Hili tangazo linalohoji matumizi ya makusanyo ya kodi ya serikali ni upotoshaji wa hali ya juu.
Tangazo hili limekuwa likioneshwa katika vituo mbalimbali vya televisheni. Kibaya zaidi tangazo hili linachochea uasi wa wananchi kutolipa kodi kwa serikali yao.
mbona deni la taifa linaongezeka siku hadi siku, watumishi mbona hawalipwi mishahara kwa wakti na wengine hadiwatake kugoma
Hivi TCRA kwa nini wasizue tangazo hili la upotoshaji? Katika tangazo hili inasikika sauti inayohoji kodi zinazokusanywa zinaenda wapi wakati jibu lake liko wazi kwani huduma mbalimbali za jamii zinazotolewa na serikali ni kazi mojawapo ya matumizi ya kodi hizi. Halikadhalika maendeleo makubwa yaliyopatikana katika nchi yetu ni matumizi mazuri ya kodi hizi.
Hivi ina maana hawa walioandaa tangazo hili hawaoni jinsi miundo mbinu ilivyoboreshwa? Ina maana haoni ujenzi wa barabara kila kona ya nchi kutokana na kodi hizi? ...hawaoni uboreshaji wa huduma za afya na elimu katika halmashauri mbalimbali?.
Mods turuhusu tumtukane mtoa mada kwa robo saa tu.
Mbona mnaweweseka ?...mna maslah gani na NGO ya kichochezi ya Policy Forum?...hakika lile tangazo halitakii mema nchi yetu.Kodi ni lazima kila mwananchi kulipa.Mmejawa na hoja dhaifu ati kodi inatumika vibaya...na hiyo misamaha ya kodi ipo hata kwa wananchi wa hali ya chini.Mathalani mjasiriamali mwenye mtaji chini ya milion 5 hapaswi kulipa kodi.Vilevile hata mfanyakazi wa kima cha chini mshahara wake hauna kodi.Mbona hamuitakii mema nchi yetu?..hamna nchi isiyokusanya mapato duniani.Tuipende nchi yetu...mihemuko ya vyama vya kipinzani haitawapeleka popote.
Nimeliona Tangazo lile mara kadhaa hata mimi pia naona ni la kichochezi. Limekaa jana kwamba kodi za wananchi hazifanyi chochote. Yaani as if hakuna maendeleo na pia as if misamaha ya kodi inatolewa hovyo.
Hata hivyo natamani nishuhudie chadema ikiingia madarakani halafu wananchi waone jinsi itakavyoshindwa kuleta marndeleo na jinsi maisha yatakavyokuwa magumu.
Ni rahisi kucheza mpira ukiwa nje. Ila ukiingia ulingoni ndo utajua.