Upotevu wa 2.4T: Wapinzani wajifunze kutengeneza uwongo ulio karibu na ukweli!

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,227
2,000
Msingi wa mafanikio ya siasa ni kuaminiwa na wananchi wengi. Huwezi kuwa mwanasiasa mwenye mafanikio ya kisiasa kama wananchi wengi hawana Imani na wewe.

Haijalishi imani hiyo kwa wananchi umeipataje lakini msingi wake ni kuongea, kuandika na kushawishi. Hapa ndio uwongo na propaganda huchukua nafasi yake ili kuishawishi jamii.

Katika masuala ambayo wapinzani wanashindwa kufanikiwa ni kutengeneza uwongo ambao hata mtu mwenye maarifa ya kawaida(common sense) hawezi kuuamini achilia mbali kuukubali. Kikubwa zaidi wanatengeneza uwongo ambao baadaye wanakuja kuutengua wenyewe.

Wanafalsafa wanasema mojawapo ya njia ya kushinda adui yako ni kujua udhaifu wake na kuushambulia kwa nguvu zote.

Wapinzani wetu badala ya kushambulia kwa nguvu zote udhaifu wa Rais Magufuli lakini badala yake wanashambulia uimara, ushapavu na uthabiti wake wakitegemea watashinda katika vita vya kisiasa. Hii vita hawawezi kuishinda badala yake watashangiliwa na kupigiwa vigeregere tu na manazi na wapambe wao badala ya wananchi wengi ambao wanatumia maarifa ya kawaida.

Moja ya udhaifu mkuu wa Rais Magufuli ni kutopenda urasimu (bureaucracy). Huu ni udhaifu mkuu kwa viongozi wanaoitwa ‘’Strongman leaders’’ ambao wanaongoza kwa kauli mbiu inayosema, ‘’If we can get a good result without regulating, let’s do that’’. Kwao urasimu ni njia inayochelewesha ajenda zao. Strongman leaders wana chembechembe za udikteta ambao haupatani vizuri na demokrasia halisi.

Hii haina mjadala kuwa uimara, ushupavu na uthabiti wa Rais Magufuli ni kupamabana na rushwa na ufisadi. Tafiti zote za kimataifa zinaonyesha uimara, ushupavu na uthabiti huo. Unaweza kusoma zaidi tafiti kwa kugonga LINK >>>Tanzania Corruption Index

Mbaya zaidi tafiti zinaonyesha wapinzani hawaaminiki ukilinganisha na taasisi ya Urais nchini. Kwa maelezo zaidi GONGA LINK>>>Do trustworthy institutions matter for development in Tanzania?

Nilishangaa kidogo kusikia wapinzani wakishupalia suala lililoibuliwa na Zitto Kabwe kuwa kuna upotevu/kutoonekana matumizi ya shilingi Trilioni 1.5. Pamoja na kwamba Zitto alikuwa mjanja katika matumizi ya maneno ambapo badala ya kusema WIZI bali alisema HAZIJULIKANI matumizi yake lakini ukweli ni kuwa alitaka kutumia hoja hiyo kama msingi wa kuonyesha wizi ndani ya serikali kuu hasa ofisi ya Rais.

Mbaya zaidi wapinzani wanakuja na uwongo ambao uko mbali na ukweli hata kwa mtu anayetumia maarifa ya kawaida (common sense). Hivi kwa nchi yenye bajeti ya Trilioni 30 halafu isijulikane matumizi ya Trilioni 1.5?. Kilichonichekesha zaidi ni kusikia wapinzani wanaongeza tena tarakimu na kusema badala ya shilingi Trilioni 1.5, kwa sasa kuna upotevu wa Trilioni 2.4. Huu uwongo hata kama wapinzani wakiusema sana hauwezi kuwa ni ukweli wa kuaminiwa na wananchi wengi pamoja na kwamba kuna dhana inayosema. ‘’uwongo ukisemwa sana hugeuka kuwa ukweli’’.

Kama kashfa ya shilingi bilioni 300 za Tegeta Escrow account ziliweza kuwafanya wahisani kutoa matamko na kusimamisha misaada nchini halafu eti shilingi Trilioni 2.4 wawe kimya. Akili ya kawaida tu anakuambia HAIWEZEKANI.

Kumshambulia Rais Magufuli kwa kutumia hoja za rushwa na ufisadi ni kupoteza muda na nguvu kwa sababu hata yeye anajua nguvu yake kubwa kisiasa ni kupambana na rushwa na ufisadi. Hawezi kuanza kuidhoofisha nguvu yake kuu iliyomuweka madarakani. Hili haliwezi kutokea.

Ni kweli kuna reallocation of funds ndani ya serikali lakini hili sio suala jipya katika serikali za Kiafrika ambazo zina matatizo mengi ya msingi huku bajeti yake inategemea 30% kutoka kwa wahisani. Hii hata wahisani wanajua na kwa msingi huu sio hoja kisiasa. Hoja ya msingi ni wizi wa mali za umma.

Wapinzani wanachotakiwa ni kushambulia madhaifu ya Rais Magufuli ili washinde vita vya kisiasa hasa ikichukuliwa hata resources za kutosha hawana lakini pia mafanikio yao yatategemea na uelewa wa wananchi juu ya faida na hasara za urasimu nchini.

VIDEO
 
Mr faru john

Senior Member
Dec 22, 2016
158
500
Kwa sisi wala karanga tunakuelewa barabara
Wakati unakula karanga bahati mbaya ukakutana na karanga chungu ama mbovu...,chakufanya ni kutema kilicho mdomoni na kuanza upya kula karanga tena kwa umakini mkubwa,ila si ivyo wengi wetu hufanya....
Tunachofanya ni kuongeza idadi ya punje za karanga mdomoni hadi hapo ladha ya sinto fahamu itapoisha mdomoni...
Tatizo si Raisi,tatizo ni MFUMO.
 
MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,227
2,000
Kwa sisi wala karanga tunakuelewa barabara
Wakati unakula karanga bahati mbaya ukakutana na karanga chungu ama mbovu...,chakufanya ni kutema kilicho mdomoni na kuanza upya kula karanga tena kwa umakini mkubwa,ila si ivyo wengi wetu hufanya....
Tunachofanya ni kuongeza idadi ya punje za karanga mdomoni hadi hapo ladha ya sinto fahamu itapoisha mdomoni...
Tatizo si Raisi,tatizo ni MFUMO.
Ninakubaliana kwa kiwango fulani na angalizo lako lakini tukumbuke kuwa hakuna mfumo usio na tatizo/matatizo hapa duniani.

Hoja ya msingi ni mfumo gani unaoendana na mazingira yetu ambao utakuwa hauna tatizo kubwa au matatizo mengi.

Wahenga walisema, mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Hii ina maana kuwa mfumo tuliolelewa kwa miaka zaidi ya 50 ndio ulivyotukuza kama taifa. Kuubadilisha mfumo kwa sasa sio rahisi kwa sababu umekomaa. Tukilazimisha kuubadilisha tunaweza kujikuta tunavunjika kama methali isemayo, samaki mkunje angali mbichi.
 
MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Oct 23, 2013
8,945
2,000
Kumbe na wewe unatetea wizi na ubadhilifu..!!

Ningekuona una akili walau kidogo kama ungepangua figures hapa kwamba CAG kwenye report yake kasema hii imetumika hivi na hii imetumika hivi..
Lakini uzi mzima kumsifia huyo Dikteta..sasa sifa kwa huyo kichaa wenu ndio kuhalalishe ubadhilifu wa 2.4Tril?

Uzi wote wapinzani..wapinzani..wapinzani..!!!

Pumbafff sana tu wewe.

