Upungufu wa msamiati au ni uvivu tu?

VanDon

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
370
645
Hivi ilikuwaje kwenye lugha ya kiswahili mpaka mke wa kaka akaitwa "shemeji" kwa ndugu wote wa mume yaani wakiume, na wa kike wanamwita "wifi". Ila mume wa dada akaitwa "shemeji" na jinsia zote mbili!?!

Inamaana walikosa kabisa jina lingine? πŸ€”
 
Bora sisi, wazungu neno uncle linahusisha ndugu wakiume wa familia. Yaan baba mdogo, mjomba, baba mkubwa, binamu wa baba au mama na marafiki wakiume wa wazazi.
 
Hao Sasa wana uzembe wa kiwango cha lami.

Uvivu tu wa kuongea!
 
Kwa Kiswahili fasaha cha Pwani, neno MWAMU hutumika kumuita mume wa dada. Naye anakuita hivyo hivyo kaka wa mke wake. Hii inaepusha kumuita shemeji mwanaume mwenzako. Msamiati huu hutumika sana mikoa ya Pwani, Tanga baadhi ya maeneo, Lindi, Mtwara na Ruvuma hasa wilaya ya Tunduru.
 
Ikiwezekana msamiati huu utumike nchi nzima. Hii mambo ya kuitana shemeji wanaume ni kama haijakaa sawa hivi.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Kwa Kiswahili fasaha cha Pwani, neno MWAMU hutumika kumuita mume wa dada. Naye anakuita hivyo hivyo kaka wa mke wake. Hii inaepusha kumuita shemeji mwanaume mwenzako. Msamiati huu hutumika sana mikoa ya Pwani, Tanga baadhi ya maeneo, Lindi, Mtwara na Ruvuma hasa wilaya ya Tunduru.
Uko sawa, neno hili nililijua miaka ya 80 ila nilidhani ni Kisambaa. Bibi yangu aliniuliza yuko wapi 'muamuo', ila maneno yote alitamka kwa Kisambaa.

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom