Upuuzeni uzushi kuwa ndege ya Tanzania inauzwa nchini Kenya

Korosho zishanunuliwa? Nasubiri kisado changu nibangue. Hizi ndege mpya mbili hata pesa malipo hayajakamilika, labda tumeshindwa kumalizia malipo. Kama unabisha, subiri uone report za CAG na budget inayokuja kuhusu pesa za kulipia ndege

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumekuwepo na uzushi kuwa Ndege ya Tanzania(Airbus) inauzwa nchini Kenya kwa sababu eti Tanzania imekosa kibali cha ndege zake kuruka katika anga za nje.

Huo ni uzushi Wa kiwango cha Juu.

Ukweli ni huu:

Kampuni iiyotengeneza ndege hiyo iliingia Mkataba na Tanzania kuwa kwa vile aina hiyo ya Ndege ni ya kwanza katika ukanda Wa Afrika, Kampuni hiyo ilikubaliana na Tanzania kuwa itakuwa inaikodisha Ndege hiyo kwenda nchi zingine , lengo likiwa ni kutangaza soko lake katika nchi hizo na hicho ndicho kilichofanyika kwa Kenya.
Hivyo basi, tuzipuuze taarifa hizo zenye nia ovu kwa nchi yetu.


Acha kudanganya watanzania, hakuna kitu km hichi duniani... yeyote anaetaka ndege kununua anakwenda kwa mtengenezaji..period... hili la kuwaambia watu eti mtengenezaji ana makubaliano na mteja juu ya ukodishaji ni UONGO mkubwa.... suala la kukodisha ni la mteja pekeee, hakuna wa kuingilia... kukodisha ndege ni jambo la kawaida, hata mwanzo ATC ilikua na ndege imekodisha km utakumbuka... kwa hyo kama na sisi tumeamua kukodisha tuseme tu ukweli lkn usiseme uongo kutuaminisha unajua sana.. Tondo loveto..Shito Nange
 
Yaani ndege yetu tumeinunua wenyewe na bado kampuni watake tuwe tunaikodisha kwenye nchi zingine ili kuitangaza?
Kwa nini kampuni wasingetengeneza ndege kama hizo na kuzikodisha huko wanakotaka zitangazike?

CC Zero IQ
Swali la msingi sana hilo, na je ikikodiwa itapakwa rangi na chata ya KQ? Hahahaha hatuna chetu hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ufafanuzi mzuri, umewakata vilimi, vizabinazabina
Mie naona kizabanazabina ni wewe, maaana hata huyo aliyeleta hicho alichoita ukweli wenyewe wala siyo msemaji wa shirika (ATCL) wala wizara husika! Jamani, kujipendekeza huku hadi lini?
 
Ndege yetu inayofanyiwa mchakato kukodiwa na wakenya kwa ajili ya maonesho ya airbus,
Imeamuliwa hivo na wakenya kuliko kukodi za mbali na zenye gharama kubwa ikabidi watujie sisi
Hivi wanaodanganya mnapataga faida gani?
Unadanganya ili iweje?
Unalipwa na nani kusambaza uongo kama huo?
Ni kwa Maslahi ya nani?

Siyo hii tu, kuna hamasa kubwa au nguvu kubwa ya ushawishi kusambaza uzushi,

Britannica
 
Naambiwa hao ndio ma superstars wenu, huwa siwafatilii, lakini maadam mmeleta uzi ngoja tuseme kidogo.
Huo ufafanuzi ili kutufanya tupuuze uzushi, ni upuuzi,ujinga na utoto kabisa. Kuna watu wanakua miili lakini akili ni za watoto wa darasa la pili B. Eti shirika linalotengeneza ndege za Boeing Airbus! Yaani jitu jinga jinga tu halijui kuwa Boeing na Airbus ni makampuni mawili tofauti, moja liko Ulaya jingine Marekani! Maelezo yaliyobakia ni upuuzi mkubwa zaidi.
 
Na hilo nalo unashangaa? Ukiwa fundi Seremala ndiyo huwezi kukodisha kiti jirani? Watu wengine bwana, mnaaibisha jinsi mnavyofikiri kwa kutumia
Ndo uchukue kiti cha mteja wako ambacho kashakilipia ukamkodishie mtu wa Malinyi eti unatangaza biashara yako jinsi ulivyo seremala maridadi na mahiri?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom