Upo wapi Anneth Benidicta?

Upo wapi Anneth Benidicta?

hivi aliyemuoa akipita anajisikiaje
 
Hi!

2014 ulinipenda pasipo chochote, sikuwa na kitu lakini hukujali, ulinipenda na umasikini wangu, licha ya kuwa ulikuwa mrembo Sana,
Nimekumbuka sauti yako nyororo na macho yaliyolegea.

Ulinichagua katika ya wanaume wengi walionizidi sifa za kihadhi, kifedha na hata kielimu.

Popote Ulipo Anastazia Benedicta jua Michael bado anakupenda,

Ulikuwa unaishi Kwa Aunt yako pale Kwenye Kota za mapolisi Moshi mjini, Nyumba yenu ilikuwa mkabala na uwanja wa mashujaa wa pale Moshi mjini.

Nimekumbuka mara ya mwisho tulivyokutana mida ya saa mbili chini ya lile sanamu la mwanajeshi pale uwanja wa mashujaa. Mpaka leo nakumbuka Marashi yako mpaka hivi leo.

Ile zawadi uliyonipa nimeitunza mpaka Leo Kama ukumbusho.

Anneth popote Ulipo nakuomba ujitokeze. Kama kuna mtu humu anamjua Aneth aliyekuwa anaishi na Aunt yake pale Kota za polisi uwanja wa mashujaa naomba amtaarifu Mick ninamtafuta Sana.

Aneth nakupenda Sana. Hata kama umeolewa, sitajali, ninachotaka nikuone roho yangu ipumzike jamani
Kama ulichoandika hapa kina ukweli na siyo changamsha genge basi haya ni matumizi mabaya ya mitandao.

Ulimwengu huu zipo njia nyingi sana ya kumsearch mtu kimyakimya kuliko njia hii unayotumia.

Wewe utajisikia vipi siku hapa JF atokee njemba na uzi wake wa kumsaka mpenzi wake wa zamani ambaye ndio mke wako?

Punguzeni upumbavu.
 
Andaa bajeti, na uende pointi zote alizokuwa anakaa huyo mpenzi wako, kuanzia kwenye nyumba, shule n.k
 
Anaitwa Anastasia Benidicta Ila alikuwa anapenda nimuite Aneth, Nimemkumbuka Sana Mpenzi wangu.

Popote Ulipo Aneth, nakuomba ujitokeze, najua umeolewa lakini nataka nikuone tuu roho yangu itulie
Wewe ulipomtosa ulifikiri hatapata wakufanana nae! Sasa unamwanika hapa ili uvunje ndoa yake? Manake kwa aunt yake unapajua uungwana nenda kaanzie hapo usiwe kivuruge
 
Kama ulichoandika hapa kina ukweli na siyo changamsha genge basi haya ni matumizi mabaya ya mitandao.

Ulimwengu huu zipo njia nyingi sana ya kumsearch mtu kimyakimya kuliko njia hii unayotumia.

Wewe utajisikia vipi siku haha JF atokee njemba na uzi wake wa kumsaka mpenzi wake wa zamani ambaye ndio mke wake.

Punguzeni upumbavu.
Nasisitiza huu ni upumbavu wa hali ya juu na wanaouendekeza ni vilaza ndio maana hata kuandika hawajui. Mademu zao waliowapenda wakiwa sijui chekechea uko wanataka kujikuta leo hii wamedata. How comes mtu walipendana sana na hajui namna ya kumpata katika ulimwengu wa sasa.

Hizi ni njia za kuchafuana, unaweza gombana na mtu uko unakuja humu kujifanya mlikuwa wapenzi na akatoa mimba. Mods wafute ujinga kama huu
 
Wewe ulipomtosa ulifikiri hatapata wakufanana nae! Sasa unamwanika hapa ili uvunje ndoa yake? Manake kwa aunt yake unapajua uungwana nenda kaanzie hapo usiwe kivuruge
Huyu ni mchawi wala hana mapenzi hapa. Kwa akili hizi huyo Aneth hampati
 
Back
Top Bottom