“Wakati huo pazia la hekalu likapasuka vipande viwili, toka juu hata chini. Dunia ikatikisika, miamba ikapasuka. Makaburi yakafunguka, na miili mingi ya watakatifu waliokuwa wamelala ilifufuka. Baada ya kufufuka kwake, walitoka makaburini wakaingia katika mji mtakatifu na kuonekana kwa watu wengi. Basi yule jemadari na wale waliokuwa pamoja naye wakimlinda Yesu, walipoona tetemeko la ardhi na mambo hayo yaliyotukia, waliogopa sana, wakasema, ‘Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu!’”* (Mathayo 27:51–54)
Mathayo, anayedhaniwa kuwa mfuasi wa Yesu, aliandika Injili yake karibu mwaka 85 baada ya Yrsu kutoweka na alinakili sehemu kubwa kutoka kwa Marko, mwanafunzi wa Petro, aliyeandika karibu miaka 65 BK. Inaelezwa kuwa Mathayo alitungia simulizi za maiti kufufuka na tetemeko la ardhi.
Tunawezaje kujua? Kwa sababu Yohana, ambaye alikuwa chini ya msalaba, hakutaja mambo hayo. Hakika, matukio ya ajabu kama hayo yangeelezwa na kila shahidi.
Kwa kuongezea, Mathayo alisahau kusema kama maiti wale walirudi makaburini. Pia, kwa mujibu wa Luka, jemadari alisema kitu tofauti: “Hakika mtu huyu alikuwa hana hatia.” (Luka 23:47)