Upungufu wa damu (Anemia) wakati wa ujauzito

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Upungufu wa damu (Anemia) wakati wa ujauzito ni tatizo linalo wapata wanawake wengi.

Tatizo hili huwaongezea hali ya kujisikia uchovu, kupauka kwa rangi ya ngozi, maumivu ya kichwa pamoja na kuongezeka kwa mapigo ya moyo. Aidha, huongeza nafasi ya kujifungua mtoto mwenye uzito mdogo, kujifungua kabla ya wakati pamoja na kufariki kwa watoto wakiwa bado wapo tumboni.

Kukosekana kwa kiasi cha kutosha cha madini ya chuma mwilini pamoja na upungufu wa virutubisho vya folic acids ndiyo sababu kuu mbili zinazofanya changamoto ya upungufu wa damu iweze kutokea.

Ili kukabiliana na hali hii, mwanamke mjamzito hushauriwa kutumia vidonge vyenye madini ya chuma (ferrous sulfate) pamoja na folic acids kila siku tangu pale anapo jigundua kuwa ni mjamzito.

Kwa kuwa dawa zenye madini ya chuma zinaweza kusababisha kuvurugika kwa tumbo, kiungulia pamoja na kichefuchefu, inashauriwa zisimezwe pamoja na kahawa au chai, pia mhusika anapaswa kuwa amekula kwanza chakula.

Chanzo: Wizara ya Afya (STG NEMLIT 2021)
 
Athari za Upungufu huu wa damu kwa mwanamke kipindi Cha kawaida (kipindi tofauti na ujauzito) ni zipi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom