SoC01 Upotevu wa tamaduni zetu ni janga kuu tusilichukulie poa

Stories of Change - 2021 Competition
Jul 29, 2021
81
158
Ni kitu ambacho kisicho fichika ya kuwa utamaduni wetu zinaendelea kutoweka kadri siku zinavyozidi kwenda. Kutokana na taarifa zilizotolewa na UNESCO ni kwamba kila baada ya wiki zaidi ya lugha mia sita (600) hutoweka. Ukiangalia kwa sasa Ni watu wengi hatutumii wala hatujui tamaduni zetu.

Tumezichukulia kama Ni mambo ya kishamba na ya kizamani Sana. Zamani nilivyokuwa mdogo ilikuwa kwenye kila sherehe zetu, tulikuwa tukicheka ngoma za kinyumbani, za Saida Kalori, lakini siku hizi, hazipigwi sana. Na hata kwenye maharusi na sherehe zinaekwa tu nyimbo za kizungu.
Na kama huamini, jaribu kuuliza kijana yeyote au kundi la vijana kama wanajua au wanaweza kuongea lugha za kabila zao. Utakuta wengi hawajui. Mimi mwenyewe sijui kuongea lugha ya kabila langu, na hata ngoma za kikwetu nimeshazisahau. Hivi ndivyo mila na desturi zetu zinavyoendelea kupotea, na baada ya muda tutakuja tutajikuta hatuna hata kilicho Cha kwetu. Vizazi vyetu havitajua chimbuko lao wala lugha zao za asili,
Mwandishi wa gazeti la UNESCO amesema, “watoto wengi zaidi hawazungumzi lugha zao za asili, kwa hiyo uenezaji wa lugha kutoka kizazi kimoja hadi kizazi kingine inapotea, na matokeo yake tunashuhudia lugha 600 za kiasili zinapotea kila wiki.”

Ametolea mfano Tanzania akisema ina lugha za asili zaidi ya 123, kando ya Kiswahili kwa hiyo Ni vyema kutambua na kuzitunza lugha hizo.
Na sio lugha tu, tuna tamaduni nyinginezo kama, nyimbo na ngoma za kiasili, vyakula vitu vya urembo kama sanamu za kuchonga na michoro.

Inabidi serikali iingilie kati kuweza kutatua changamoto hii, ingawa sisi vijana pia tunatakiwa kuweka muda wa kurejea makwetu na kujua chimbuko letu. Ili tuweze kueneza kwa watoto wetu, asili yetu ambayo Ni fahari yetu.

Lakini pia, serikali inajukumu la kuhakikisha kuwa tamaduni zetu zinapewa kipaumbele sana, ili zisiweze kupotea. Njia mbalimbali zinaweza kutumika kuinua tamaduni zetu, kwanza kuanzisha mashindano ya tamaduni mbalimbali ambapo washindi watapewa zawadi nono, hii itasaidia kufanya watu waweze kujifunza tamaduni zao ili waweze kushiriki mashindano hayo.

Pili, kuanzisha maonyesho ya ya tamaduni mbalimbali, za makabila yote ya Tanzania. Siku au wiki moja iweze kutengwa ambayo itakuwa siku au wiki ya utamaduni na kabila, ambapo kutakuwa na maonyesho ya michezo, na mavazi, na mapambo mbalimbali na sanamu za kuchonga na kadhalika. Na katika maonyesho haya tunaweza kualika maraisi au viongozi na wageni wengine kutoka mataifa ya nje ili kuweza kushiriki katika wiki hii. Hii itaongeza uenezaji wa tamaduni zetu ndani na nje ya nchi.
 
Back
Top Bottom