Upinzani unaelekea shimoni

wandamba

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
510
839
*UPINZANI UNAELEKEA SHIMONI*

*Na Shilatu E.J*

Mwaka 1992 Serikali ilianzisha mfumo wa vyama vingi hapa nchini na mwaka 1995 ulifanyika uchaguzi mkuu wa kwanza katika mfumo wa vyama vingi.

Tofauti na inavyotarajiwa upinzani kukua nchini badala yake unaelekea shimoni na dalili ya hayo ni kuona vyama vya upinzani vikishindwa kila siku kwenye chaguzi; Umoja na ushirikiano baina yao ukizidi kupungua; viongozi wa vyama vya upinzani wakiwemo waandamizi, Madiwani na Wabunge wamekuwa wakihama vyama vya upinzani na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi.

Kwa wanaofuatilia kwa makini siasa hapa nchini watakubaliana nami upinzani nchini ulikuwapo haswa miaka ya nyuma, ambapo upinzani kulijaa magwiji wa siasa tofauti na sasa.

Wakati wa enzi za ukoloni Tanganyika ilikuwa na chama cha kisiasa kijulikananacho kama TAA (Tanganyika African Association) kilichoanzishwa mwaka 1923. Baadaye kikaja chama cha TANU (Tanganyika African National Union) kilichoanzishwa mwaka 1954 kwa upande wa Bara; na kwa upande wa Viziwani (Zanzibar) kulikuwa na chama cha Afro Shiraz Party (ASP) ambavyo kwa pamoja chama cha TANU na ASP viliungana mnamo tarehe 12/05/1977 na kuunda Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Tangu enzi za utawala wa serikali ya awamu ya kwanza iliyokuwa ikiongozwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ambaye mwenyewe alikiri uwepo wa upinzani mkali toka kwa vyama vidogo vidogo vya kiuharakati ambavyo kimsingi vilikuwa ni kama vyama kwani mfumo wa kipindi kile ulikuwa ni wa chama kimoja.

Kwa wanaokumbuka vizuri watakubaliana nami kuwa kulikuwa na vikundi vya kiuharakati kama vile United Tanganyika Party kilichokuwa kikiongozwa na Hussein Juma; kulikuwa na African National Congress (ANC) kilichokuwa kikiongozwa na Zubeiry Mtemvu (Baba yake na Mbunge wa Temeke CCM wa kipindi kilichopita, Abbas Zubeiry Mtemvu); Civic Movement chake James Kabaro Maparara; People Democratic Party kilichokuwa kikiongozwa na Kasanga Tumbo; pamoja na Chama cha AMNUT kilichokuwa kikiongozwa na Sheikh Yahya Hussein.

Kundi na vikundi hivi kuzidi kushamiri na kutaka kuielemea Serikali ya awamu ya kwanza kwa hoja na si vurugu (kama ilivyo sasa) vilivunjwa rasmi na Bunge la Tanzania mnamo mwaka 1965.

Serikali ya Rais Karume ilikuwa ikikabiliwa na upinzani mkali toka kwa kundi la Kamati Huru ya Mageuzi (KAMAHURU), Muslim Brotherhood na kundi la Bismillah.

Mara baada ya 1965 watu walioendeleza mapambano ya dhidi ya serikali zilizokuwapo madarakani wakizipinga kwa hoja ni kama vile Joseph Kasella Bantu, Tuntemeke Sanga, Modestus Choga, Kassanga Tumbo na Chifu Abdallah Fundikira ambao wote walikuwa magwiji wa hoja na utaratibu wa kudai madai yao dhidi ya Serikali.

Miaka ya nyuma siasa ilikuwepo, wanaharakati walikuwepo ambapo wanaharakati ama wanasaiasa wa zamani walikuwa ni weledi kuliko hata wa sasa. Uweledi unaanzia kwenye ukweli, namna wanavyousimamia ukweli na jinsi ya kuuwasilisha ukweli ambapo wanasiasa wa zamani walijaaliwa uweledi na ukweli tofauti na wanasiasa wa sasa.

Viongozi wa zamani walijenga vyama pasipo kuwagawa Watu kwa misingi ya udini, ukabila na ukanda. Tangu enzi za zamani CCM toka TANU ilijenga taasisi yenye ushawishi kila pembe ya nchi, makundi yote ya dini, ya kikabila, kikanda, Wafanyakazi, Wakulima na Wafanyabiashara. CCM haijawahi kutekeleza msingi huu wa kuwaunganisha Watu tofauti na ambavyo vyama vya upinzani vimeendelea kuwagawa Watanzania kwa misingi ya ukabila, udini na ukanda.

Siku hizi Wapinzani wamekuja na mtindo mpya wa kugomea chaguzi ili kutaka wanayoyataka yasikike. Lakini wanasahau kugomea uchaguzi hakujawahi kumsaidia Laila Odinga kule Kenya, wala kumsaidia Maalim Seif kule Zanzibar. Na hata hakujawahi kuisaidia Chadema kwenye chaguzi hizi ndogo.

Kususa uchaguzi ni sawa na kumsusia Nyani shamba la mahindi, utavuna mabua na hatimaye kufa njaa kabisa.

Upinzani nchini unazidi kuelekea shimoni kutokana na utekelezaji safi wa ilani ya uchaguzi na wakati mwingine Rais Magufuli amekuwa mjanja na msikivu zaidi kwa kutekeleza vilio vya wapinzani na hatimaye kuwafilisi ajenda. Mathalani kupinga ufisadi, mafisadi kupandishwa mahakamani na mengineyo ni mifano hai ya kuhama ajenda na kuipa turufu kubwa CCM.

Wenye hekima na busara wanaona vyama vya upinzani nchini vimepoteza dira na mwelekeo na utawala wa Rais Magufuli unazidi kujizolea umaarufu kutokana na kuwa watekelezaji wazuri ilani ya uchaguzi na kikubwa kuwa sauti na watetezi wa Wanyonge.

Wapinzani hawa wameamua kutelekeza ajenda zilizowainua na sasa kuamua kuishi kwa matukio. Kitendo cha Wapinzani kutekeleza ajenda ya ufisadi kumewaonyesha kwa jamii namna wasivyo na msimamo na kukosa nia ya dhati ya kutafuta dola.

Jambo lingine linalowapeleka shimoni vyama vya upinzani nchini ni kutokana na kukosa umoja, upendo baina yao. Ni jambo la kawaida kusikia Chadema wanapambana na ACT Wazalendo, Chadema wanapambana na CUF ni mambo ya aibu yanayowapeleka shimoni.

Kama haitoshi ugomvi wa ndani kwa ndani kwenye vyama vya kisiasa vimezidi kuzorotesha umoja, mahusiano na nia ya pamoja na hivyo kujikuta wakijipeleka shimoni.

*Na Shilatu E.J*
Januari 15, 2015
 
CCM endeleeni tukupandisha hasira tu!

Tunasubiri tume huru ya uchaguzi sio hii ya CCM halafu tuwafanyizie vibaya sana 2020.

Nipo nakula standup comedy kusahau machungu ya hii serikali:

Ungeweka na simu kabisa.Uchaguzi wa wabunge kura zote mlizopata ni only 11% bado upinzani unaingia shimoni anyway pole
 
Hawo wanyonge ni akina nani ?

Milioni hamsini kila kijiji kimeshapata ?

Vipi kuhusu viwanda vingapi vimejengwa na kuanza kazi ya uzalishaji ?

Mwisho uongo na njaa zako usitupofushe na sie baki nayo mwenyewe
 
Who is shilatu BTw!!?
 
42 - 1,
Rais ni JPM,
Majority bungeni ni wa JPM,
Popularity votes mitaani kutokana na vyombonvya utafiti chadema ni 19%, this is pathetic. Wakati JPM anapaa.

Hivi unaelewa swali uliloulizwa?

Sijaomba matokeo ya uchaguzi mlioiba mwaka 2015.

Umeombwa utuambie ni lini wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walikataa Tume Huru ya Uchaguzi?

Hilo ndilo swali.

Hivi shule ulikua unajibuje mitihani maana hapa umejibu kitu ambacho hukuulizwa!
 
Imekataliwa na Watanzania lini?

Who,where and when?

Toa fact..
Acha kujitoa ufahamu, hilo swali ulilouliza hapo juu umeshasahau mara hii??
Hivi unaelewa swali uliloulizwa?

Sijaomba matokeo ya uchaguzi mlioiba mwaka 2015.

Umeombwa utuambie ni lini wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walikataa Tume Huru ya Uchaguzi?

Hilo ndilo swali.

Hivi shule ulikua unajibuje mitihani maana hapa umejibu kitu ambacho hukuulizwa!
Dah!
 
Acha kujitoa ufahamu, hilo swali ulilouliza hapo juu umeshasahau mara hii??

Dah!

Umenipa matokeo ya "UCHAGUZI" ambayo ni irrelevant here!

Lini hoja ya Tume Huru ilipigiwa kura na Watanzania ikakataliwa?

Vyovyote upendavyo,jibu ulililotoa ni la hovyo kwa sababu unamaanisha kwamba kumbe kuichagua CCM maana yake ni "Kukataa Tume Huru ya Uchaguzi"?

Yaani kwa lugha ingine ni kwamba CCM haipendi tume huru,inapenda tume ya uchaguzi inayoendeshwa na CCM.Ndio maana yake.Yaani CCM inasimamia na kupenda sana tume isiyo huru.

Ndio maana hampendi Tume Huru,mnaogopa upinzani ndio maana yake!

Nishawaelewa,ndio maana CCM ni wachawi!
 
Polisiccm+ccm+rc+dc+ded+nec = upinzani, siku hao washirika wa ccm wakijiengea kuwa sehemu ya vyama vya siasa, ccm ni wepesi kama manyoya
 
Back
Top Bottom