe hivyo haitohitaji nyama.

Ifikapo atua hii, wanaweza kurudiana? Wataalamu wanasema kwamba, urafiki wa kweli hauishi na ata kama wakitengana, wakikutana uendelea pale pale walipoishia.

Ndugu, tushirikishane, wewe ni nini unadhani kinafanya usiwe na rafiki ambaye ulikua ama ulikuwa naye? Mnaweza murudisha urafiki.

I am The Alchemist.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rafiki yangu wa utotoni akageuka kua mpenzi wangu, baadae tukatenganishwa na shule hatimaye nchi, tumekutana ukubwani hakuna tena chochote ingawa yeye bado yupo single,

Rafiki mwingine tulitenganishwa na kukua i think, akawa na tabia tofauti sikuzivumilia,

Rafiki wa chuo mwingine aligeuka kua mpenzi, wivu ulimzidia nikaona ataniyumbisha tukaachana for good,

Kwa sasa rafiki yangu ni mpenzi wangu na my cousins sina mpango wa kurudisha marafiki wa zamani.
 
Rafiki yangu toka chekechea, msingi, secondary tulitengana sababu ya kutafuta maisha hadi sasa sina rafiki mkubwa kama yule saivi na watu wa karibu tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ili udum katika urafiki unapaswa kua na mipaka ya faragha katika maisha yako, ujue chakushare na rafiki na cha kukeep mwenyewe...
usimwamini binadam hata uwe na ukaribu nae kiasi gan
 
Back
Top Bottom