NTIGAHELA
JF-Expert Member
- Jan 1, 2014
- 362
- 254
KISIASA, Mafia State humaanisha nchi kuwa na serikali jambazi. Ama inatenda uhalifu moja kwa moja kupitia vyombo vyake au inaendesha makundi hatari ya uhalifu.
Jana, Rais Samia alieleza kuhusu fedha za watuhumiwa wa kesi za uhujumu uchumi kufichwa China. Ni zile watu walilipishwa ili kununua uhuru wao kupitia makubaliano ya kufupisha mlolongo wa kesi na punguzo la adhabu, yaani plea bargain.
Baada ya Rais Samia, raia namba moja na Amiri Jeshi Mkuu, kutamka kwa ulimi wake kwamba fedha za plea bargain zilipigwa, sasa tupo kwenye wakati mzuri kuhitimisha kwamba nchi ilikuwa na serikali jambazi. Tanzania ilikuwa Mafia State.
Kesi za uhujumu uchumi ziligeuzwa chanzo cha mapato ya nchi. Watu walitishwa kukubali makosa vinginevyo wangeozea jela. Vile kesi hizo hazina dhamana. Basi, mtuhumiwa akatakiwa achague kutoa pesa au kuzoea maisha ya nyuma ya nondo.
Namfahamu mzee aliyefuatwa na kuambiwa kampuni yake iliacha deni la Yen za Japan 3,000 (Sh53,000). Deni hilo likapigwa faini kutoka Sh53,000 hadi kuwa Sh72 milioni. Akaambiwa alipe au akawe mgeni wa jela kwa kesi ya uhujumi uchumi.
Mzee hakuwa na pesa. Alishanyang'anywa kiwanda na nyumba mbili. Ikabidi aitishe michango ya ndugu. Walipoanza kulipa, walielekezwa kuingiza malipo kwenye akaunti binafsi.
Huo ukawa mwendo. Kampuni zilipewa mzigo wa faini za kodi, kisha fedha zikalipwa akaunti za watu binafsi.
Ilikuwa Mafia State. Polisi hadi JWTZ walitumika kudhulumu haki. Wenye maduka ya kubadili fedha walifilisiwa ndani ya saa chache. Walinyang'anywa fedha zao benki. Ofisi zao zikafungwa.
Ilikuwa serikali jambazi. Watu waliokuwa na fedha nyingi benki, walishangaa salio linasoma sifuri. Wafanyabiashara wengi wakaogopa kuweka pesa benki.
Serikali inayopora raia ni jambazi. Kwa bahati mbaya sana, Watanzania walisalitiwa. Walijua wana serikali, kumbe lilikuwa genge la wahalifu. Hawakuona aibu kuiba na kudhulumu.
Naijua story ya kiwanda cha uchapaji cha Business Printers Limited (BPL), kilivyoporwa, kisha kikawa kinachapa magazeti ya Cyprian Musiba bure. Hata kura za Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020, zilichapwa BPL kwa dhuluma. Wenye kiwanda wamefilisika hadi leo.