Upinzani usipopata 50% ya viti vya ubunge Viongozi wote Wajiuzulu

Nyamgluu

JF-Expert Member
Mar 10, 2006
3,160
1,719
Habari wadau,
Tukiweka ushabiki pembeni ni dhahir serikali yetu chini ya CCM imefeli katika kuleta maisha bora kwa watanzania wengi. Kiwango cha kufeli hicho kinaweza kujadilika lakini swala la kufeli ni dhahir.

Vyombo vya habari vimeweza kuonyesha umma ufisadi,kiburi, dharau, wizi, ubadhilifu wa mali za umma, unyanyasaji, unyimwaji haki na upuuzi wa viongozi wengi wa CCM kiasi kwamba nina imani hakuna mtanzania mwenye akili timamu na asie na maslahi binafsi na CCM atakua tayari kumchagua mtu kama Muhongo, Komba nakadhalika na kumwacha mtu mwingine yeyote.

Yani haingii akilini kuwa ukamsimamisha Komba na Nyamgluu mbele ya walimu na wakulima walioshuhudia kupitia vyombo vya habari umalaya wa komba na mabinti wadogo, ubadhilifu wa hela BMK na kukandamiza haki, na wakaelezwa yote juu ya hawa watu (na nyamgluu akiwa hana historia yyt ya siasa) bado huyo mwalimu aliekatwa elfu 30 ya kujenga maabara na mkulima aliekosa soko la bidhaa zake akampigia tiki Komba na kumwacha Nyamgluu.

Ikitokea hivyo basi ni dhahiri Nyamgluu ni hafai kupita maelezo mbele ya hao wananchi. Mtu akiona Komba, Sanga ni bora kuliko wewe ni tusi kubwa sana.

Sasa basi kutokana na madudu ya CCM kwa kweli upinzani umerahisishiwa zaidi kazi, kama bado mwakani hawatafikisha asilimia 50 au hata 45 ya wabunge basi viongozi wote wajiuzulu na hata wale walioshindwa na akina Sitta,Lukuvi KIHALALI waache siasa na wafanye kazi zao.

Nikisimama kugombea jimbo na Hawa Ghasia halafu ashinde kwa kishindo kuna haja ya mimi kujiangalia mara 2 kama kweli siasa ni wito wangu.

Hakuna kipindi CCM imedhoofika kama sasa chini ya dhaifu. Ikifanikiwa kupita hapa bila pigo la nguvu ninafikiri inaweza imarika huko mbele na kufanya ndoto za upinzani kuendelea kuwa ndoto tu.
Hivyo ndivyo nionavyo mimi.
 
wewe ni mwalimu au mkulima, mbona unawasemea wenzako? Nakuona kama mmoja wa wale wafuasi wa Reginald Mengi vile?
 
wewe ni mwalimu au mkulima, mbona unawasemea wenzako? Nakuona kama mmoja wa wale wafuasi wa Reginald Mengi vile?

Sijakuelewa. Ila kukujibu mimi ni mwalimu pamoja na mkulima. Wafuasi wa Reginald Mengi ndio wakoje?
 
Mkuu umefanya nikumbuke ile kasi ya Lowassa 2006-2008, ebu jaribu ku contemplate saizi tungekuwa wapi, is not a secret saizi tungekuwa mbali sana sana.
 
hauna 45% au zaidi chini ya SLAA, MBOWE na LIPUMBA.

Basi kama wana nia ya kweli na maendeleo ya nchi na wananchi wake na sio uchu wa madaraka hawana budi kuachia nyadhifa kiroho safi ifikapo hapo baada ya uchaguzi.
 
Basi kama wana nia ya kweli na maendeleo ya nchi na wananchi wake na sio uchu wa madaraka hawana budi kuachia nyadhifa kiroho safi ifikapo hapo baada ya uchaguzi.

SLAA na MBOWE wana majini UONGOZI kama vile walivyo na majini Mahaba, kuachia ni ndoto.
 
Sijakuelewa. Ila kukujibu mimi ni mwalimu pamoja na mkulima. Wafuasi wa Reginald Mengi ndio wakoje?
Mkuu hii biashara ingekufaa sana ila mambo ya uchambuzi ni zero kabisa.
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    414.8 KB · Views: 83
unajikana kuwa wewe siyo mfuasi wa Reginalg Mengi, wakati maandiko yako yanaonesha ni mfuasi wake

Kumtaja kwangu Muhongo negatively ni kutokana na kukingia kifua wawekezaji wa nje kwenye swala la gesi na kusema sisi tunaweza viwanda vya juisi tu, badala ya kupanga mikakati ni namna gani tunaweza miliki na kuendesha rasilimali zetu wenyewe.
Kama bado hatuwezi si iachwe tu kwani inaoza ile? Kuliko kuwapa wageni watuibie na kujiimarisha wao huku wakitukandamiza sisi wananchi.
Sasa sijui hapo nakueje mfuasi wa Mengi. Kweli mmefikia hatua hio ya kukosa uzalendo kiasi hicho? Unafikir maendeleo ya dhati yataletwa na mwekezaji wa nje au wa ndani? Nitajie nchi zilizoendelea kwa kukabidhi rasilimali zao kwa wawekezaji wa nje?
 
unajikana kuwa wewe siyo mfuasi wa Reginalg Mengi, wakati maandiko yako yanaonesha ni mfuasi wake

watu masikini huwachukua watu wenye nacho, na mtu mpumbavu humchukia mwenye akili, na mtu asiye na elimu humchukia mwenye elimu ,sijuwi upo upande gani au we nifukara wa mali na elimu?
 
Back
Top Bottom