MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,975
Msingi wa mafanikio ya siasa ni kuaminiwa na wananchi wengi. Huwezi kuwa mwanasiasa mwenye mafanikio ya kisiasa kama wananchi wengi hawana Imani na wewe.
Haijalishi imani hiyo kwa wananchi umeipataje lakini msingi wake ni kuongea, kuandika na kushawishi. Hapa ndio uwongo na propaganda huchukua nafasi yake ili kuishawishi jamii.
Katika masuala ambayo wapinzani wanashindwa kufanikiwa ni kutengeneza uwongo ambao hata mtu mwenye maarifa ya kawaida(common sense) hawezi kuuamini achilia mbali kuukubali. Kikubwa zaidi wanatengeneza uwongo ambao baadaye wanakuja kuutengua wenyewe.
Wanafalsafa wanasema mojawapo ya njia ya kushinda adui yako ni kujua udhaifu wake na kuushambulia kwa nguvu zote.
Wapinzani wetu badala ya kushambulia kwa nguvu zote udhaifu wa Rais Magufuli lakini badala yake wanashambulia uimara, ushapavu na uthabiti wake wakitegemea watashinda katika vita vya kisiasa. Hii vita hawawezi kuishinda badala yake watashangiliwa na kupigiwa vigeregere tu na manazi na wapambe wao badala ya wananchi wengi ambao wanatumia maarifa ya kawaida.
Moja ya udhaifu mkuu wa Rais Magufuli ni kutopenda urasimu (bureaucracy). Huu ni udhaifu mkuu kwa viongozi wanaoitwa ‘’Strongman leaders’’ ambao wanaongoza kwa kauli mbiu inayosema, ‘’If we can get a good result without regulating, let’s do that’’. Kwao urasimu ni njia inayochelewesha ajenda zao. Strongman leaders wana chembechembe za udikteta ambao haupatani vizuri na demokrasia halisi.
Hii haina mjadala kuwa uimara, ushupavu na uthabiti wa Rais Magufuli ni kupamabana na rushwa na ufisadi. Tafiti zote za kimataifa zinaonyesha uimara, ushupavu na uthabiti huo. Unaweza kusoma zaidi tafiti kwa kugonga LINK >>>Tanzania Corruption Index
Mbaya zaidi tafiti zinaonyesha wapinzani hawaaminiki ukilinganisha na taasisi ya Urais nchini. Kwa maelezo zaidi GONGA LINK>>>Do trustworthy institutions matter for development in Tanzania?
Nilishangaa kidogo kusikia wapinzani wakishupalia suala lililoibuliwa na Zitto Kabwe kuwa kuna upotevu/kutoonekana matumizi ya shilingi Trilioni 1.5. Pamoja na kwamba Zitto alikuwa mjanja katika matumizi ya maneno ambapo badala ya kusema WIZI bali alisema HAZIJULIKANI matumizi yake lakini ukweli ni kuwa alitaka kutumia hoja hiyo kama msingi wa kuonyesha wizi ndani ya serikali kuu hasa ofisi ya Rais.
Mbaya zaidi wapinzani wanakuja na uwongo ambao uko mbali na ukweli hata kwa mtu anayetumia maarifa ya kawaida (common sense). Hivi kwa nchi yenye bajeti ya Trilioni 30 halafu isijulikane matumizi ya Trilioni 1.5?. Kilichonichekesha zaidi ni kusikia wapinzani wanaongeza tena tarakimu na kusema badala ya shilingi Trilioni 1.5, kwa sasa kuna upotevu wa Trilioni 2.4. Huu uwongo hata kama wapinzani wakiusema sana hauwezi kuwa ni ukweli wa kuaminiwa na wananchi wengi pamoja na kwamba kuna dhana inayosema. ‘’uwongo ukisemwa sana hugeuka kuwa ukweli’’.
Kama kashfa ya shilingi bilioni 300 za Tegeta Escrow account ziliweza kuwafanya wahisani kutoa matamko na kusimamisha misaada nchini halafu eti shilingi Trilioni 2.4 wawe kimya. Akili ya kawaida tu anakuambia HAIWEZEKANI.
Kumshambulia Rais Magufuli kwa kutumia hoja za rushwa na ufisadi ni kupoteza muda na nguvu kwa sababu hata yeye anajua nguvu yake kubwa kisiasa ni kupambana na rushwa na ufisadi. Hawezi kuanza kuidhoofisha nguvu yake kuu iliyomuweka madarakani. Hili haliwezi kutokea.
Ni kweli kuna reallocation of funds ndani ya serikali lakini hili sio suala jipya katika serikali za Kiafrika ambazo zina matatizo mengi ya msingi huku bajeti yake inategemea 30% kutoka kwa wahisani. Hii hata wahisani wanajua na kwa msingi huu sio hoja kisiasa. Hoja ya msingi ni wizi wa mali za umma.
Wapinzani wanachotakiwa ni kushambulia madhaifu ya Rais Magufuli ili washinde vita vya kisiasa hasa ikichukuliwa hata resources za kutosha hawana lakini pia mafanikio yao yatategemea na uelewa wa wananchi juu ya faida na hasara za urasimu nchini.
VIDEO