Upinzani penetration...

Tatizo siyo upinzani sijui mjini sijui vijijini huo ni uwongo kama mjini upinzani wanakubalika mbona hawajapita. Tatizo ni tume huru ya uchaguzi na hilo haliwezi kuwa jukumu la upinzani hilo ni jukumu la watanzania wote ili maamuzi yao yaheshimiwe yasichakachuliwe. Tume huru ya uchaguzi inatakiwa kupigiwa kelele na watanzania wote wanaopenda haki na wenye hofu ya Mungu. Marehemu Mkapa alishaanzisha hiyo hoja lakini haijulikani ilizimika tu kama vile haina umuhimu

Tume ya taifa inatakiwa iwe hoja ya kudumu na ifanyike kampeni ya kutosha kuhamasisha watu pamoja na kuelimisha kwanini Kuna umuhimu wa kuwa na tume guru ya uchaguzi.
 
Yaani hayo masanduku ya kura zilizopigwa tayari + kutokuruhusiwa mawakala wa CHADEMA vituoni, ulitegemea nini? CHADEMA wakipata hata 1 nitashangaa.
Kwa visingizio hamjambo. Hata mngekuwa na mawakala elfu kichapo kilikuwa palepale. Kuishinda CCM inabidi ipasuke kwanza,kama mlivyobahatisha 2015 badala ya kufunga goli mlikazia kuzungusha mikono na viuno tu. Kwa style yenu ya kujenga tumbo la mwenyekiti wenu kuwaongoza watanzania sio leo wala kesho. Magufuli akiingia sahauni siasa mpaka uchaguzi 2025 hapo mtakuwa mmelegea kama mlenda. Anyways, mmevuna mlichopanda.
 
Ccm.....naomba mungu awachukue wote.
 
Lissu fungua charity usisubiri mpaka uchaguzi ufike ndio utembeze bakuli,,,,,

This is the way to get support unawavuta wanachama unafanya chama kinenepe😊😊😊, kinakua kikubwa both in numbers ya wanachama pamoja na income.... after all Sio lazima uwe serikalini ndio uhudumie watanzania
 
Mambo yanarudi kule kule. Uchaguzi umekwisha wote mnafungiwa kufanya shughuli zozote za kisiasa au kijamii kasoro ccm.
 
Kuna tofauti ya kushinda na kutangazwa mshindi, watanzania bado hawajafikia level ya kupigania ushindi wao, naamini iyo siku ipo karibu
 
Kwahiyo yaliotendeka jana umeona yapo sawa? Na ndio uchaguzi wa vyama vingi unavyoendeshwa?
 
Unadhani ni rahisi kiasi hicho? Kuwa mpinzani ni kazi ngumu sana Tanzania. Nani kwanza anakula uhuru wa kuanzisha hiyo charity, serikali ipi imruhusu Lissu kuanzisha charity? Waulize tu kuanzisha media house yenye nguvu waliweza? It's not easy kuwa mpinzani kwa nchi za kiafrika, labda tuhamie huko mbelez.
 
Mimi nadhani bila tume HURU, (ambayo kwa sasa kupiata itakuwa kupanda mlima Kilimanjaro), sahau upinzani kuwa chama dola.
 
Ninauhakika hata hiyo charity haiwezi kusajiliwa na wakiisajiri basi haitakaa muda wataifungia kwa madai ya kujihusisha na siasa, solution wajipenyeze watu kwenye taasisi za ulinzi na usalama ili siku ikifika wasimame nao kwani huko ndio kwenye backbone ya ccm
 
Mkuu ukishakua karibu na watu ni rahisi kuwa mobilise watu wadai tume huru, you cant just sit far na kusema tunahitaji tume huru .. lazima uwa engage kwanza... Kama upinzani hauhitaji charity unahitaji nini mkuu?? Funguka
Wanasema sio kazi za mbunge hizo.

Ndio hoja yao wakiwa wanaomba kura.
 
kama serikali ya Magufuri watakubari. hawakawii kusema charity inafadhiliwa Na mabeberu.
 
Ukitaka kumpiga nyoka piga kichwani, pamoja na ulioleza yote, tuanze na moja tu. Tume ya uchaguzi iundwe upya ili pamoja na watu wengine iwe na wawakilishi wa vyama na wakurugenzi waondolewe kwenye kusimamia uchaguzi. Huo ndio utakuwa mwisho wa CCM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…