Upweke unanimaliza, naombeni msaada

Upweke unanimaliza, naombeni msaada

No wife, no kids, no job and still live in my mother place.

Wakuu, nimemaliza chuo four years previously baada ya kusoma sana kwa shida kutokana na kutokuwa na wa kunilipia ada. Toka nimemalize mpaka leo sijapata kazi zaidi ya kufanya kazi ngumu kama porter mlima Kilimanjaro na wakati mwingine nikawa napata za kufunga hema mbuga za wanyama ama kufua nguo za wageni, lakini toka rais aanze kubana na kazi zenyewe hazionekani tena.

Nipo kwenye nyumba ya mama till now na miaka ndio inayoyoma sana coz am over 30 saa ingine uwa naona ata aibu kutembea barabarani. Pamoja na hayo sina ata mtoto ila to be honest I wish even to have a single child, girls today are really tough to handle and I can't afford them, nimebaki njia panda sijui nilisoma ya nini ningejua maisha yangewa magumu hivi ningempa mtu mimba kipindi nipo chuo coz kuna fursa nilikuwa nazipuuzia.

Naombeni ushauri wenu wakuu labda utanisaidia na kunipa mwanga maana maisha yamekuwa magumu sana.
Polesana mkuu Mungu atakusaidia usikate tamaa
 
Thanks mkuu, unajua sio rahisi kuwa na mchumba ata hela huna ata akiwa na kazi ni pagumu pia anaweza kukukimbia, ofcoz nimeplan kama nikifanikiwa kupata kamtaji nianze ujasiriamali naona kama utanipaI mwanga zaidi
Hii ndio shida ya kusomea fani nyepesinyepesi
 
Sasa huyo mtoto atalelewa na nani? Au nae atakuwa mzigo wa bibi? Shughulika na changamoto moja ndio uwaze nyingine.
Mwanaume hakati tamaa.
 
Sasa huyo mtoto atalelewa na nani? Au nae atakuwa mzigo wa bibi? Shughulika na changamoto ya moja ndio uwaze nyingine.
Mwanaume hakati tamaa.
Hata wanawake msikatee
 
Pole sana , kama ulivyo kaza buti hadi kupata elimu pia inabidi usikate tamaa session hii uliopo sasa kwani ndio inahitaji uvumilivu na jitihada zaidi yaani ukaze buti zaidi na zaidi na utafanikiwa kupata kazi unayohitaji
 
Pole sana mkuu
Ipo sku watanzania tutaiona nuru tena
 
Mungu akutie nguvu kaka,Akujalie upate mafanikio.
 
Back
Top Bottom