Mkamap umesema lakini.....
Naongeza neno la 'ubinadamu'na kuridhika'. Viongozi wetu, aliye na mali kidogo labda ana gari 8, nyumba (ghorofa)5, mashamba ekari 80, mifugo mingi sana(hakuna idadi), account yenye sh. 600m.
Watu hawa, wanafamilia ya watoto 2 au 3. umri wao wanakaribia kufa (hakuna atakaye ishi zaidi ya miaka 15). Magari yao hayatumiki wanatumia ya serikali pamoja na mafuta, madereva. Nyumba wanaishi za serikali kwa huo umri walionao, sasa nyumba zao wataishi humo lini? magari watayatembelea lini? acha nyumba zao, kuna nyumba hawawezi kuingia humo hadi upite mwezi 1 au 2.
Roho gani zisizo ridhika? Waafrika hatulidhiki au ni hawa mafisadi tu?Kuna watu wana shida rukkuki hakuna hata anayewaangalia, wao na matumbo yao.
Mikakati uliyoitaja kamwe haiitafanikiwa kama haya mashimo yasiyojaa yasipofukiwa (kung'olewa). Wafikie hatua waliridhike. Pita mikocheni, utaona roho zisizo ridhika.