Upinzani hauna tija kwa watanzania

Upinzani hauna tija kwa watanzania

2kimo

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2014
Posts
2,029
Reaction score
2,072
Kushindwa kwa upinzani kushika dola mwaka huu ni uthibitisho uliodhahri kuwa umekosa tija na kujenga matumaini kwa watanzania.

Kuna sababu nyingi unapolizungumzia hili lakini kwa ufupi naomba tuangalie vipengele hivi;

1. Kukosa dira inayoeleweka
Upinzani ulikosa kabisa muelekeo hassa baada ya ujio wa Lowasa na kuondoka kwa Slaa.

Watanzania walioahidiwa mabadiliko thru M4C walikuwa wakijua fika changes walzokua wanazitaka ni za utawala bora na si vinginevyo! Kwa bahati mbaya utawala bora ukawa hausemeki tena, na jibu likawa shida sio mtu bali ni mfumo, bila ya kujali kuwa mifumo inaharibiwa au kuboreshwa na watu! Mbaya zaidi mwisho ikawa hata mkituwekea jiwe tutalixhagua hapo nadhani watu walishakubali kuwa mgombea wetu hafanani na chochote tunavhohubiri! Kinyume chake ni ccm kuleta all justification kuwa mgombea wao ndiye mtu ambaye watanzania walikuwa wakimtafuta!

Simply ccm walisema kweli chama chetu hakipo safi Ila sio mfumo Bali ni kikundi tu cha watu akiwemo huyo aliyekuja kwenu na wengine wachache! Kama mfano wa Magufuli wa kitanda na kunguni! Nadhani watanzania walipima gharama ya dawa ya kuua wadudu au kununua godoro jipya na kitanda!

2. CCM ilikuwa katika migogoro mikubwa zaidi ya 6 lkn bado wapinzani walishindwa kutumia fursa.
A. Sakata la escrow
B. Tatizo la umeme
C. Kipindupindu
D. Ukosefu wa ajira kwa vijana
E. Malipo ya watumishi wa umma
F. Kuporomoka na uratibu mbovu wa elimu (nursery-university)

Kila mgogoro hapo juu ni topic on its own, lakini kwa kutojipanga wapinzani hawakutoa majibu kwa wananchi, yaani kwa kifupi bado wananchi waliona kuwa hata huko napo watakuwa wanabahatisha tu. Ccm ilikuwa imeshimdwa mno ktk maeneo hayo, lkn Lowasa hakuja na jibu hata la tatizo moja.

3. Muungano wa mashaka
Pamoja na kuunganisha vyama vinne bado upinzani ulishindwa kuiporomosha ccm, na changamoto kubwa ilikuwa n ndoto ya kuiangusha ccm bila kujali msingi unaosimamia umoja wao! Ishara za kutoaminiana zilipoanza ndani yao, ccm ilitoosha kutumia hizo propaganda!

Lakini ikumbukwe kuwa wakati wapinzani walipokuwa wakiungana ccm ilikuwa inamegeka, so ukawa walishindwa kuiangusha ccm ktk muda ambapo ccm ilikuwa dhaifu kuliko wakati wowote kwenye historia!

4. Mbinu chafu na kutumia ujinga kama mtaji
Siasa za mwaka huu, zimetumia sana kampeni chafu, ikiwemo vurugu, kashfa kwa wagombea, mipango ya wizi wa kura na ulaghai kwa wapiga kura au baadhi ya maofisa!

Wote ccm na ukawa waliyafanya yote hapo juu, kitu hiki kwa chama tawala ndio sehemu ya ushahidi wake tunaosema watoke, sasa inapotumiwa chama kichanga kinaxhotaka kuingia madarakani sijui inatoa picha gani.

All in all wapinzani wanapaswa kujipanga na kutorudia makosa haya tena, otherwise wapinzani jina hili la upinzani litakuwa ni sehemu ya maisha yenu!
 
Yani hiyo yote inamaanisha kuwa, mipango bila akili bado ni sifuri2. Watanzania hawataki utawala wa hisia, tunataka utawala bora na makini. Ndio maana ukawa (Ukiwa) wanahaja ya kujipanga upya kwaajiri ya uchaguzi wa mwaka 2025. Samahan lakn
 
Tume huru lazima iwepo ikiwa na wawakilishi kila kutoka kila chama. Hapo nguvu ya upinzani itaonekana.
 
Tume huru lazima iwepo ikiwa na wawakilishi kila kutoka kila chama. Hapo nguvu ya upinzani itaonekana.

Tume huru haina uwakilishi wa vyama!
Kuna ofisi hazina siasa! Tume si chombo cha kisiasa hakina na wala hakihitaji uwakilishi wa kisiasa!
Lakini kabla kuangalia matatizo kwa tume hebu angalia jinsi ukawa walicyojipanga!
Uhuru wa tume unataka kwenye serikali tu au hadi ktk vyama! Kuna mfumo rasmi wa uchaguzi na uteuzi ukawa? Lakini hakuna uchaguzi uliokuwa huru na fair kama wa mwaka huu! Sidhani kama kuna tume huru Africa inayoweza kupiga kazi ya ajabu sana! Tume nyingi Africa ambazo ni excellent zitakuwa kama hii yetu au hii inaweza kuwa around 80% ya any best tume unayoifahamu hapa Africa!
Mje na mipango zaidi ya kuinvest kwenye lawama!
 
kiukweli mwakahuu angekuwa dr SLAA jukwaani akiusema ufisadi vilivyo CCM walikuwa na wakati mgumu.maana hili la akina tibaijuka lilikuwa ajenda kubwa kwa wapinzani lakini sijui walilishwa nini nikashangaa kimya hawauzungumzii tena ufisadi
 
Tume huru haina uwakilishi wa vyama!
Kuna ofisi hazina siasa! Tume si chombo cha kisiasa hakina na wala hakihitaji uwakilishi wa kisiasa!
Lakini kabla kuangalia matatizo kwa tume hebu angalia jinsi ukawa walicyojipanga!
Uhuru wa tume unataka kwenye serikali tu au hadi ktk vyama! Kuna mfumo rasmi wa uchaguzi na uteuzi ukawa? Lakini hakuna uchaguzi uliokuwa huru na fair kama wa mwaka huu! Sidhani kama kuna tume huru Africa inayoweza kupiga kazi ya ajabu sana! Tume nyingi Africa ambazo ni excellent zitakuwa kama hii yetu au hii inaweza kuwa around 80% ya any best tume unayoifahamu hapa Africa!
Mje na mipango zaidi ya kuinvest kwenye lawama!
Kwa hakika wewe unaishi nwezini, na siku moja moja ukishuka duniani huwa unaishia Hollywood.
 
Tume huru lazima iwepo ikiwa na wawakilishi kila kutoka kila chama. Hapo nguvu ya upinzani itaonekana.
Huo ndiyo ukweli na ndiyo siri inayofanya CCM inaendelea kupata ushindi kila unapofanyika uchaguzi.
Kama nchi yetu isipopata Katiba mpya ambayo itaruhusu kuwa na Tume huru za uchaguzi basi tuitarajie CCM kuendelea kuitawala nchi hii hadi mwisho wa dunia.
Kwa hiyo wito wangu kwa vyama vyote vya upinzani ambavyo viko serious na mustakabali wa nchi walibebe suala la upatikanaji wa Katiba mpya yenye kuruhusu Tume huru za uchaguzi kuwa ndiyo agenda kuu.
Kwa maana wabunge wote wa upinzani waliopata fursa ya kuingia mjengoni wahakikishe pamoja na uchache wao walione suala la kuwa na Katiba mpya inayotokana na maoni ya wananchi yaliyomo kwenye Rasimu ya Warioba kuwa priority no 1, priority no 2 na priority no 3 hata ikibidi wawe tayari hata kuzichapa 'kavukavu' mle bungeni ili mradi tu kuwezesha Katiba hiyo ndiyo inayopaswa na Bunge ili ikapigiwe kura za maoni na wananchi.
Kama itatokea CCM wakalazinisha wananchi tuipigie kura ya maoni Katiba yao iliyoandikwa na Chenge, hiyo itakuwa sawa na watanzania kuikabidhi CCM hati miliki ya kuitawala nchi hii milele na milele Amen.
 
Sitachoka kulisema hili:

Kwa kadri tume ya uchaguzi ikiendelea kuundwa na CCM hakuna mgombea wa upinzani atakayeiona ikulu.
 
Tume huru lazima iwepo ikiwa na wawakilishi kila kutoka kila chama. Hapo nguvu ya upinzani itaonekana.

Uchaguzi Zanzibar u meharibiwa na tume yenye makamishina 4 wanasiasa toka ccm na cuf na watatu wasio na vyama Tulionya mapema tume huru haiwezi kuwa na wanasiasa ni kuzalisha migogoro
 
Wapinzani hawana tatizo.
Tatizo lipo kwa mwenye nchi.
 
Kwa katiba hii gandamizi huwezi kuona umuhimu wa upinzani hapa TZ,
 
CCM hawajashinda uchakuzi wametangazwa tu na lubuva. Nakuhakikishiya CCM hawawezi hata siku moja kushinda uchaguzi ulio huru na haki tume yote ni miCCM mitupu wewe mfano nzuri ni Zanzibar jeshi lililoletwa Zanzibar hata tulipopigana na Uganda halikupelekwa jeshi kubwa hivyo yote nilazima CCM ibakiye madarakani. CCM hawataondoka kwenye madaraka kwa kura nawashasema mara nyingi tu CCM wanatumiya ubabe tu .Bila ya mapanga CCM wataendelea kutumiya ubabe tu.
Kama kweli CCM wanajiamini waweke tume huru ya uchaguzi.
 
Tatizo si Lubuva tatizo ni pandikizi wa CCM ndani ya Tume(Kapilima).
 
Wapinzani aina ya Mbowe wanastahili kuuawa popote pale
 
Watanzania suala la ufisadi sio suala muhimu tena wamekubali liendelee kwani hawana uwezo Wa kulizuia hivyo hata Dr. Slaa angelihubiri singemsaidia kupata kura .Mbona kina Change , Mama Tibaijuka wamechaguliwa kwa wingi Wa kura.?
 
Back
Top Bottom