Binadam bora na mstarabu haangalii amefanya kipi cha kufurahisha watu bali asifanye nini cha kuumiza watu.
Baadhi ya makabila na mila Afrika ,zamani watoto wenye ulemavu walitupwa kwenye miamba mirefu na watu kwa kusgawishiwa kuwa hilo lilikua jambo bora walishangila na kuona kuwa ni kitu cha kawaida.
Hali iliendelea hivyo kwa karne nyingi na mwafrika aliyepinga aliadhibiwa vikali.
Walipinga kwa siri sana.
....Mpaka wakoloni weupe walipokuja ndipo walipoanza kupinga na kupambana na mila potofu zilizotumika kuua watu na kudhalilisha watu.
Karne 21 kuna watu bado wanafurahia kuuawa kwa binadam wenzao mfano ni Msibamsibamkuu. Huyu anatangaza na kuhamasisha kuuawa kwa watu ili iwe kafara ya maendeleo.
Haya ndiyo yaliyowafanya waafrika wapenda haki kuanzisha harakati za ukombozi na kupambana kwa nguvu zote na kuwatoa wakoloni katili weupe .
Hata hivyo kwa bahati mbaya wazungu walifanikiwa kuwaweka madarakani wakoloni weusi kwa katiba,sheria,mitizamo,mifumo na mitizamo ile ile waliyokuwa nayo.
Mpaka leo Afrika hawajapata kile babu zatu walichokidai toka kwa wakoloni ,yaani Utu ,haki na usawa.
Mareli,mabarabara na majumba hayawezi kuwa mbadala wa maisha ya ndugu zetu.
Kama kuna mzalendo kuliko wote anayependa madaraja ,Mareli,mandege,mabarabara kuliko uhai wake na wa familia yake tunaomba ajitokeze afanye jambo dogo sana ili reli zijengwe kwa jasho lake pia yaani atoe pesa zake zote na mali zake zote na mshahara wake ubaki kwa ajili ya chakula cha kubangaiza alimradi maendeleo ya vitu yawepo huku familia yake ikiishi maisha ya shida. Wafanye hivyo kwa sababu uhai sio jambo la maana kama madaraja. Wangeweza kufanya haya kwa ajili ya kulijenga taifa ningewaamini na ningewapinga wale wanaosema maendeleo yaanze kwa wote kuwa na maisha bora na kulinda uhai na maisha ya wote kwa usawa bila kujali vyama.
Naamini Mali walizonazo makada wa wa chama kikubwa na kikongwe Barani Afrka wakiziuza na kupeleka pesa zao zote hazina ili zikatumike kujenga miundo mbinu basi Tanzania ingekua paradiso kwa mabustani na miundo mbinu mizuri. Na maskini wasingeumizwa na makodi makodi kila siku.
Lakini watu hao wasiojali maisha ya binadam wenzao Pesa na mishahara minono kwao ni muhimu lakini kwa wananchi pesa sio muhimu na hawatakiwi wawe nazo bali wafunge mikanda. Wao wana maisha mazuri kwa pesa za walipa kodi. Wao wana Mali nyingi kupitia mishahara na maslahi mazuri waliojiwekea na wanagombania kupata vyeo ili wasikose maslahi halafu wanatudanganya kuwa tufunge mikanda.
Vitabu vya dini vinasema usimtendee mwenzako kile ambacho hungependa utendewe .
Ningewakubali wakoloni na mabeberu weusi kama wangejitoa muhanga kulijenga Taifa kwa kujitoa kwa moyo hata miaka kumi tu.
Wangeamua kukataa magari ya kifahari yanayoligharimu taifa na kuwaumiza walipa kodi wasio na hata baskeli. Wangekataa kukimbilia kujenga maofisi yasiyozalisha chchote badala yake wakajenga viwanda.
Wangepunguza misururu ya misafara inayotumia mafuta malaki ya lita. Mafuta yanayoagizwa kutoka nje kwa kodi za wananchi . Misafara ya kwenda kuzindu choo kimoja cha shimo.
Ningewaona wazalendo na wenye nia ya dhati kwa kutumia TV ya Taifa kuhamasisha haki na kukataa kizazi kinachonufaika na dhulma.
Ukishangilia Wizi wa kura na kunyanganya wagombea formu za kugombea ili mtoto wa chama fulani apate kwa dhulma ni kuhamasisha kizazi cha kihalifu. Kizazi kisichopenda haki,kizazi chenye ubaguzi,kizazi kisicho na usawa, kizazi chenye kuamini kuwa bila dhulma huwezi kupata mafanikio.
Ndio maana chaguzi za Afrika zimegubikwa na ushirikina.
Sent using
Jamii Forums mobile app