Uchaguzi 2020 Upinzani wakihubiri haki huwa wanamaanisha nini?

Nguruka

Senior Member
Dec 6, 2006
178
122
TANGU Jumatatu ya Oktoba 19,2020 hadi hivi sasa ninapoandika andiko hili, nashindwa kuelewa wala kupata jibu stahiki juu ya kile ambacho vyama vya Siasa nchini Tanzania vinamaanisha pale vinapozungumzia HAKI.

Wagombea na wanachama, wafuasi, wapambe na mashabiki katika vyama hivyo hasa vya upinzani vimekua vikiimba juu ya HAKI. Kauli Mbiu ya Mgombea Urais wa Chadema inasema “UHURU, HAKI na MAENDELEO YA WATU” lakini sijui inakuaje hapo kuhusu haki.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imezungumzia kuhusu HAKI ya Kupiga Kura. Na hii imeainishwa katika Ibara ya 5 (1) ambayo inaeleza ifuatavyo;

“Kila raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka kumi na minane (18) anayo HAKI ya kupiga kura katika uchaguzi unaofanywa Tanzania na wananchi. Na HAKI hii itatumiwa kwa kufuata masharti ya ibara ndogo ya (2) pamoja na masharti mengineyo ya Katiba hii na Sheria inayotumika nchini Tanzania kuhusu mambo ya uchaguzi”

Ukiangalia katika Ibara ya 5 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefafanua masharti ambayo yanapaswa kutimizwa kuwezesha raia kuitumia haki yake ya kupiga kura.

Katika Ufafanuzi huo inasema “Kila raia anayo haki ya kupiga kura katika uchaguzi iwapo ametimiza miaka 18 na kuendelea. Raia anayepiga kura lazima awe na akili timamu, awe ni raia wa Tanzania,awe hajatiwa hatiani kwa makosa fulani ya kijinai, lazima awe na kitambulisho cha kudhibitisha umri, uraia au uandikishwaji kwenye daftari la wapiga kura.

Katiba hiyo hiyo pia katika Ibara ya 5 (3) inaipa mamlaka Bunge la Tanzania kutunga sheria ya Uchaguzi ambayo itaweka masharti kuhusu mambo kadhaa ikiwepo;

Uanzishwaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, na kuweka utaratibu wa kurekebisha yaliyomo katika Daftari hilo; Kutaja sehemu na nyakati za kuandikisha wapiga kura katika Daftari hilo.

HAKI ya kupiga kura katika changuzi mbali mbali ndio mamlaka kuu aliyonayo mwananchi katika kuamua hatma ya uongozi na mwenendo wa nchi yake. Kila mwananchi anapaswa kuifahamu HAKI hii na kuitumia ipasavyo kila nafasi ya uchaguzi inapojitokeza ili kushiriki katika maamuzi juu ya mustakabali wa sasa wa nchi na maisha ya baadae.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliona umuhimu wa HAKI hii ya Mtanzania aliyekua amejiandikisha katika daftari la kudumu la Mpigakura lakini Mwananchi huyu kutokana na sababu moja ama nyingine kadi yake ya mpiga kura ameipoteza jambo ambalo linamkosesha haki ya kupiga kura.

Hivyo tume baada ya kusikia kilio cha wananchi juu ya hali hiyo na kwa kuzingatia kuwa taarifa za mtu huyu aliyepoteza kadi yake zipo katika kituo alichojiandikishia na atapigia hapo ikaamua kuruhusu vitambulisho vinavyotolewa na mamlaka za serikali kama vile Leseni ya udereva, Kitambulisho cha Taifa kutoka NIDA na Pasi ya kusafiria vitumike kama mbadala wa kumtambua mpigakura husika akifika katika meza ya Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi.

Tume imeona HAKI ya mtu isipotee ikaruhusu hilo, maana mtu huyu taarifa zake zipo katika daftari kituoni pale na hata nje katika orodha ya wapigakura mtu huyu atakuwepo na mawakala ambao ni wenyeji wa eneo husika watamtambua aweze kupiga kura yake na kuchagua viongozi wake.

Lakini nimeshangazwa na wananchi na wanaharakati na baadhi ya wanasiasa kuanza kusema njia hiyo ni mpango wa tume wa kuiba kura kwaajili ya Chama cha Mapinduzi.

Ah! Najiuliza hili linatoka wapi? Mbona tunahubiri HAKI lakini mwananchi ambaye alishakata tamaa kua atakosa HAKI ya kupiga kura sasa kapewa matumaini mnasema hiyo ikataliwe?
Labda niwaulize humu wapinzani hasa Chadema na ACT Wazalendo hivi katika hizo HAKI mnazohubiri jukwaani hiyo ya kupiga kura haipo?

Nilidhani tutafurahia na kuipongeza Tume kwa maamuzi hayo lakini ndo tumekua vinara wa kupiga uamuzi huo wa Busara wa Tume.
Niwasihi wale ambao wanapinga jambo hili, kuacha na kutoa fursa ya watanzania Wenzetu hawa kupiga kura na ili kutimiza HAKI ya ya kikatiba.

Asanteni.
VITAMBULISHO MBADALA.jpeg
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom