Upungufu wa kinga za kiroho

Upungufu wa kinga za kiroho

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,210
Reaction score
829,203
Wengi tunapoongelea neno KINGA tunapeleka mawazo yetu moja kwa moja kwenye mipira ya kufanyia ngono yaani kondomu. Lakini wengine watadhani ni kinga dhidi ya maradhi ama kinga dhidi ya ajali barabarani na wezi majumbani huku wachache wakiwaza kinga dhidi ya watoto nknk. Akitokea mmoja akazungumzia kinga ya kiroho huyo itabidi umwangalie mara mbili kwakuwa si kawaida na si mazoea.

Tumekuzwa kwenye kuulinda mwili, kulinda vile vinavyoonekana, tunauhudumia mwili wa nyama uwe na siha njema, sura ivutie, nywele zivutie, nguo zikubali, tunaunywesha na kuulisha mwili wa nyama uharibikao na kusahau kabisa msingi wa kinachoufanya huo mwili uhudumiao uuhudumie.

Mwili dhaifu usio na kinga imara ni rahisi sana kushambuliwa na magonjwa mbalimbali, kuna watu haipiti mwezi kaugua hiki ama kile. Hawa automatically miili yao haina kinga thabiti. Ni watu wa spana mkononi kama gari bovu trip moja kazini, trip moja kwa fundi
Sasa mwili huohuo unaoweza kuwa na afya na siha njema usioshambuliwa na magonjwa ya mara kwa mara unaweza kuwa na upungufu mkubwa wa kinga za kiroho.

Pigo lolote likirushwa humpata yeye kama sio jini makhaba, basi ni zongo, kama sio zongo basi ni mapepo, kama sio mapepo basi ni chochote kibaya cha roho chafu kitampata.

Mtu mwenye upungufu wa kinga za kiroho mambo yake hayaendi kwenye stark, hayanyooki, hayasimami sawasawa, kama ni ajira inakuwa ngumu kupata, na akiipata hachelewi kuacha kuharibu ama kufukuzwa.. Kama ni biashara nuksi tupu, kama ni mahusiano balaa tupu, hakuna atakaloshika likakaa sawa.

Kuna vitu husababisha upungufu wa kinga za kiroho. Mungu (kwa wale waamini na waaminio) huleta duniani kiumbe kamili chenye kinga zote(usichanganye na wale watoto wa kichawi na majini) Lakini katikati ya harakati za maisha watu hupoteza ama kupunguza kinga zao kwa kwenda kwa waganga wa kienyeji, kuhangaika bila kuwa na msimamo wa kiimani, kufanyiwa mambo mabaya ma jirani ndugu ama rafiki.

Habari za kusafishwa nyota ama kupewa Pete za bahati ni vitu vibaya kabisa kiroho.

Habari za kuhangaika kwa waganga wa kienyeji ni kuzidi kujichafua kiroho na kujiharibia kabisa.. Yani mwili wako unakuwa kama punching bag, kila mtu anajaribu hapo.

Kutangatanga kiimani, mara huku mara kule unahangaisha bure roho yako na kuichosha sana mwisho inakuwa dhaifu kabisa
Jijengee msingi imara wa kinga ya kiroho kwa kubaki na imani moja bila kujali unaamini katika nini.

Pambana na hali yako kwa njia chanya. Kila mmoja wetu ana changamoto nyingi sana za maisha. Epuka nguvu hasi yoyote kwa manufaa binafsi. Unajiharibia.

Epuka epuka epuka kujihusisha na mambo ya giza huko huendi kutengeneza bali kujimaliza. Unafuu wake ni wa muda mfupi sana.
Wengi wanaohagaika leo wenye upungufu wa kinga za kiroho angalia historia zao wengi wamepitia hayo hapo juu. Simama na Mungu wako ujenge kinga imara ya kiroho.
 
Mshana Jr on ktk ubora wake
the-immune-system.jpg

Tunatumia damu kurekebisha mambo yetu yakae sawa. Lakini wakati huohuo damu hiyo ni kitu hai, damu ina roho na unaichukua baada ya kuteketeza roho isiyo na hatia. Huku ni kujiingiza kwenye maagano mabaya zaidi na vita ya kiroho amabayo mwisho wake huiacha roho yako ikiwa taabani kwa kipigo na kuondolewa kinga zake zote.... Vita huleta udhaifu
 
Umenena vyema mkuu,hasa hapo kwenye kuhangaika kiimani, yakati hizi za mlipuko wa manabii, watu kila siku ni kukimbia huku na huko kuwafata bila kuzingatia si wote ni wa Mungu wa Nuruni. Unawekewa mikono na kila anayejiita nabii,bila kujua unazidi kuwa dhaifu na kupoteza kabisa Kinga ya kiroho, hata ile ndogo uliyokuwa nayo.
 
Umenena vyema mkuu,hasa hapo kwenye kuhangaika kiimani,nyakati hizi za mlipuko wa manabii,watu kila siku ni kukimbia huku na huko kuwafata bila kuzingatia si wote ni wa Mungu wa Nuruni.unawekewa mikono na kila anayejiita nabii,bila kujua unazidi kuwa dhaifu na kupoteza kabisa Kinga ya kiroho,hata ile ndogo uliyokuwa nayo.
Huku unawekewa mkono wenye unabii bandia, mkono wenye nguvu za kichawi, mkono wa kuzimu unachukua kinga yako halisi na kukuachia bandia
Unaenda kule unapewa kitambaa chenye upako feki unakitumia huku tayari una nguvu ile nyingine
Mara unaenda kupewa kichupa cha maji ya baraka, mara maombezi ya usiku kucha, unaichosha roho yako kwa kukaribisha wageni wane tofauti ambao kila mmoja anataka kukumiliki kiroho
 
Huku unawekewa mkono wenye unabii bandia, mkono wenye nguvu za kichawi, mkono wa kuzimu unachukua kinga yako halisi na kukuachia bandia
Unaenda kule unapewa kitambaa chenye upako feki unakitumia huku tayari una nguvu ile nyingine
Mara unaenda kupewa kichupa cha maji ya baraka, mara maombezi ya usiku kucha, unaichosha roho yako kwa kukaribisha wageni wane tofauti ambao kila mmoja anataka kukumiliki kiroho
Pamoja na kukuondolea kinga ya kiroho,wanakuacha maskini pia,maana vyote hivyo,maji,mafuta,chumvi,kitambaa,hawapewi bure inabidi ununue.wanaita kupanda mbegu.
 
Ubarikiwe mtumishi umenena vyema

Bwana mtoa mada naona hii hali ya kutoa uzi mida mibovu unawafanya watu wanacomment huku wanausingizi hivi kweli leo hii wewe wakuitwa mtumishi wa Bwana?? Inamaana tunguli huna tena?? Anyway ngoja nivute shuka nlale
Heri wao waliofunuliwa na kuiona ile kweli kwakuwa hawakutazama tu bali wameona pia, hawakusikia tu bali wameelewa pia usihukumu usije ukahukumiwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom