Upotevu wa 2.4T: Wapinzani wajifunze kutengeneza uwongo ulio karibu na ukweli!

Kwani maelezo ya Asunga ndivyo majibu ya serikali yanavyotakiwa yatolewe kwa mujibu wa sheria? Yaani CAG anajibiwa kwa staili hii?
Uzuri Kamati ya PAC iko chini ya kambi ya upinzani.

Mwenyekiti wa Kamati alishatoa taarifa yao haya mengine ni yaleyale ninayoyasema kuwa wapinzani wanatakiwa watengeneze uwongo ulio karibu na ukweli.
 
Nianze kwa kumshukuru sana na kumpa pongezi nyingi MsemajiUkweli kwa bidii anayoionesha katika kutetea juhudi za awamu ya tano isiyokubali kukosolewa wala kupangiwa. Nina swali moja tu kwa MsemajiUkweli, hivi mpaka sasa tumetumia fedha kiasi gani katika manunuzi ya ndege! Nina hakika swali dogo kama hili halitakutatiza hata kidogo na kumbuka aulizaye ataka kujua.
 
Kwani kuna sehemu CAG kahoji 1.5T ktk ripoti yake?

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
Kinachofurahisha ni kuwa aliyeanzisha hoja ya 1.5T kwa sasa ameishahamia kwenye hoja zingine wakati waliobaki na hoja hiyo ni wale kasuku wa kisiasa.

Ndio maana nikasema, wapinzani wajifunze kutengeneza uwongo ulio karibu na ukweli.
 
Ninakubaliana kwa kiwango fulani na angalizo lako lakini tukumbuke kuwa hakuna mfumo usio na tatizo/matatizo hapa duniani.

Hoja ya msingi ni mfumo gani unaoendana na mazingira yetu ambao utakuwa hauna tatizo kubwa au matatizo mengi.

Wahenga walisema, mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Hii ina maana kuwa mfumo tuliolelewa kwa miaka zaidi ya 50 ndio ulivyotukuza kama taifa. Kuubadilisha mfumo kwa sasa sio rahisi kwa sababu umekomaa. Tukilazimisha kuubadilisha tunaweza kujikuta tunavunjika kama methali isemayo, samaki mkunje angali mbichi.
Huu wa sasa wa kuficha kila kitu ndo mbovu kuliko hata iliyopita. Mfumo wa kupaka rangi uchafu kama unavyojaribu kufanya wewe na wabunge wako ni hatari mno. Hata fedha za Tegeta Escrow mwanzoni mlijtahidi kuficha hivi hivi, usitudanganye kwamba ripoti ya Tegeta Escrow ilisomwa "from a white plate", ni uongo. Ilitoka kwa mbinde ingawaje angalau Kikwete alikuwa tayari hata kuvuliwa shati ili kifua kionekane. Lakini huyu kwa vile anataka watu waamini ni msafi kumbe kuna madudu kibao, hataki hata kuvuliwa koti. Ukweli uko wazi fedha zimepigwa. Na hili la kila sehemu nyeti kuwekwa "watoto wa Dada" matokeo yake mtayaona na kuyakiri ninyi wenyewe akishatoka madarakani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzuri Kamati ya PAC iko chini ya kambi ya upinzani.

Mwenyekiti wa Kamati alishatoa taarifa yao haya mengine ni yaleyale ninayoyasema kuwa wapinzani wanatakiwa watengeneze uwongo ulio karibu na ukweli.
Kuibwa na kutokujulikana zimetumikaje ni vitu viwili tofauti lakini kimoja inawezekana kikawa chanzo cha kingine.

Inawezekana kuwa hazijulikani zimetumikaje, lakini mwisho wa siku uchunguzi ukifanyika itagundulika kwamba kulikuwa na wizi ama ufujaji wa fedha za Umma.
 
Tuhuma za uongo lazima zichuje, kuna tofauti ya kauli mbiu za kampeni na tuhuma za uongo zinazotengenezwa na viwanda vya uongo vya wanasiasa. “Terrible teen “ ni uongo wa mchana wa Zitto, 1.5trilioni ni ujinga wa Zitto kushindwa kuelewa CAG report, watu 400 Mkiru pia ni kiwanda cha uongo cha Zitto. Na tuhuma zote hizi zitapotea na muda tu kwa sababu zimejengwa kwenye misingi ya uongo.

Kwahiyo uchumi wa gas ilikuwa ni kauli mbiu ya kampeni? Huna utetezi wa maana bali unalazimisha tu.
 
Huwa sihangaiki na maneno ambayo naona hayana Tija, watadanganywa hao , na ukiongelea tena udanganyifu wa kina Zitto unaendelea kuvuta attention ya watu kwa hilo,

Mi huwa ni vigumu kunilisha matango pori na niko hivo, wala sijawahi kufikiria kama Kuna upotevu wa 1.5 maana ni uongo mtupu
 
Mbona ripoti ya CAG hakuna sehemu iliyosema kuna wizi wa 1.5tr, na ripoti ya PAC pia imetoka na imefafanua hicho hicho, hakuna hata thumni iliyoibiwa ndio maana umemuona Zitto amefunga bakuli lake saivi.
Ni kweli report inaonyesha hakuna sehemu hela imeibiwa! Anachouliza CAG ni matumizi yake na siyo wizi! tofautisha vitu viwili
 
Tuhuma za uongo lazima zichuje, kuna tofauti ya kauli mbiu za kampeni na tuhuma za uongo zinazotengenezwa na viwanda vya uongo vya wanasiasa. “Terrible teen “ ni uongo wa mchana wa Zitto, 1.5trilioni ni ujinga wa Zitto kushindwa kuelewa CAG report, watu 400 Mkiru pia ni kiwanda cha uongo cha Zitto. Na tuhuma zote hizi zitapotea na muda tu kwa sababu zimejengwa kwenye misingi ya uongo.
Weka fact hapa acha mbwembwe! Kwanza elimu yako kiasi gani labda tuanzie hapo:rolleyes::rolleyes::rolleyes:
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom