Upi umri sahihi wa binti kuhama nyumbani?

Upi umri sahihi wa binti kuhama nyumbani?

Maki J

Senior Member
Joined
Mar 22, 2017
Posts
154
Reaction score
162
Wasalamu JF members,kuna mtu ametoka kupost uzi akiuliza upi umri sahihi wa kijana kuhama nyumbani na kwenda kujitegemea, comments nyingi zinawalenga wanaume Sanaa....

Hivyo naomba kujua mtt wa kike akiwa na umri gani anapaswa kuhama nyumbani? Au yy hapaswi kwenda kujitegemea mpaka aolewe?

Mm ninaumri wa miaka 24 nimepanga mwishoni mwa Mwaka huu nataka niondoke nyumbani na kwenda kujitegemea mwenyewe nianze kulipa bills na vitu vingine,tayari Nina adia ya biashara namalizia kukusanya mtaji tu,karibuni mchangie mada naomba kama kuna mabinti wanao jitegemea mje mtupe uzoefu na chang'amoto za kusimama binti kama binti.

NB:Tafadhali naomba muwe wawazi sipendele mabinti wanaojitegemea na kulipa bills kwa kutegemea kuhongwa au kuchuna,naomba uzoefu wa wale hardworking girls.
Karibuni

Sent from my ALE-L21 using JamiiForums mobile app
 
Kwani huolewi?
Huoni wivu kuwa Mama yako anaishi na Baba yako ila wewe wtaka ondoka ishi mwenyewe?
Muulize Mama yako kama ni sahihi wewe kuondoka enda ishi mwenyewe
 
Wasalamu JF members,kuna mtu ametoka kupost uzi akiuliza upi umri sahihi wakijana kuhama nyumbani na kwenda kujitegemea, comments nyingi zinawalenga wanaume Sanaa....

Hivyo naomba kujua mtt wa kike akiwa na umri gani anapaswa kuhama nyumbani? Au yy hapaswi kwenda kujitegemea mpaka aolewe?

Mm ninaumri wa miaka 24 nimepanga mwishoni mwa Mwaka huu nataka niondoke nyumbani na kwenda kujitegemea mwenyewe nianze kulipa bills na vitu vingine,tayari Nina adia ya biashara namalizia kukusanya mtaji tu,karibuni mchangie mada naomba kama kuna mabinti wanao jitegemea mje mtupe uzoefu na chang'amoto za kusimama binti kama binti.

NB:Tafadhali naomba muwe wawazi sipendele mabinti wanaojitegemea na kulipa bills kwa kutegemea kuhongwa au kuchuna,naomba uzoefu wa wale hardworking girls.
Karibuni

Sent from my ALE-L21 using JamiiForums mobile app
Hakuna Umri sahihi wa Mtoto wa Kke kuhama Nyumbani bali Mpaka kuwe na Sababu za Kuolewa ndiyo anafanyiwa Sendoff ikiwa ni Official muagano wa Mtoto Wa kike kutoka kwa Wazazi wake. Zaidi ya Hapo hakuna Umri Sahihi wa Yeye Kuhama Nyumbani kwa Wazazi wake.
 
Kama huna kazi wala biashara dada tulia nyumbani kwenu, mcheza kwao hutunzwa atii...Or else utajikuta umeanza kujiuza kirejareja
Leo uko kwa hasan atakupa 50elfu ya kusogeza siku kesho kwa hamis anakupa 30elfu ya umeme na maji
Weekeend kwa John atakulipia kodi
 
Kuondoka nyumbani eti kisa tu unepata vijihela. na kwenda kupanga kwa msichana sio adabu.

Ondoka nyumbani unaenda masomoni au kwenye ajira(hapa Kama umepangiwa mbali na nyumbani)

Kinyume na hapo sio heshima.

Kuondoka nyumbani na kuelekea kwa mwenzi wako huku ukiwa Una Baraka zote za wazazi ndio heshima kubwa kwa mwanamke.
 
Ila Mimi ua sishauri watoto wa kike waame kwao, ila napendekeza wawe independent lakin sio mpaka watok kabisa nyumbani sio busara sana,.. Ila tu akiolewa

Sent from my SM-G950FD using JamiiForums mobile app
 
Ni mawazo hafifu ya wachache kati ya wengi... lakin ni vema mwanamke kama umemaliza chuo ukahama nyumban ukaanza kujitegemea ingawa utakua huru zaid juu ya mapenz kitu ambacho kinaweza kuleta hitilafu kama haupo vizur kifikra
 
Mtoto wa kike kuishi kwenu ndo utaratibu, sema sasa hivi ni sababu ya kuajiriwa kwenye mikoa tofauti, ila hata kama umeajiriwa karibu na kwenu ishi na wazazi wako tuu...

Kupanga kuna vishawishi vingi mnoo...
 
Me nadhani umri mzuri wa kwenda kuanza maisha ni pale bint anapoolewa bila kujali ana umri gani wa kuzaliwa.
Pili,binti anapozalia nyumbani lazima ahame akajitegemee.
Kishajipachika unungayembe huyo. Kuendelea kukaa nyumbani kwa utovu wa maadili kiwango hicho anaweza kuharibu kabisa mustakabali wa wadogo zake ambao ni samaki wabichi wanaoendelea kukunjwa.
Sisi wengine tusio na mfumo dume, watoto wote wana haki sawa mbele ya wazazi. Hata mtoto wa kiume akijichanganya kuzaa na kimada wakati akiishi nyumbani na habari ikathibitika, nitamfukuza hima, kawa kidume huyo akapambane na maisha, shenzy kabisa.
 
Mimi nilikaa nyumbani hadi siku ya harusi ndiyo nilihama.
Mimi nadhani binti ni vyema ukae kwenu kama hamna sababu ya wewe kuhama.

Sent from my HTC ONE using JamiiForums mobile app
 
Unamalizia kukusanya mtaji wapi huko?
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] imebidi nicheke....umenichekesha mkuu...namanisha kunakibarua nafanya ndo nakusanya mtaji

Sent from my ALE-L21 using JamiiForums mobile app
 
Hakuna Umri sahihi wa Mtoto wa Kke kuhama Nyumbani bali Mpaka kuwe na Sababu za Kuolewa ndiyo anafanyiwa Sendoff ikiwa ni Official muagano wa Mtoto Wa kike kutoka kwa Wazazi wake. Zaidi ya Hapo hakuna Umri Sahihi wa Yeye Kuhama Nyumbani kwa Wazazi wake.
Mkuu hata kama hufanyi kazi (hujaajiriwa) uendelea kuishi nyumbani so matumizi unamwomba baba au mama yani kama pedi,losheni,kusuka,vocha,nauli za kutoka out na marafiki,kununua nguo na viatu hivyo unamwomba mzazi???

Sent from my ALE-L21 using JamiiForums mobile app
 
Kama huna kazi wala biashara dada tulia nyumbani kwenu, mcheza kwao hutunzwa atii...Or else utajikuta umeanza kujiuza kirejareja
Leo uko kwa hasan atakupa 50elfu ya kusogeza siku kesho kwa hamis anakupa 30elfu ya umeme na maji
Weekeend kwa John atakulipia kodi
Mrembo Rubi kama umesoma vizur nimesema ninampango wa kuanzisha biashara

Sent from my ALE-L21 using JamiiForums mobile app
 
Nasaka jiko

Sent from my TECNO_W4 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom