upuuzi wa ccm na VIBARAKA WAKE;

upuuzi wa ccm na VIBARAKA WAKE;

Ujitazame wewe mwenyewe kama umeandika cha maana badala ya kuhangaika kumkejeli mwenzako"
1. ".. kwamba Chadema inakubalika Arusha...hilo liko wazi na kwa watu wenye akili kubwa na uelewa kama sisi tunalitambua hilo,isipokuwa tatizo ni kwamba hakuna amani Arusha" Hapo umeeleza nini cha maana? umeeleza kwamba liko wazi kwako unayejidai kwamba una akili bali kinachokutatiza ni kutokuwepo amani. Umeshindwa kutueleza kinachosababisha ukosefu wa amani lakini bado unajidai una akili. Kama ni CCM ueleze ni kwa vipi na kama ni CDM ni kwa namna gani na utoe vielelezo vinginevyo ulichoandika ni ----- tu. Mimi kwa maoni yangu yanayosababishwa Arusha yanatokana na dola ya nchi ambayo inaundwa na seriakali ya CCM yenye wajibu wa kulinda amani.Muda haunirusu kueleza kwa kina.

2. "walipaswa kutumia mwanya huo kuliweka jiji la Arusha...sasa wangetumia kuweka kila kitu sawa". Mwanya upi na waweke sawa nini? Hivi unapotoa nadharia isiyo na ufafanuzi wowote inamsadia nani.Viongozi wa CDM wananya kazi ya Siasa na wala hawapo kwenye uongozi wa dola. Wanafanya kazi ya kuwashawishi wananchi wawachague viongozi wa chama chao lakini wenye dola ni wengine. Kwa bahati CCM inaitumia dola vibaya kwani inawaagizi wakuu wa mikoa na wilaya na polisi kufanya mambo ya ajabu kama waliyofanya mara nyingi.

3."kila vurugu na mauaji ya watu ni lazima zitokee kwenye mkutano wa chadema,ok.yawezekana ni wapinzani wao CCM...Great Thinker walipaswa kubadili mbinu na kutumia mbinu nyingine katika kufanya siasa zao." Kama unaamini wanaoleta mauaji kwenye mikutano ya CDM ni CCM, suala siyo viongozi wa CDM wabadili mbinu bali ungewashauri CCM waache maaji maana siyo jambo halali. Unashauri watumie mbinu gani? Nadhani huelewi unachokisema. Watu waliokuwa katika mkutano wa kisiasa, hawafanyi vurugu yoyote wala hawamkashifu mtu yoyote, wanaorushiwa bomu halafu mpuuzi kama wewe unakuja na ushauri wa kipuuzi kwamba 'watumie mbinu nyingine katika kufanya siasa".

Kwa taarifa yako waliokufa Arusha wengine hawakuwa kweny mkutano wa siasa bali walikuwa wanafanya shughuli zingine. Vile vile historia inaonyesha kuwa mara nyingi serikali inayotaka kubaki madarakani kwa nguvu huwaua raia wake ikiwaita magaidi, wahaini nk. Vile vile serikali ya namna hiyo haichoki kuwatesa viongozi wa vyama vya upinzani. Jifunza historia wala usihangaike kubuni vitu vipya.

Nadhani akili yako haiko sawa itakuwa imepinda kidogo,sasa hapo umeandika nini,maneno mengi halafu hewa!!
 
Hapo kwenye RED unamaanisha nini CDM inafanya siasa kwa kuitisha mikutano na mikutano hiyi ndo inavamiwa na Polisi na kushambuliwa kwa Risasi na Mabomu sasa wewe ulitaka wafanyeje au ulitaka wawe wanalihutubia Taifa kupitia TV kama anavyofanya Rais kila mwisho wa mwezi?

Hilo swali kawaulize wenye akili zilizoko kwenye kichwa kama chako!!!!
 
Kwanza nenda shule ukajifunze kuandika jambo na kulipa shape ya kueleweka kwa wasomi na waelewa,nashukuru umesema una uelewa mdogo,lakini ndani ya CHADEMA kuna waelewa wengi tena chuo kikuu,jitahidi wakati mwingine waone wakusaidie ku-shape stori yako then leta humu.Humu kuna Great Thinkers kibao sasa unapokuja na uelewa wako mdogo unazidi kujiaibisha pamoja na kwamba una jambo muhimu!

La pili sikiliza wewe Dogo mwenye uelewa Mdogo,hakuna ubishi kwamba Chadema inakubalika Arusha,na hakuna Ubishi kwamba Chadema haiongozi Arusha,hilo liko wazi na kwa watu wenye akili kubwa na uelewa kama sisi tunalitambua hilo,isipokuwa tatizo ni kwamba hakuna amani Arusha.

Kwa maelezo yangu hapo juu na kwa nguvu iliyonayo CHADEMA mjini Arusha nilitegemea sana kupata matokeo chanya na viongozi wake walipaswa kutumia mwanya huo kuliweka jiji la Arusha katika ramani nzuri kwa sababu kuna faida nyingi kwenye jiji hilo na moja kubwa ni kwamba ni jiji linaloingilika sana na wageni kutoka nje ya nchi,sasa wangetumia kuweka kila kitu sawa ikiwa ni pamoja na siasa zake zinazoongozwa na Chadema ili wageni wapate la kusema.


Kibaya sana na kinachonishangaza ni kiwamba kila vurugu na mauaji ya watu ni lazima zitokee kwenye mkutano wa chadema,ok.yawezekana ni wapinzani wao CCM ndio wanaowafanyia hivyo ili waonekane wana vurugu,lakini kwa sababu kuna watu wengi ndani ya Chadema ni Great Thinker walipaswa kubadili mbinu na kutumia mbinu nyingine katika kufanya siasa zao.

Leo hii hata wageni wanaobahatika kuingia Arusha na kushuhudia matukio hayo,wanaondoka na sura kwamba Chadema ndio wakiorofi.nasema sipendi,sipendi sipendi kabisa.

Nawe tumia miguu pia
 
Back
Top Bottom