Upofu huu utatumaliza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Upofu huu utatumaliza

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MkamaP, Oct 17, 2007.

 1. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2007
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Habari zenu
  Jamani Watanzania wezangu tuamkeni,tufungueni macho,tushikamane sote pamoja ,tuwe wa bunifu na tufanye kazi na uchumi utapaa zaidi ya rocket

  Mazingira ya kuendeleza chi ile bado yapo ,mianya bado ipo,sababu bado zipo hapa na maana sababu ya kuindeleza ipo na imefunuliwa bayana .
  hizi hapa ni sababu ya nchi kuendelea.
  1.watu
  2.amani
  3.malighafi
  4.kuchapa kazi
  5.ubunifu& kufikiri(Elimu)
  6.solidality &patriotism
  hizo sababu ndizo muhimili wa maendeleo kwa nchi yoyote duniani.
  kwa sisi watanzania tunapungukiwa vipengele no 4,5,na 6 ambavyo urekebishwaji wake ni mda mfupi na hatimaye Uchumi kupaa mwendo wa rocket tofauti na nchi nyingi za afrika zinazopungukiwa na vipengele vitatu mhimu vya mwanzo.

  Kuchapa kazi
  Hakuna nchi yoyote duniani ambayo inaweza kendelea kama watu wake watabaki vijiweni na kupiga sogo la maisha Bora hapa ukweli tutakuwa tunamuonea bure JK.Tuangalie china ilikuwa masikini sana jamaa mmoja kaingia madarakani kawapigisha kazi ya uhakika leo China inapaa mwendo wa ............

  Ubunifu & Fikra(Elimu)
  Ukweli hili tatizo ni kwa waafrika wote ila mie na stiki kwa ndugu zangu watanzania,
  Watanzania hatujaelimika awe profesa ama mtu wa elimu ya msingi na kutoelimika huku ndiko kunapelekea watu kutokuwa na fikra ktk mambo yao na hii ni sumu mbaya sana ktk suala zima la maendeleo.
  mfano saizi mtanzania yoyote akipata matatizo ama ya kifedha ama ya kijamii kitu cha kwanza kufikiri ninani ndugu mwenye fedha alitatulie tatizo lake, kama ndugu huyo tegemewa wakati huo akiwa hana fedha basi tatizo hilo linakuwa sugu kama ni mgonjwa atafariki.watanzania wezangu tuelimike tufukirie jinsi ya kutatua matatizo yetu na si kuangalia nani mwenye msaada.
  Tatizo hili ambalo naweza kuliita UGONJWA WA KUTOFIKIRI umemkumba hadi kiongozi wetu mkuu JK anamaatatizo nyumbani mwake ya kifedha badala ya kufikiri jinsi ya kuyamaliza yeye amekuwa akihaha kule na huku kutafuta msaada leo hapa kesho pale siku akirudi atakuta mgonjwa hana tena msaada zaidi ya kifo.
  Tuweni jamani wa bunifu na watu wakufikiri pia kunyanyambua mambo

  Solidality & patriotism
  Jamani hili hata sina hamu ya kulielezea
  watanzania hatuna hichi kitu na jinsi gani tukipate ni suala lako nami tufikri namna gani na kwa jinsi ipi ili tufanikishe hilo.
  kwa kukosa hilo ndio maana unaona leo jamaa anabeba mihuri ya wizara na kutimuka zake nchi za nje kutia mikataba ,CHIEF MANGUNGO yule wa USEVERO alikosa hiki kitu na kuwauza babu zetu.
  Kifupi Patriotism ni kuifanya kama wewe ni mtanzania basi TZ iwe mke/mtoto/mpwa/baba/mama wako yani unafanya kitu kwa moyo wote na hata kwa kujitolea maana unampa future nzuri mwanao/mkeo yani Tanzania.
   
 2. K

  Kalalangambo Member

  #2
  Oct 19, 2007
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkamap umesema lakini.....

  Naongeza neno la 'ubinadamu'na kuridhika'. Viongozi wetu, aliye na mali kidogo labda ana gari 8, nyumba (ghorofa)5, mashamba ekari 80, mifugo mingi sana(hakuna idadi), account yenye sh. 600m.

  Watu hawa, wanafamilia ya watoto 2 au 3. umri wao wanakaribia kufa (hakuna atakaye ishi zaidi ya miaka 15). Magari yao hayatumiki wanatumia ya serikali pamoja na mafuta, madereva. Nyumba wanaishi za serikali kwa huo umri walionao, sasa nyumba zao wataishi humo lini? magari watayatembelea lini? acha nyumba zao, kuna nyumba hawawezi kuingia humo hadi upite mwezi 1 au 2.

  Roho gani zisizo ridhika? Waafrika hatulidhiki au ni hawa mafisadi tu?Kuna watu wana shida rukkuki hakuna hata anayewaangalia, wao na matumbo yao.

  Mikakati uliyoitaja kamwe haiitafanikiwa kama haya mashimo yasiyojaa yasipofukiwa (kung'olewa). Wafikie hatua waliridhike. Pita mikocheni, utaona roho zisizo ridhika.
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Jun 14, 2017
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,427
  Likes Received: 22,349
  Trophy Points: 280
  Yeah
   
 4. mitale na midimu

  mitale na midimu JF-Expert Member

  #4
  Jun 14, 2017
  Joined: Aug 26, 2015
  Messages: 5,591
  Likes Received: 9,053
  Trophy Points: 280
  Tatizo letu wengi tunategemea wanasiasa kubadili maisha yetu...
  Bila kugundua mwanasiasa au chama cha siasa kina uhai wa miaka mitano kuendelea kuwepo hapo madarakani baada ya hapo ni majaliwa...
  Tushikamane sisi kwa sisi, tusichukiane kwa Misingi ya wanasiasa ambao wanatemporary positions.

  Katika vitu ulivyoorodhesha binafsi naamini katika Amani kwanza. Maana Kuna creative beings wamekimbia miradi yao kibiti kisa Amani.
  Kukiwa na Amani nitafanya shughuli popote nchini hata Bila kujihusisha na siasa zaidi humu jukwaani kama burudani kuchallenge wadau kidogo siku ziende...

  Mkuu mkama umeandika madini yenye thamani zaidi ya makinikia...
   
 5. Erickford4

  Erickford4 JF-Expert Member

  #5
  Jun 14, 2017
  Joined: May 22, 2017
  Messages: 799
  Likes Received: 527
  Trophy Points: 180
  ni kujituma tu tutajikwamua
   
Loading...