Upotoshaji wa tangazo la 'Policy Forum' kuhusu kodi...

Upotoshaji wa tangazo la 'Policy Forum' kuhusu kodi...

mbeyaman

Member
Joined
Sep 28, 2013
Posts
97
Reaction score
28
Hili tangazo linalohoji matumizi ya makusanyo ya kodi ya serikali ni upotoshaji wa hali ya juu.

Tangazo hili limekuwa likioneshwa katika vituo mbalimbali vya televisheni. Kibaya zaidi tangazo hili linachochea uasi wa wananchi kutolipa kodi kwa serikali yao.

Hivi TCRA kwa nini wasizue tangazo hili la upotoshaji? Katika tangazo hili inasikika sauti inayohoji kodi zinazokusanywa zinaenda wapi wakati jibu lake liko wazi kwani huduma mbalimbali za jamii zinazotolewa na serikali ni kazi mojawapo ya matumizi ya kodi hizi. Halikadhalika maendeleo makubwa yaliyopatikana katika nchi yetu ni matumizi mazuri ya kodi hizi.

Hivi ina maana hawa walioandaa tangazo hili hawaoni jinsi miundo mbinu ilivyoboreshwa? Ina maana haoni ujenzi wa barabara kila kona ya nchi kutokana na kodi hizi? ...hawaoni uboreshaji wa huduma za afya na elimu katika halmashauri mbalimbali?.
 
Mleta mada kala YAMINI na Serikali iloyopo madarakani jamani hivi kama huoni hata basi kusikia pia ni tabu. Tangazo liko vema linaloongelewa halihitaji mbwembwe kulijua.

Punguza jazba lisikilize/tazama vizuri tangazo ninahakika utalielewa. Kama unakula mboga saba huwezi jua nchi hii ina shida sana.

Tembea ujionee mwenyewe usingoje usimuliwe.
 
Kwa hiyo mwananchi akitaka kuhoji matumizi ya kodi yake atumie utaratibu gani we punga?
 
Kama hujui kusoma hata picha huzioni??? Ni kitu gani sasa hibi Tanzania huchangii?? Kodi ni kwa ajili ya safari za Rais na kuhonga wapinzani wauwe vyama pinzani. Muulize Chemba alimvutia Zittoccm ngapi kuisambaratisha Chadema? Pia muulize Wasira wanamlipa ngapi Msando kufungua kesi ya kuhisi mahakama kuu?? Yaani shida kweli kweli, dalali wa viwanja anafungua kesi ya kuhisi Zittoccm atavuliwa uanachama wa Cdm.
 
Lile tangazo bomba sana!


Linasema ukweli mtupu

Ushahidi ni wao kutibiwa nje,watoto kukaa chini,kero za maji n.k.

Au wewe unaishi ulaya?!

Acha kutetea watawala,tetea mlalahoi anaekula mlo mmoja kwa siku.

Ukifanya hivyo, hata mbinguni utaingia.
 
Mtu mzima hovyo ..tangazo linahoji kwa nini kampuni kubwa zinasamehewa kodi wakati mwananchi wa kawaida kila kitu analipa kodi bila kupewa msamaha.

Umekurupuka ebu fatilia uoni Kampun kubwa zinavyosamehewa kodi.

Wewe kabla ujaanza biashara unaambiwa ulipie kodi wakat kampuni zinapewa miaka 5 bure.

Mfano uko Mererani makampuni ya madini hayajawai kulipa kodi
 
Unataka matangazo ya Kidumu Chama cha Mapinduzi? Tena inabidi NGO na CSO's ziige mfano wa Policy Forum watuelimishe ili Mafisadi watorokee USWISS wakatumie hizo ambazo wameshaficha.
 
Hivi ni kwa nini magamba wanawalazimisha watu kuona vitu wasivyoviona? Kuwaaminisha watu vitu wasivyoamini? eti 'maendeleo'...Maendeleo gani ambayo watu hawayaoni mpaka uwalazimishe kufungua macho waone?

Nafikiri magamba na mleta thread wanatakiwa kuwa 'wazee wa kiroho', maana huko ndiko tunapoaminishwa tusivyoviona..
 
Sio upotoshaji ila ni haki ya mwananchi kujua haki yake maana ukusanyaji kodi umeboreshwa kwa teknolojia ya hali ya juu (efd machine) lakini udhibiti wa matumizi bado upo analogia badala ya digitali na isitoshe huoni kila siku bungeni watu wanahoji tamisemi kwa ubadhirifu na huoni viongozi wa serikali wanavyofaidika na kodi zetu. Nadhani muda sio mrefu wananchi wataanza kuhoji uhalali wa serikali iliyo madarakani.
 
Naogopa Ban ya kudumu,sichangii ila jua nimekupa matusi ya nguoni(ulivyofunika na nguo nimevitaja)
 
Hahahaaaaa yaaani anaepingA lile Tangazo atakua na upungufu WA akili. Invisible Kuna thread ilikuwepo tayari, Naomba ziunganishwe
 
Last edited by a moderator:
Tangazo lipo sahihi
Lahimiza latusihi
usiku na asubuhi
Tujadili kodi zetu

Tuhoji zinapokwenda
kwani maisha yapanda
maisha yanatushinda
Gharama zaota mbawa

Wenyewe wanajigamba
tena nyimbo wanaimba
Eti kodi zina tamba
Miundo mbinu zajenga

Umeme bei ya ghali
Gesi nayo siyo mali
Mkaa watoka mbali
Wananchi tuko hoi

Kila kukicha kilio
wananchi twenda mbio
Tukisikia mlio
Twajua mambo tayari

Tukamlilie nani
Kwa mapambio tughani
haya ni maisha gani
Mbona hayana thamani

viongozi wamelala
vyao viko kwenye ghala
sie tuko kwa msala
machozi jasho na damu

Wakilifuta tangazo
wakaliweka vikwazo
tutajua hamnazo
Limewafika shingoni

kuna siku itafika
sote si tutaamka
itakuwa patashika
Ndipo mtapoelewa

Mnatufanya mazuzu
kutugeuza kauzu
pale tutakapofuzu
hakika tutawanyosha

Mundu nimeghazibika
Najua nimesikika
litapozuka gharika
Msishangae wakubwa!!
 
toa mawazo yako ulitaka asemeje kwa lugha nyingine..?
 
Nimeliona Tangazo lile mara kadhaa hata mimi pia naona ni la kichochezi. Limekaa jana kwamba kodi za wananchi hazifanyi chochote. Yaani as if hakuna maendeleo na pia as if misamaha ya kodi inatolewa hovyo.

Hata hivyo natamani nishuhudie chadema ikiingia madarakani halafu wananchi waone jinsi itakavyoshindwa kuleta marndeleo na jinsi maisha yatakavyokuwa magumu.

Ni rahisi kucheza mpira ukiwa nje. Ila ukiingia ulingoni ndo utajua.
 
Mtu mzima hovyo ..tangazo linahoji kwa nini kampuni kubwa zinasamehewa kodi wakati mwananchi wa kawaida kila kitu analipa kodi bila kupewa msamaha.

Umekurupuka ebu fatilia uoni Kampun kubwa zinavyosamehewa kodi.

Wewe kabla ujaanza biashara unaambiwa ulipie kodi wakat kampuni zinapewa miaka 5 bure.

Mfano uko Mererani makampuni ya madini hayajawai kulipa kodi
Nilitaka nimjibu hivyo hivyo!!huenda kalisikia tangazo usingizini.Inshu kwanini watu wasio jiweza wanalipa Kodi na makampuni makubwa yanasamehewa!serekali iliyopo ni kwa ajili ya kuwasaidia wananchi au kuwaumiza


Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Hahahaaaaa yaaani anaepingA lile Tangazo atakua na upungufu WA akili. Invisible Kuna thread ilikuwepo tayari, Naomba ziunganishwe

Mpwa kuna watu wanatafutia wenzao ban za bure tu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom