KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,590
- 4,601
Bado ubongo wangu unatafakari mengi sana juu ya upinzani wa Tanzania ambao umefikia mahali kuonekana ni chombo cha kuhamasisha ajenda za siri ambazo watanzania hawakubaliani nazo. Sura ya kwanza ya upinzani watanzania tuliujua kama wa maandamano na migomo lakini miaka hii michache ya Rais Magufuli umetusaidia kuujua upinzani katika sura ya pili ambayo hatukubahatika kuijua hapo kabla. Sura ya pili ya upinzani ambayo INABEZA, INALAUMU, INAPINGA kila jitihada chanya za serikali ya nchi hii.
Nikiendelea kutafakari Zaidi najikuta katika wimbi zito la kufikiri, kuwaza na kuwazua ni nini wapinzani wanataka serikali ifanye kwa ajili ya watanzani ? watanzania tulio wengi tunaona matokeo ya maamuzi tuliyofanya mwaka 2015 ya kumchagua Rais Magufuli kuwa Rais wetu , ni maamuzi yenye tija, ya hekima na busara nyingi. Rais ambaye anatekeleza aliyoahidi na anafanya yale wapinzani waliyokuwa wanayasema ni fahari kubwa watanzania.
Katika hili la kupinga na kubeza kila kitu, upinzani umekuwa tatizo kwa watanzania kusonga mbele. Ni hakika kabisa mpinzani wa kweli kutoka CHADEMA alikuwa ni Dkt.Slaa tu kwa sababu ameamua kuachana na utoto wa kisiasa wa CHADEMA wa kupinga yale aliyokuwa anayaamini na kuamua kuwa upande ule ambao unayafanya kwa vitendo nao ni CCM.
Aibu gani hii? Fedheha ya namna gani hii kwa watanzania? Hakika watanzania kuendelea kukumbatia upinzani huu usio na malengo ni kujirudisha nyuma enzi za ujima na ukabaila , enzi ambazo maendeleo yalikuwa hafifu. Watanzania wa sasa wanataka maendeleo ya kasi ya viwanda, kilimo, elimu, miundombinu , afya na uvuvi na kiongozi tuliyenaye sasa anajua mahitaji ya watanzania na anajitahidi kufanikisha kuyatimiza hata kama si kwa asilimia 100 ila kwa kiwango alichofikia tunaweza kusema maendeleo ya Tanzania yapo juu.
Kwa nini watanzania waendelee kushiriki utoto wa kisiasa wakati dira na muelekeo wa maendeleo chini ya Rais Magufuli ni mzuri na wenye nuru kwa kizazi cha sasa na vizazi vijavyo. Utoto wa kisiasa wa upinzani uliwatumbukiza watanzania kwenye siasa za matukio na purukushani badala ya siasa za utendaji ambazo kwa hakika awamu hii ya tano umezianika wazi.