Hivi ukiwa CCM kumbe lazima uwe mjinga eehh!

Mkuu Evarist Chahali njoo uone huku kuna mtu amehalalisha ule wizi wa 2.4Tril.
 
mtanzania1989

JF-Expert Member
May 20, 2010
3,166
2,000
JK alikuwa anapenda kusema kuna watu wana viwanda vya uongo, huu uzushi wa 2.4trilioni ni mojawapo ya mifano hai. Vingine ni kama “terrible teens “ , kuuliwa watu 400 mikoa ya kusini nk.

Kinachosikitisha ni uzushi huu wote wa propaganda za upotoshaji unachochewa na Zitto mwanasiasa kijana anayejiona msomi na ameelimika. Ubaya wa siasa za upotoshaji na ulaghai huwa hazikai, zinakosa uungwaji mkono wa watu wenye uelewa na zinakufa kifo cha asili. “Terrible teen” limeshasahaulika kwa kuwa ulikuwa uzushi, 1.5trillioni wanaona aibu kuitaja saivi kwa kuwa mwenyekiti wa PAC ambaye ni Mbunge wa NCCR Mageuzi ametoa ripoti inayowaumbua. Hata hiyo 2.4trilioni na yenyewe itakufa kifo cha asili tu.

Zitto ni mwanasiasa mzuri ila kadri siku zinavyoenda ile anazidi kuonyesha kuwa anategemea siasa za upotoshaji na majungu, siasa za propaganda na sio hoja. Siasa za namna hii inabidi uwe na manyumbu ambao ukiwarushia chochote wanabeba tu , kitu ambacho kwa ACT hana. Anazidi kujijengea sifa ya mtu asiyeaminika mbele ya macho ya welevu.
 
MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,227
2,000
Ni kweli kuna reallocation of funds ndani ya serikali lakini hili sio suala jipya katika serikali za Kiafrika ambazo zina matatizo mengi ya msingi huku bajeti yake inategemea 30% kutoka kwa wahisani. Hii hata wahisani wanajua na kwa msingi huu sio hoja kisiasa. Hoja ya msingi ni wizi wa mali za umma

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu;
Vipi?
 
sheiza

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
5,125
2,000
Ninakubaliana kwa kiwango fulani na angalizo lako lakini tukumbuke kuwa hakuna mfumo usio na tatizo/matatizo hapa duniani.

Hoja ya msingi ni mfumo gani unaoendana na mazingira yetu ambao utakuwa hauna tatizo kubwa au matatizo mengi.

Wahenga walisema, mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Hii ina maana kuwa mfumo tuliolelewa kwa miaka zaidi ya 50 ndio ulivyotukuza kama taifa. Kuubadilisha mfumo kwa sasa sio rahisi kwa sababu umekomaa. Tukilazimisha kuubadilisha tunaweza kujikuta tunavunjika kama methali isemayo, samaki mkunje angali mbichi.
Msemakweli mabadiliko ya mfumo yanafanyika ila tunaona wao ndio wa kwanza kupiga kelele na kulia njaa..wao huwa wepesi kutamka maneno na wanajisahau kuwa watamkayo ndio yafanyiwayo kazi na wao hao ndio wako busy kuyapinga matokeo ya hayo mabadiliko. Tuliona mbowe kipindi cha mwanzo akilalamika kanisani kuhusu wafanyakazi wasio na vyeti kupigwa chini..

Mifumo ya demokrasia za kutukana na kudhalilisha wengine..ilishachukuliwa kama jambo la kawaida..

Ukwepaji kodi na kuhodhi maeneo makubwa bila kuyaendeleza..wao ndio huwa wanakuja na kusema biashara zinafungwa, watu wanaonewa..sasa huto ukimuuliza mfumo uweje au umefanyaje hatakuwa na jibu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CHLOVEK

JF-Expert Member
Mar 8, 2017
537
1,000
Uki- reallocate kitu ni lazima ujue umekipeleka wapi, sasa hizi 1.5T mbona CAG mwenyewe hajaziona walipo zi- reallocate? Serikali yenyewe ilizitafuta kwa torch kuja kutuambia sijui zipo Znz na porojo nyinginezo. 960B kuzipeleka ikulu ili zisihojiwe na CAG nalo hili ni kutupiga changa la macho. Hili la kukwepa bureaucracy, mara nyingine hurahisisha matumizi mabaya ya fedha.
 
Bome-e

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
12,929
2,000
Msemakweli mabadiliko ya mfumo yanafanyika ila tunaona wao ndio wa kwanza kupiga kelele na kulia njaa..wao huwa wepesi kutamka maneno na wanajisahau kuwa watamkayo ndio yafanyiwayo kazi na wao hao ndio wako busy kuyapinga matokeo ya hayo mabadiliko. Tuliona mbowe kipindi cha mwanzo akilalamika kanisani kuhusu wafanyakazi wasio na vyeti kupigwa chini..

Mifumo ya demokrasia za kutukana na kudhalilisha wengine..ilishachukuliwa kama jambo la kawaida..

Ukwepaji kodi na kuhodhi maeneo makubwa bila kuyaendeleza..wao ndio huwa wanakuja na kusema biashara zinafungwa, watu wanaonewa..sasa huto ukimuuliza mfumo uweje au umefanyaje hatakuwa na jibu..

Sent using Jamii Forums mobile app
Kaa kimya tu,huelewi maana ya mfumo!!!Mifano yote haiendani kabisaaa na maana halisi ya mfumo imara!!!!
 
MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,227
2,000
JK alikuwa anapenda kusema kuna watu wana viwanda vya uongo, huu uzushi wa 2.4trilioni ni mojawapo ya mifano hai. Vingine ni kama “terrible teens “ , kuuliwa watu 400 mikoa ya kusini nk.

Kinachosikitisha ni uzushi huu wote wa propaganda za upotoshaji unachochewa na Zitto mwanasiasa kijana anayejiona msomi na ameelimika. Ubaya wa siasa za upotoshaji na ulaghai huwa hazikai, zinakosa uungwaji mkono wa watu wenye uelewa na zinakufa kifo cha asili. “Terrible teen” limeshasahaulika kwa kuwa ulikuwa uzushi, 1.5trillioni wanaona aibu kuitaja saivi kwa kuwa mwenyekiti wa PAC ambaye ni Mbunge wa NCCR Mageuzi ametoa ripoti inayowaumbua. Hata hiyo 2.4trilioni na yenyewe itakufa kifo cha asili tu.

Zitto ni mwanasiasa mzuri ila kadri siku zinavyoenda ile anazidi kuonyesha kuwa anategemea siasa za upotoshaji na majungu, siasa za propaganda na sio hoja. Siasa za namna hii inabidi uwe na manyumbu ambao ukiwarushia chochote wanabeba tu , kitu ambacho kwa ACT hana. Anazidi kujijengea sifa ya mtu asiyeaminika mbele ya macho ya welevu.
Mkuu
Ninakubaliana na comment yako kwa kiwango kikubwa.

Inashangaza sana kuona watu wanaojiita wachumi lakini hoja zao hazina hata mantiki ya kiuchumi.

Ninaamini wanajua kuwa wanadanganya au kupotosha lakini tatizo lao ni kuleta uwongo ambao hauna mantiki hata kwa mtu mwenye maarifa ya kawaida.
 
MISULI

JF-Expert Member
Jan 15, 2014
7,356
2,000
Kwani maelezo ya Asunga ndivyo majibu ya serikali yanavyotakiwa yatolewe kwa mujibu wa sheria? Yaani CAG anajibiwa kwa staili hii?
Kwani kuna sehemu CAG kahoji 1.5T ktk ripoti yake?

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom