Upuuzi Mwingine wa Muungano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Upuuzi Mwingine wa Muungano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Intellect, Apr 4, 2012.

 1. Intellect

  Intellect Member

  #1
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  ​Moja kati ya kero ambazo zimeutia dosari kubwa Muungano wa Jamuhuri ya Tanzania ni juu ya Mamlaka ya Mapato TRA.

  Leo hii tumeshuhudia kamata kamata ya daladala na gari zote za biashara kwa kodi ya TRA, ambayo ni laki unusu kwa mwaka, sasa wiki hii ambayo ndio ilikuwa deadline ya kulipa kodi hiyo tangu january 2012 imesababisha kero kubwa kwa wakazi wa mkoa wa Mjini Magharibi kwa kukosekana kwa usafiri wa daladala barabarani. Wamiliki hawajalipa kodi hiyo ya TRA, kwa madai kwamba kodi zishakuwa nyingi, ZRB, insurance, Road license na sasa TRA utadhani gari ni mpya na atakayelipa baada ya tarehe 1 april atatakiwa kulipa faini ya 30,000/-Tsh

  Hiki kimekua kilio cha muda mrefu na hapaonekani kuwepo jitihada mahususi ya kuondokana na kero hii hivyo wazanzibari wanaona ni bora Muungano uvunjwe ili kodi hii iondoke sambamba na kero nyingine nyingi!
   
 2. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Ungetumia akili yako kidogo tu kufikiri ungejua kulipa kodi ni muhimu kwa ustawi wa nchi yo yote. Lakini kwa kuwa umetumia viungo visivyo sahihi kwa kufikiri unadhani kuwa hiyo ni kero ya muungano!
   
 3. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #3
  Apr 4, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,313
  Likes Received: 3,079
  Trophy Points: 280
  Yaani kweli kuna Wazanzibar kufikiri kwao ni kufupi sana, kama huyu mtoa thread hii. Sasa nimegundua yale mengi watu wanayosema ni kero za Muungano ni uppuzi usio na mbele wala nyuma. Yaani nyie mnajilinganisha na nchi kama Emirates na Saudi Arabia ambako hawatozi kodi ya vitu kama hivi na kuona kodi za TRA ni kero za Muungano? Nadhani si mbali tutasikia fine za traffic ni kero za Muungano. Mnataka msilipe kodi mnafikiri hao Wawakilishi wenu wanalipwa mawe? Barabara zenu zinajengwa na Bill Gates? Polisi wenu wanaowafanya muwe salama wanalipwa mchanga wa fukwe zenu?

  Mimi nadhani kero kubwa kuliko zote za Muungano ni kuungana na watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri kama wewe, ambao inaonekana mko wengi sana huko visiwani. Nyerere alisema mnakuwa kama mtoto mdogo anayekunyea halafu yeye ndie analia. Kweli nyie ni tofauti mno na generation ya Karume.
   
 4. k

  karafuu Member

  #4
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mie nadhani mtoa mada amesahau kidogo suala la ulipaji kodi kuwa ni la lazima,lakini tatizo la wazanzibar katika kodi ni kuilipia bidhaa moja zaidi ya mara moja(double payment)ni makosa kwa tathnia ya uhasibu na kamati nyingi za kutatua kero za muungano zimeshindwa kulipatia suala hili ufumbuzi wa uhakika na wa kueleweka.kiufupi wazanzibar wameshapima kila kitu na ni watu waliojaaliwa upeo wa juu,yupo Dr Salim A Salim na wengine akina Prof Abdrahman Babu.
   
 5. Intellect

  Intellect Member

  #5
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Si dhani kama ni vyema kutoa maneno ya dhihaka! Umuhimu wa kulipa kodi hakuna asiyeufahamu! Hoja hapa ni juu ya swla zima la "double taxation" kumbuka kuwa Zanzibar kuna mamlaka ya kodi pia sasa je itakua sahihi kama wafanya biashara wa bara nao watatakiwa kulipa TRA pamoja na ZRB?
   
 6. J

  JacksonMichael JF-Expert Member

  #6
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 339
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lipa kodi kwa maendeleo ya TAIFA: Ujumbe huu umeletwa kwa hisani ya watu wa DOLE
   
 7. k

  kkitabu Senior Member

  #7
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 122
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Walipe mbona sisi huku bara tunalipa kwani muungano ukivunjwa ndo hawatalipa
   
 8. A

  Ama Amaa Member

  #8
  Apr 4, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 75
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  natamani hivi visiwa visukumwe katikati ya bahari mbali kabisa na Tanganyika maana ni mzigo na kero tosha
   
 9. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #9
  Apr 4, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwani huu muungano faida zake ni zipi? Baada yakuzijua ndo tuangalia umuhimu wa kuwepo ama kutokuwepo
   
 10. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #10
  Apr 4, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,738
  Likes Received: 6,014
  Trophy Points: 280
  Leo Tanzania Daima limeripoti hivi:

  Kamati ya Utendaji ya Chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA) imemteua Hemed Moroco kuwa kocha Mkuu wa timu ya soka ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, ambayo itashiriki mashindano ya nchi zisizo wananachama wa FIFA (VIVA), itakayoanza kutimua vumbi Mei 29 nchini Kurdistan.

  Hiyo ni mara ya kwanza kwa Zanzibar kushiriki michuano hiyo hivyo itakuwa imeandika historia mpya hapa nchini.

  Ikumbukwe, ZFA imekuwa na kilio cha muda mrefu kutaka uanachama wa FIFA lakini imekuwa ikikumbwa na vikwazo kadhaa vya KISIASA ikiwamo Zanzibar KUTOTAMBULIWA KAMA NCHI KATIKA SHIRIKISHO HILO.


  ...


  MY TAKE:

  Sijui ni kwani wazanzibari wanapenda kulalamika kila mara. Hivi hiyo kodi inayolalamikiwa inatozwa Zanzibar peke yake na kuacha upande wa pili wa Muungano? Hiyo TRA inafanya kazi visiwani peke yake? Kama ni wingi wa kodi uko pia huku bara na njia bora za kumalizana na "kero" hiyo ni kupitia mamlaka zinazohusika hasa Baraza la Wawakilishi; kama iliwezekana Katiba Mpya na hatimaye Serikali ya Umoja wa Kitaifa, hili linashindikanaje?

  Ndugu zetu wazanzibari, mtake msitake, kama ilivyoshindikana kujiunga na FIFA hatimaye mkatimkia VIVA, kwa kuwa Zanzibar sio nchi bali sehemu ya JMT na chombo kikuu cha ukusanyaji wa kodi ni TRA, mnapaswa kuitii mamlaka hiyo halali iliyowekwa na wananchi. Kukimbiakimbia au kuingiza siasa ilhali ni suala la utendaji na utekelazaji wa sheria haisaidii kwa sasa. La msingi, fuateni taratibu kupitia mamlaka zilizowekwa kisheria kupata ufumbuzi kama kweli ni kero.

  Hata hivyo kwa ushauri tu, msidhani mkijiondoa kwenye Muungano ndio hamtalipa kodi. Huenda hali ikawa mbaya mara dufu labda mkikubali kuuza uhuru wenu na kuwa koloni.
   
 11. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #11
  Apr 4, 2012
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Lazima kwanza tuwe na taarifa sahihi juu ya kile kilichotokea Zanzibar ili tuweze kutoa maoni kwa usahihi, maana ukiangalia mwanzisha thread jinsi alivyochanganya mambo, unaweza kuingia mkenge bure. Kodi ziko za aina mbali mbali, na kodi ya TRA ni kodi ya Muungano.

  Hata magari ya ZnZ yaliyokuwa yakija huku, ilikuwa yanalipishwa kodi ya muungano (Import duty ambayo yakiwa Zanzibar huwa haitozwi) na wala si double taxation.

  Na ukiangalia kwa makini, ndiyo maana inaonekana ni kero ambayo haijatatuliwa, lakini inawezekana hata mamlaka, ikiwamo ya Kero za Muungano, zimegundua haiwezekani kufuta kodi, kwani kufanya hivyo ni kufuta maendeleo ya Taifa. Pengine tu, watu hawaambiwi ukweli baadhi ya mambo ambayo inabidi wafahamu na kutilia maanani.
   
 12. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #12
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Nakushauri ure-phrase hoja yako ili upate michango mizuri lakini kwa namna ilivyo unaonekana mpuuzi!
   
 13. k

  karafuu Member

  #13
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ujumbe
   
 14. k

  kicha JF-Expert Member

  #14
  Apr 4, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 499
  Likes Received: 518
  Trophy Points: 180
  pasipo usawa na haki kamwe hakuna ataekaa kimya bila kulalama, kutwa humu watu wanalia na kulalamika magamba hivi magamba vile na sbb kuu wanaona wazi kua haki inapindishwa na wenye nguvu, sasa iweje mzenji akilalamika kuhusu jambo la wazi inakua nongwa? sikatai na kulipia kodi lkn je mbona zimekua nyingi na bila utaratibu? nahofia kuongezwa nyengine for afrca dvpt wakikaa kimya
   
 15. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #15
  Apr 4, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Mimi bado ninailaumu Serikali ya CCM. Kuna Wizara ya Muungano, pia kuna kamati ya kushughulikia kile kilicho batizwa jina la KERO ZA MUUNGANO.

  Lakini ukiuliza Wizara ya Muungano kero za Muungano ni zipi HAWAZIJUI. Mimi ninawapa CHALLANGE Wizara ya Muungano kwanza waainishe KERO ZA MUUNGANO ni zipi, ili tufahamu 1,2,3,4,5,6,7................. ndiyo kero za Muungano. Halafu Wizara ya Muungano iandae ROAD MAP ya kutatua hizo kero za Muungano.

  Lakini kwakuwa wizara ipo kisiasa ndiyo maana unaona kila tatizo lionatokea ZNZ Wazanzibari wanaita KERO ZA MUUNGANO. Mafuriko yakitokea Kero ya muungano, MV Spice Island ikizima KERO za Muungano, Taifa Stars Selection kero ya Muungano, Kulipa kodi TRA kero ya Muungano, NECTA kuawafutia matokeo wanafunzi waliofanya udanganyifu kero ya Muungano, JMT kuomba UN kuongezewa EEZ kero ya muungano, Rais wa SMZ kuhudhuria baraza la mawazuiri wa SMT kero ya Muungano, Mahakama kuzuia Hamad Rashid kuvuliwa ubunge na CUF kero ya muungano!

  Ninashauri wizara ya Muungano, Mh. Samia Suluhu aturodheshea kwanza kero za Muungano ili tuzifahamu. kwasababu kujua tatizo ni one step towards solution, halafu tukishafahamu hizo kero za Muungano tuna draft ROAD MAP ya kuzitatua. Wazanzibari acheni kulalamika wabaneni WAWAKILISHI wenu.
   
 16. Intellect

  Intellect Member

  #16
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kama tunasema Zanzibar ni mzigo kwa mungano, kwa nini tuendelee kuung'ang'nia? Wazanzibari waachwe wawe huru hatakama ni kupata tabu zaidi wapate wakiwa huru! Mbona South Sudan Imechwa huru, ugumu kwa Zanaibar unatokea wapi?
   
 17. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #17
  Apr 4, 2012
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Hilo la TRA linatukera hata sisi wa BARA. Hii mamlaka ivunjwe na kodi zikusanywe na halmashauri kwa maendeleo ya halmashauri
   
 18. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #18
  Apr 4, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Bara kuna serikali moja tu, huko Zenji zipo mbili, na ni lazima zilipiwe kodi. Poleni sana ndugu zangu. Hiyo kodi mwisho wake ni Nungwi.
   
 19. c

  chilubi JF-Expert Member

  #19
  Apr 4, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 3,027
  Likes Received: 1,016
  Trophy Points: 280
  Hivi izo kodi zinazokusanywa faida zake ni zipi? Labda kuwalipa viongozi, lkn barabara zinajengwa kwa misaada ya USA, maji, afya ni misaada kutoka nje, kodi ya TRA NA ZRB ZOTE HAZISAIDII WANANCHI!

  Btw kuna jamaa ameuliza maswali kama kodi haikusanywi wabunge watalipwa fukwe? Sijui marais watalipwa karafuu? Etc, yani amejidhihirisha kama ivo vitu alivovitaja vinamuumiza roho akiona zanzibar inavyo! :D

  Afu mi nashangaa, Nyerere alisema kuwa angekuwa na uwezo angevisukuma visiwa hivi, lakini kwanini bado ameshikilia kuviunganisha? Kwanini bado serikali ya muungano inashikilia znz iwepo katika muungano?
  Maendeleo ya nchi hayaletwi kwa kodi za dhulma kama wengine wanavofikiri, kuna njia nyingi tu za kuimarisha zanzibar! BANDARI HURU inatosha visiwani, na NDIO tunaweza kuwa kama Dubai na tanganyika kuwa kama UGANDA ENZI ZA VITA VYQ UBAGUZI! hebu tanganyika tafuteni uhuru na zenji watafute uhuru kisha mutizame nani ataendelea zaidi!
  Rasilimali nyingi zipo tanganyika lakini maendeleo hayaendani na mapato!!

  IDARA ZA KODI ZOTE ZIVUNJWE! ZIMEKUWA!
  Na labda hamujui kwanini wazenji tunalalamikia iyo kodi ya TRA, ni kwasababu tayari tunalipa ZRB, tunalipa kodi katika bodi 2, TRA na ZRB je huoni km iyo kero?
   
 20. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #20
  Apr 4, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 548
  Trophy Points: 280
  Masikini Muungano. nashindwa kuelewa kwa nini wakati bara tunalamika tatizo ni CCM, Pemba wanalalamika tatizo ni Muungano? kama matatizo yetu ni yale yale kwa nini tunalalamikia vitu viwili tofauti? au sisi tunaolalamikia CCM tuko wrong? au ni tabia ya ulalamishi tu?
   
Loading...