Upotoshaji kuhusu mizimu

Mkuu, Asante kwa Uzi mzuri, nilikuwa nimetekwa na dini za wazungu, lakini baada ya kusoma shule ya kanisa tukifunzwa bible knowledge, nilishangazwa kuambiwa bibilia iliandikwa na wazee 70 lakini tuwapo kanisani utasikia bibilia iliandikwa na roho mtakatifu. Profesa wangu chuo kikuu, akamaliza kabisa kwa kusema dini zote ni uupuzi isipokuwa African Tradition Religion.

Ni kweli, kutukana mizimu yako ni kujitenga na mafanikio yako ya kweli kimaisha. Niliacha kuabudu Mungu wa mzungu na dini yake tangu wakati huo.
 
wafu hawajui lolote

Jifunze kuhusu dimensions au njia za ulimwengu zipo tisa hii ya ubinadamu ni ya tatu. Ukitoka hapa kuna zingine safari yako itaendelea labda kama you have no soul.
 
Jifunze kuhusu dimensions au njia za ulimwengu zipo tisa hii ya ubinadamu ni ya tatu. Ukitoka hapa kuna zingine safari yako itaendelea labda kama you have no soul.
there is only one true dimension
 
Jifunze kuhusu dimensions au njia za ulimwengu zipo tisa hii ya ubinadamu ni ya tatu. Ukitoka hapa kuna zingine safari yako itaendelea labda kama you have no soul.
ulichokiongea ni kweli kwa asilimia zote,
kuna kisa kimoja kiliwah kumtokea
kumtokea mama mkubwa wangu
mnamo mwaka 2008
yeye alikufa kwa mda,
kisha akafufuka na baada ya kufufuka alielezea yaliyomkuta pindi amekufa.

Yeye alifarik dodoma mjini,
na nyumban ni kijijini, hivo uliandaliwa utaratibu wa kusafilisha mwili wa marehemu hadi kufika nyumbn ni mwendo wa masaa mawili
walifika nyumban na mwili wa marehemu,
Walikaa masaa mawili
yule bi mkubwa akaamka watu waliokuwa hapo walishangaa sana na hata wengne kukimbia
yeye bi mkubwa akawaambia naomba maji ya kunywa maana nmechoka sana,
nmetembea kwa mda mlefu na nmetoka mbali sana,
basi wakampatia maji na kisha akawaeleza kisa alichokutana nacho,

nanukuu kama nilivyosikia kutoka kwake
anasema alikuwa anatembea kwa mda mlefu huko alikokuwa alikuwa akipita kwenye milima na mabonde bila kuelewa anaelekea wapi alitembea kwa mda mlefu mwisho alikuta kuna mlango mkubwa wa kuingia basi alibisha hodi na mlango ukafunguliwa
baada ya mlango kufunguliwa aliona ile sehemu ina mwanga mweupe na unaong'aa sana tofauti na wadunian
hakuna jua ila mwanga umetapakaa sehemu yote,
kifupi ni kama wana dunia yao tofaut na sisi,
alipoingia ndani alikutana na ndugu zake wa zamani waliokuwa wamekufa dunian akawakuta kule
anasema kuna watu wengi sana kule
hata hivyo anasema wale watu hawakumpokea maana walikuwa wameinamisha vichwa chini
yeye aliendelea mbele akakuta babu yake mzaa baba ake amekaa kwenye kiti na yule babu yake pia hakumtazama uso ila alikuwa kainamisha kichwa
alipofika yule babu yake akamuuliza
wewe nani?
akajitaja jina
akaulizwa umekuja kufanyaje,
akawaambia nmekuja kama nyinyi mlivyo kuja,

babu akamwambia umekuja kabla ya mda wako chukua haya maji unywe upate nguvu ugeuke uludi ulikotoka
mda wako wa kuja huku ulikuwa bdo haujafika bali kuna mtu alikuroga hivo sisi hatukupokei,
mda wako wa kuja ukifika tutakupokea,
baada ya hapo alianza kurudi alitembea umbali kidogo baada ya kuvuka mlango wa kule
ndo akastuka akiwa kitandani.
na akasimulia kama nilivowaelekeza hapo juu,

Tokea cku hyo nilijifunza mambo meng kupitia hii story ya kweli kabisa
kwamba kuna dunia baada ya kufa
na ukifa unaenda kuungana na ndugu zako waliokutangulia kabla
ambao sisi ndo tunawaita mizimu.
hata hivyo huyo mamkubwa ameshafariki kwa sasa.
lakin aliniachia somo kwamba nijitambue kuwa baada ya kufa kuna maisha,
na maisha yenyewe ni kuungana na ndugu zako waliokutangulia,
 

Hii ni kweli kabisa kitaalamu inaitwa Near Death Experience
 
Mkuu kwani Mungu wako mwenye uwezo wote, anaejua yote na alie mahali popote..YUKO WAPI MBONA SHETANI ANAZIDI KUTESA NA KUPOTEZA UMAARUFU WA MUNGU MWWNYEWE??

AU

Alikuwa wapi hadi Eva na Adam wanarubuniwa na shetani ili waasi?? mbona hakuzuia????

AU


Huyo Mungu wako yuko wapi mbona watu wake wanateseka na majanga, magonjwa na mabalaa mengine, MBONA HAZUII YASITOKEE??????????
 
Nakubali sana Mkuu hii ndio elimu tunatakiwa kupeana
 
Okay...hivo ndo umeelewa ww,lkn ukisoma Kitabu cha Matendo ya Watume utaelewa jinsi Injili ilivoenezwa kutoka Uyahudi kwenda Asia,Ulaya na maeneo mengine.Hao Rumi hawakuwa Wakristo hapo kwanza,walikuwa na miungu yao.
Ndio maana umeambiwa huyo alikua ni Mungu wa wa Israel wewe mswahili huku anakuhusu nini kwa nini Injili hiyo Isitokee ipogolo pale kuelekea huko Uyahudi?kama kweli alikua Mungu wetu
 
Hoja hujibiwa kwa majibu sio tena maswali mengine yasio na kichwa wala miguu!
 
MUNGU yuko mmoja tu juu mbinguni, na chini duniani.

miungu iko mingi sana hapa duniani chini ya mbingu na ndani ya nafsi zetu.

Je, wewe unaeabudu mizimu aliyekuumba ni nani? Na huyo aliyekuumba alikuumba kwa kusudi gani? Na alikupa maelekezo gani?
 
This is pervesion to the extreme,duh!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…