Upotoshaji wa Taarifa waongezeka kuelekea Uchaguzi nchini Ujerumani

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Wakati Ujerumani ikijiandaa na Uchaguzi wa Bunge unaotarajiwa kufanyika Septemba 26, ripoti mpya ya Taasisi isiyo ya Kiserikali nchini humo ya Avaaz imeonesha kuongezeka kwa matukio ya upotoshaji wa taarifa.

Ripoti ya Taasisi hiyo imemtaja mgombea wa Chama cha Green, Annalena Baerbock kuwa mhanga mkubwa zaidi wa upotoshaji huo wa taarifa, akiathiriwa na zaidi ya asilimia 70 ya matukio yote ya upotoshaji yaliyorekodiwa.

Matukio hayo ya upotoshaji yanatajwa kuwafikia watu wengi nchini Ujerumani, zaidi ya nusu ya wapiga kura wote nchini humo wakifikiwa angalau mara moja na taarifa za upotoshaji kuhusu Baerbock kupitia mtandao wa Facebook, kwa mujibu wa ripoti hiyo.

Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Christoph Schott ametaja sababu ya kiwango kikubwa cha taarifa za upotoshaji kumhusu mgombea huyo kuwa inaweza kutokana na misimamo yake ya kisera, au sababu za jinsia, kwa kuwa ni mwanamke.
“Lakini ni ngumu sana kupata ushahidi kuhusu sababu hizo,” alisema Schott.

Taifa hilo lenye nguvu kubwa zaidi ya kiuchumi Barani Ulaya linatarajiwa kufanya uchaguzi wa kumtafuta mrithi wa Kansela Angela Merkel hapo Septemba 26.

Changamoto ya uposhaji wa taarifa inatajwa kuathiri mwelekeo wa maoni ya umma nchini humo kabla ya kufikia tarehe ya uchaguzi. Ongezeko la matumizi ya intaneti na mitandao ya kijamii nchini Ujerumani linatajwa kuongeza athari za upotoshaji, ambapo zaidi ya 89% ya watu nchini humo wanatumia intaneti, huku zaidi ya watu milioni 66 wakitumia mitandao ya kijamii (sawa na 78.7 ya wakazi wote wa taifa hilo).

Chanzo: DW

1631000324823.png

Mgombea wa Chama cha Green, Annalena Baerbock
 
Back
Top Bottom