Upinzani kuchukua nchi labda baada ya miaka 1000

Upinzani kuchukua nchi labda baada ya miaka 1000

Nebuchadinezzer

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2018
Posts
1,403
Reaction score
2,550
Wasalaam wanaJF,

Kwanza nianze kwa kujisemea kuwa binafsi sio muumini wa chama chochote cha siasa ila siasa ni maisha yangu.

Kwa mambo yanayoendelea hususani kwa hawa viongozi wetu wa vyama pinzani mi nadhani upinzani bado sana kuchukua madaraka.

Ukiwaangalia viongozi hawa ni watu wazima kabisa ila mambo wafanyayo yana utoto mwingi sana.

Eti mtu anayetegrmea kuchukua nchi na kuwa mfariji mkuu anachekelea watu wake kuzuiwa kuuza mahindi nje ya nchi.

Anafurahishwa na tetesi za kuugua kwa rais aliyechaguliwa na wananchi.

Anaungana na upande wa watesi wetu waliotunyonya miaka nenda rudi.

Mwingine ni kiongozi ila ni mlevi. Sifa ambaye maandiko ya Mungu yanasema kuwa mlevi ni mtu mpumbavu haijalishi ni nani.

Kwa hali kama hii napendekeza Magufuli aongezewe miaka 10 baada ya 2025 ili anyooshe mapito yaliyopinda. Na ikiwezekana atawale mpaka afie madarakani maana huyu rais ni chaguo la Mungu na ni mzalendo kweli kweli!
 
Hivi kati ya aliyesababisha yakazuiwa na anayechekelea kuzuiwa nani hana akili hapo? anayehoji kuhusu kuugua kwa kiongozi (nyie mnasema anachekelea) na anayeficha taarifa za kiongozi mgonjwa nani mwenye matatizo.

Ni ibara gani ya katiba ya jamhuri ya muungano inayozuia kiongozi kunywa pombe?
 
Mimi ningekuelewa ungesema kuwa hawajajiandaa kuongoza kwa kuwa hawapo tayari kutumia fursa zinazojitokeza. Mfano kupoteza muda kujadili ibara ya 37 badala ya kutangaza kuwa kuanza sasa wao ndio watawala, hapo tungeelewana.
 
Ngoja nifuatilie kama na wafuasi wa Bob Wine nao wana akili za funza kama wa hapa kwetu...ama kweli Tanzania hatujawahi kuwa na Wapinzani wa kweli, kuna kikundi cha wasaka tonge na wajinga wengi! Kwa akili hizi CCM itaongoza milele!
 
tufanye sawa ma ccm yataongoza miaka 1000, ndio kusema ukoo wako wote pamoja na mmeo mtapata "maendereo" kama ya mabeberu wa kure "uraya"?!.
 
Kura ziliibiwa nyinyi wenye kura mkiwa wapi? Mmelala au? Sasa tukiwapa nchi nayo si itaibiwa? Basi hatuwapi nchi mpaka mjipange vizuri na kujitambua tusije tukaibiwa nchi jumla jumla!!
Mimi binafsi nilipigwa bila hatia
 
Mbona miaka 1000 umewapa michache sana!??? Labda SKWEA YA KIPEO CHA PILI CHA ELFU 🙂 Upinzani wala hata hautaki kuchukua nchi, bali kuchakachua nchi --- upigaji madili ndiyo referendum & ilani ya Chama cha Demoghasia & Maombolezo plus mshirika wake aliyepoteana. Anywezs, mia tano tena!!!
 
Kwa hali kama hii napendekeza Magufuli aongezewe miaka 10 baada ya 2025 ili anyooshe mapito yaliyopinda. Na ikiwezekana atawale mpaka afie madarakani maana huyu rais ni chaguo la Mungu na ni mzalendo kweli kweli.!
Aongezewe na nani ? Niwapeni dokezi tuu, madaraka aliyopewa raisi wa Tanzania yanamzidi hata mfalme wa nchi duniani. Nakupeni dokezi tuu, kabla hamjaanza harakati ya kumuongeza kwanza mtafakari hili.

Niseme kwa nchi za EA, nawapongeza sana Kenya. Jamaa wako mbali sana katika safari yao ya kuelekea maendeleo na demokrasia. Tanzania ikiwa wananchi wao bado wanamawazo ya namna hii, naona ndio itachukua hio miaka 1000
 
Back
Top Bottom